Serikali: Fedha za Maafa ya Tetemeko Kagera zimeelekezwa kwenye Taasisi za Umma

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Wakuu,

Kuna habari picha ambayo inasambaa mitandaoni (hususani Whatsapp) yenye maneno kuwa..

"Serikali imewaomba wakazi wa Kagera walioathirika na tetemeko kujijengea wenyewe kwani michango iliyochangwa na wadau imeelekezwa kwenye taasisi za serikali."

Picha hiyo ni ya kutoka ukurasa wa Facebook wa Simu Tv ambayo inamuonesha mtangazaji wa channel ten kama ndiye aliyeitangaza habari hiyo.!

Kwa wale mnaoangalia habari channel ten mnaweza kututueleza katika hili.

Je, kuna ukweli katika hili?
--------
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewaomba wakazi wa Kagera walioathirika na tetemeko kufanya jitihada za kujijengea nyumba zao wenyewe kwani michango iliyochangwa na wadau imeelekezwa kwenye taasisi za serikali.

Mkuu wa Mkoa amedai kuwa jumla ya fedha zilizochangwa ni zaidi ya Bilioni 5.4 na kusema kuwa zimeelekezwa katika kukarabati miundombinu ya taasisi za Serikali na kuwataka wananchi wanaosubiri msaada wa serikali kusubiri mchango itakayotolewa na wadau walioahidi kuwasaidia waathirika moja kwa moja.

Chanzo: Chanel 10
 
Hizi nyumba hata mia hazifiki wawape tenda sumajkt wafyatue matofali ya saruji kila kaya ipewe tofali elfu tatu na mifuko mia ya cement na mandali kumi za bati wajijengee wenyewe.

Pesa ipo, wanajeshi wanalipwa mishahara na serikali hata wasipoifanya hiyo kazi watalipwa tu mwisho wa mwezi, tatizo ni nini hasa?
 
Haya mbona yameanza kusemwa kitambo tu! Mimi nilijiuliza, hivi waliochanga walichanga wakiyajua haya au yameamuliwa baada ya michango kukusanywa?

Nijuavyo, kinachoweza kumfanya mtu aadhirike ni godoro lake kuwa nje kiasi tukaona kofuli zake na za mkewe, choo kilichovunjika kiasi akitaka kujisaidia baba basi Mama asaidie kwa kumzingira kwa khanga au wasubiri giza.

Nakumbuka hata muandishi wa ITV aliwekwa kuzuizini kwa muda baada ya kurusha habari ya njaa huko huko Kagera. Baadaye akaachiwa na misaada ya chakula ikapelekwa. Mungu atujalie rehema.
 
Habari wanaJF,

Back
Top Bottom