Fedha za Radar Kurudishwa: Mgogoro kati ya BAE, TZ na UK

Anadai kwamba hizo hela ziliibiwa serikalini. Ingekuwa bora zaidi kama wale walioziiba walikamatwa na kupelekwa mahakamani. Nakubaliana na ABB kutoa hizo fedha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kwa sababu ingepewa serikali zingepotelea mara nyingine tena kwenye mifuko ya wajanja.

Hata hao waingereza walilazimika kuchunguza kwa kina kupata kujua kwamba kulikuwa na njama za kuiibia serikali ya Tanzania na ndipo walipochukua hatua na pengine kama siyo ule utapeli ambao BAE waliwafanyia wamarekani wakapigwa ile fidia ya kufa mtu basi issue hii isingejulikana. Sasa suala hapa ni kwamba aliyeibiwa ndiye wa kulipwa. Let's face it!
 
Serikali imeshindwa kuwafungulia mashtaka wahusika wala kuwawajibisha hadi serikali ya Uingereza ikafungua kesi,tena kuna watu kama mama Short aliamua kujiuzulu uwaziri kwa kutoridhika na mauzo hayo ya Rada,Leo hii bila aibu serikali inasema inazitaka hizo hela ni zake inazitaka, kwa kweli serikali hii inatutia aibu sana
 
Serikali imeshindwa kuwafungulia mashtaka wahusika wala kuwawajibisha hadi serikali ya Uingereza ikafungua kesi,tena kuna watu kama mama Short aliamua kujiuzulu uwaziri kwa kutoridhika na mauzo hayo ya Rada,Leo hii bila aibu serikali inasema inazitaka hizo hela ni zake inazitaka, kwa kweli serikali hii inatutia aibu sana

sijui hao waandish waliuliza hlo swali?
Kama mi ningekua journalist,ningembana membe awataje wakwapuaj,au aseme zilikwapuliwaje?sio leo aongee had mishpa na mate yamtoke
 
Membe ni Mnafiki kama alivyo bosi wake Kikwete, kama anauchungu na nchi basi wakatae kulipa dei la Dowans na kuwafikisha Mafisadi wote mahakani bila ya kufanya hivyo ni usanii, hizo pesa ni bora BAE wasizilipe kwa maana kuwa wakina Membe watakuja kuzukwapua kama walivyofanya kwenye EPA. wanatafuta pesa za 2015 Magamba.

BAE we dont need Money for now, keep your money away from Criminal Magamba. Ukiwapa watazitafuna zote na Watanzaia watazisikia tuuuuu
 
Kwa nini usijitahidi tu kueleweka ili watakaochangia waone tatizo ni nini. Yeye Membe anatoa msimamo wa serikali kwa sababu ukweli ni kwamba Serikali ndiyo iliyoibiwa fedha hizo na ndiyo inayostahili kurejeshewa fedha hizo. Uhalali au kukosa uhalali na fedha hizo hakutokani na jinsi serikali ilivyolishughulikia suala hili kwa sababu mpaka kabla ya uamuzi wa mahakama kuwatia hatiani BAE hauna ambaye angeweza kusema kwa uhakika kwamba kulikuwa na usanii. In any case waliofanya wizi huo walifanya in their personal capacities na hiyo haiwezi kuwa basis ya serikali kunyimwa fedha hizo. Hizi ni fedha ambazo serikali ilitapeliwa na anayetakiwa kurudishiwa ni yule aliyetapeliwa. Sasa cha ajabu hapo ni nini?

mkuu yaelekea ujui kilichotokea, hii issue ya kununua RADA kuna mama claire short alikuwa waziri wa uingereza , wizara ya maendeleo ya Afrika yeye alijiudhuru kupinga serikali yetu na ya Blair kuhusu manunuzi ya hiyo RADA.
Waziri wako wa maji Prof Mwandosya na Mkuu wa kaya kipindi Hicho Mkapa na huyu Kikwete alikuwa mambo ya nchi. bunge watu walipinga na uingereza hii issue ilipingwa lakini hiyo timu niliyokutajia hapo juu wakalazimisha kununua kwa maslahi yao binafsi.
Mungu mkuu mambo yamelipuka baada ya serikali ya BROWN kuingia madarakani , TAKURUKU waliwahi kusema hakuna rushwa, lakini waingereza kwa sababu wao ndio wanatujaza note kwenye bajeti zetu walikomaa nayo. mambo sasa yako wazi.
hakuna aliyetapeliwa kila kitu kilikuwa wazi lakini wao wakaziba masikio, kinachotutafuta ni baada ya kumpoteza raia mmoja wa india aliyekuwa hapa bongo maana ndiye aliyetoa mgao kwa viongozi wetu.
Kama kwenye serikali ni wadilifu na wanaona uchungu na hizo pesa tulizolangulia Prof mwandosya anafanya nini serikalini? kwa nini asijiudhuru maana kesi imekwisha na mambo ni kwamba tulidhurumiwa kwa uzembe wake au kupewa mgao? Kikwete kwa nini haombi radhi maana alikuwa nao kwenye baraza la mawaziri.
toa hoja kama unajua kiini cha tatizo sio kila kitu unapaswa kulopoka na kutetea kwa sababu tu kinawahusu ccm.
wewe unadhani waingereza ni wajinga ?
hiyo hela ni yao anyway wao ndio wahisani wakubwa wa nchi hii, hivyo wanajua wanachofanya,
membe na genge lakini ni wala posho tu hakuna kitu hapo.
mimi nilitegemea wao kama serikali kutoa kauli ya kuchukua hatua zidi ya wazembe/wezi wa hizo pesa na sio kujifanya wanataka madawati!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Serikali ya Tanzania imepinga vikali uamuzi wa kampuni ya silaha ya Uingereza –BAE Systems wa kulipa fidia ya Paundi milioni 29.5 za Uingereza kwa Tanzania kupitia asasi isiyo ya kiserikali badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja serikalini kufuatia kukamilika kwa kesi ya rushwa ya ununuzi wa Rada.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Kampuni ya BAE System iliiuzia Tanzanai Rada kwa gharama ya Paundi milioni 41 za Ungereza wakati gharama halisi ilikuwa Paundi milioni 12.

Akitangaza msimamo wa serikali leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amesema, uamuzi huu unaenda kinyume na msimamo wa serikali yetu uliotaka fidia hiyo irejeshwe serikalini.“Fedha hizo ziliibwa kutoka serikalini na hazina budi kurejeshwa serikalini,” amesema.

Tamko la Serikali limekuja miezi sita baada ya uamuzi uliotolewa na Jaji Bean wa mahakama ya Southwark ya Uingereza Desemba 21,2010 kutoa uamuzi kuwa BAE kulipa Paundi milioni 29.5 kwa wananchi wa Tanzania.

Jaji Bean alitoa uamuzi huo baada ya kutorishika na na maelezo ya makubaliano ya Ofisi ya Makosa makubwa ya jinai ya Uingereza SFO na BAE.
Kwa mujibu wa Waziri Membe, kampuni ya BAE system badala ya kulipa fedha hizo moja kwa moja kwa wananchi wa Tanzania, imeamua kuunda jopo litakalojumuisha watu kutoka ndani mwake kuishauri jinsi itakavyotumia fedha hizo kupitia kwa asasi isiyo ya kiserikali ya uingereza na sio kwa serikali ya Tanzania.

“Msemaji wa BAE amenukuliwa na Ubalozi wa tanzania nchini Uingereza akisema kampuni yake inaongozwa na sera ya kutoa misaada ya kihisani kwa asasi zisizo za kiserikali tu. Kwa msingi wa sera hiyo, kampuni hiyo haitaweza kulipa fidia hiyo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania,” amesema.

Waziri Membe amesema kuwa uamuzi hu wa BAE unalengo la makusudi kuonyesha sura ya kutokuamini mpango wa pamoja wa Serikali za Tanzania na Uingereza ulioelezea jinsi fedha hizo zitakavyotumika.

“Serikali ya Tanzania ilikusudia kutumia fedha hizo kununua jumla ya vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 katiak shule 16,000, kununua madawati 200,000 kwenye shule zilizo na upungufu wa madawati na kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, kujenga vyoo 2,900’ amesema.

“BAE wanajaribu kujikosha mbele ya asasi mbalimbali zisizo za kiserikali za Uingereza baada ya kukosolewa sana kwa kashfa ya rushwa na kutoka sasa kuonekana kwamba inawajali zaidi Watanzania kukliko serikali yetu,” ameseam.
Waziri Membe ameeleza kuwa kampuni hiyo silaha ikikaidi kutoa fedha hizo moja kwa moja kwa serikali ya Tanzania, hakuna asasi isiyo ya Kiserikali ya Uingereza itakayopewa fedah hizo na kuruhusiwa kuja nchini.

Imeandikwa na Joseph Ishengoma
MAELEZO, DAR ES SALAAM

Hii ni aibu sana kwa serikali kulilia pesa ya BAE, wajue kuwa pesa ile si change kwani makubaliano ya awali yalikuwa ni kuuziana radar ya GBP 12m kwa GBP 41m. BAE wamefanya jambo bora sana kuinyima hazina pesa hizo, kama mpango wa kujenga madarasa ulikuwa ni bora zaidi kwa nini serikali hii hii iliweka kipaumbele kwenye kununua radar?, je na zile pesa walizotaka kuwalipa dowans nazo je?, mradi wa vitambulisho pia?, inaonesha ni jinsi gani walivyochanganyikiwa na pesa hii ambayo kiukweli si change bali ni humanitarian aid iliyotakiwa kutolewa kwa watanzania ili kuua shauri la rushwa lilikokuwa linaiandama BAE. Tena BAE wanatakiwa kutoa pesa hizo kwa asasi za kiraia za UK ambazo zipo well regulated na kufanya mambo yao transparency ikiwemo ku-Publish statements of financial activities and Trustees annual reports, filing annual returns to the Charity Commission. Kitu ambacho kitakuwa kinaeleza kila penny ilivyotumika badala ya kuwakabidhi Serikali wakalipie madeni ya mishahara na posho zao za semina elekezi. Kama Membe atakataa Asasi hizi kuja kufanya kazi Tanzania basi tutashauri uanzishwe mfuko wa kusomeshea watanzania wasio na uwezo nje ya Tanzania ambao mwananchi ataomba kupitia British Council ambayo itamuunganisha na asasi iliyokabidhiwa pesa hizo na akiwa na vigezo anapewa scholarship kuliko kuwakabidhi watu wanaodai change wakati hakuna mtu hata mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa kulisababishia taifa hasara ya GBP 29 m!
 
Siku zote Mwizi BAE Systems umuofia Mwizi mwenzake Vigogo wa serikali ya TZ! Ndio maana wanataka wapewe vyama vya Kijamii ili mafisadi wa TZ wasije faidi mara mbili!

Kama Membe angekuwa serious, angesema serikali ya JK imechukua hatua zipi kwa akina Chenge na wenzake kujihusisha na sakata hili. Analeta blabla ili zipotee kama za EPA!

Warudishe kwanza za Chenge ili BAE nao walete zao.
 
Kwa nini usijitahidi tu kueleweka ili watakaochangia waone tatizo ni nini. Yeye Membe anatoa msimamo wa serikali kwa sababu ukweli ni kwamba Serikali ndiyo iliyoibiwa fedha hizo na ndiyo inayostahili kurejeshewa fedha hizo. Uhalali au kukosa uhalali na fedha hizo hakutokani na jinsi serikali ilivyolishughulikia suala hili kwa sababu mpaka kabla ya uamuzi wa mahakama kuwatia hatiani BAE hauna ambaye angeweza kusema kwa uhakika kwamba kulikuwa na usanii. In any case waliofanya wizi huo walifanya in their personal capacities na hiyo haiwezi kuwa basis ya serikali kunyimwa fedha hizo. Hizi ni fedha ambazo serikali ilitapeliwa na anayetakiwa kurudishiwa ni yule aliyetapeliwa. Sasa cha ajabu hapo ni nini?

Mbopo,

Kama serikali ingekuwa na uchungu kiasi hicho isingezembea hadi hizo hela ziibiwe

Kaama serikali na wizara ya mambo ya nje mngekuwa na uchungu kiasi hicho mngetoa ushirikiano kuhakikisha wale watuhumiwa wanafikishwa mahakamani,kama hiyo ni ngumu inakuwa vipi rahisi kudai haki ya hizo hela?Let us be realistic bwana.

By the way,let me ask ou a very pertnent qstn,Nani alikuwa waziri wa mambo ya nje kipindi mkataba wa kununua Rada unasainiwa?

Sina shaka na usomi na uzoefu wa membe,lakini aache ku-compromise taaluma yake.Nitakuja tena kama utaendeleza mjadala



 
BAE systems wameamua kuzipatia asasi zisizo za kiserikali (NGOs) fedha (pound 29m) walizopiga cha juu wakati wa ununuzi wa rada badala ya kuipatia serikali, kwa misingi kwamba wana sera ya 'kuzisaidia' taasisi zinazoshughulika na masuala ya maendeleo. Sasa leo Membe (Waziri wa mambo ya nje) alikuwa anawaka kwamba lazima ipatiwe serikali maana ndio iliyoibiwa wakati wa ununuzi wa rada hiyo.

Kama kweli serikali ina uchungu na fedha hiyo mbona haikuwachukulia hatua wale wote waliohusika na wizi huo? Kwanini waliwaachia SFO peke yao wachunguze ishu hiyo wakat serikali yetu nayo ilikuwa na maslahi na ukweli kuhusiana na kashfa hiyo? Mi naunga mkono NGOs kupewa fedha hiyo, maana serikali imeona waliofanya wizi huo hawana hatia, lakini pia napinga BAE kutoa fedha hiyo kwa misingi ya 'msaada'. Karibuni tujadili........
 
..only fool can handle the money to CCM guys!! safi sana tena wasimamie wenyewe hadi senti ya mwisho!! walituona hatuko serious baada ya kututafunia kila kitu lakini EC akawa anaongezewa vyeo kila kukicha. Waingereza wamekasirika sana!!
 
Ni mwehu tu anayeweza kuwapa magamba wasimamie pesa hizo. Yaani leo pesa zimetoka ndo magamba wanaziona tamu eeeh. Kisheria pesa zile zko chini ya mahakama ya uingereza ndo yenye kuamua zitumikeje. Lakini kuzipa asasi za kiraia ni muafaka zaidi. Ila hizo ngo ziwe za tz zikishirikiana bega kwa bega na ngo za uingereza(ubia flani hivi).sio kuwapa zote ngo za uingereza maana membe kasema hawatapewa certifcates za kuoperate tanzania once wakija kuomba usajiri. Nimesikia bbc swa service kuwa serikali ya magamba imepanga kununua madawati na vitabu kwa ajhili ya shule za tz. Huu ni usanii. Pesa haujaipata ushaipangia matumizi.
 
Mh. Membe anafurukuta kwa vile anategemea kugombea Urais 2015 ili watanzania tuone anatetea haki.....Wakati hizo pesa zinakwapuliwa Mh. Membe kama mmoja wa UWT, anataka kusema hawakujua? Kwani Mh. Membe na UWT hajui hao watanzania wasaliti, wezi na wahujumu uchumi walioiba hizo fedha ili kuwanufaisha Waingereza?

Mh. Membe aache usanii na asifikiri kuna watu katika enzi hizi watampongeza!

Hii yote ni AIBU ya kufa mtu hususani kwa Serikali ya Mh. J.K............Pole sana Mh. J.K.
 
Ni mwehu tu anayeweza kuwapa magamba wasimamie pesa hizo. Yaani leo pesa zimetoka ndo magamba wanaziona tamu eeeh. Kisheria pesa zile zko chini ya mahakama ya uingereza ndo yenye kuamua zitumikeje. Lakini kuzipa asasi za kiraia ni muafaka zaidi. Ila hizo ngo ziwe za tz zikishirikiana bega kwa bega na ngo za uingereza(ubia flani hivi).sio kuwapa zote ngo za uingereza maana membe kasema hawatapewa certifcates za kuoperate tanzania once wakija kuomba usajiri. Nimesikia bbc swa service kuwa serikali ya magamba imepanga kununua madawati na vitabu kwa ajhili ya shule za tz. Huu ni usanii. Pesa haujaipata ushaipangia matumizi.

.... wakipewa zinaweza zikapotea kama zilivyopotea zile zilizorudishwa na wezi wa EPA!
 
Kuliko zirudishwe kwa hawa wahuni waliozigawa ni bora kuwapa SFO kwa kazi nzuri waliyofanya wakati UWT wakiwa usingizini.
 
hata hao waingereza walilazimika kuchunguza kwa kina kupata kujua kwamba kulikuwa na njama za kuiibia serikali ya tanzania na ndipo walipochukua hatua na pengine kama siyo ule utapeli ambao bae waliwafanyia wamarekani wakapigwa ile fidia ya kufa mtu basi issue hii isingejulikana. Sasa suala hapa ni kwamba aliyeibiwa ndiye wa kulipwa. Let's face it!

sasa mbopo aliyeibiwa hapa ni nani? Tuliobiwa kodi ze2 tulilalamika mapema ila st walikubali deal liliktwa halal ibin hakh. Tunataka kuona waliosabisha wanapata hakh yao- waka2mie mtondoo, c sharia zipo wajameni? Au 7bu wabia wenu wamewapiga kanzu bac mwatak
 
Wametafuna za hazina zmeisha na sasa wanazifukuzia za nje nazo wazitafune,serikali ya Tanzania haiaminiki tena imekuwa kama deci,hata wahisani baadhi wameshtuka wamesema watachangia bajeti yetu indirectly,kama ni afya watatoa magari,na dawa,kama ni elimu watatoa kwenye miradi kama ujenzi na vifaa,n.k,...hii iko safi sana tuone magamba yataishije!
 
Membe anaziita "HELA ZETU WALIZOCHUKUA"??! Mimi nadhani angeziita HELA TULIZOWAPELEKEA.
 
Back
Top Bottom