Fedha za KUJIKIMU kwa walimu wa DIPLOMA na GRADE A kiasi gan?

Patflax jr

Member
Apr 11, 2011
72
1
Wakuu habar za asubuh? Naomba kujuzwa ni kiasi gan cha FEDHA wanachostahili kulipwa waajiriwa wapya wa UALIMU kwa ngaz ya DIPLOMA na CHETI waliopangwa katika HALMASHAURI? Na je kiasi hicho ni sawa na Tshs ngap kwa siku? Na inastahili iwe kwa siku ngap? Coz kuna halmashaur moja nimepita nikakuta walimu wapya wa ngaz ya CHETI (GRADE A) waliokuwa wakihimizana KUGOMA baada ya kuambiwa kuwa stahiki zao za KUJIKIMU ni shiling LAKI MOJA TU. huku wale wa DIPLOMA na DEGREE wakiwa hawajaelezwa chochote. naomba kuwasilisha wakuu
 
Viwango vya posho ya kujikimu kama wewe si MHESHIMIWA, posho zinazingatia mambo yafuatayo:-

  1. Ngazi yako ya Mshahara (Siyo cheo au cheti)
  2. Mahali husika (Manispaa/jiji, hamashauri ya mji, kijijini)
Kwa mtumishi yeyeote anayeanza kazi, analipwa kwa siku 7 na kwa uhamisho analipwa siku 14.
Diploma, Grade A na Degree kwa wanaoanza kazi, viwango vyao vya posho viko sawa i.e. 45,000/- na 55,000 kama umeripoti jiji au manispaa.
 
which is which? kuweni serious mtu anapohitaji kufahamu jambo kama hujui pita tu kama mm ninavyopita
 
Kwa watumishi wengine wa uma, huwa inakuwa stahili yako ya kujikimu (per diem) ya siku 14 endapo umepelekwa nje ya mkoa uliopo, au perdiem za siku 7 kama uko kwenye mkoa huo huo uliopangiwa. Ulizia level ya perdiem yako.
 
Utaratibu wa siku 14 ulibadilishwa tangu mwaka jana mwezi wa nne sasa ni siku saba tu Halmashauri ni 30,000-35,000/day sisi tulichukua 490,000 kijijini ni 25,000/day hao ni TGHS A. ambaye ni mshahara wa 260,400/= pia usisahau kuhifadhi tiketi utarudishiwa pesa hizo za usafiri thats what iknow
 
Wakuu kuna mahali nimeomba posho ya kujikimu na nikanukuu kwamba nilipwe kwa mujibu wa sheria ya umma namba 8 ya mwaka 2002 ikisomwa pamoja na kanuni zake...Sasa kabla boss hajapitisha nilipwe file langu kalipeleka kwa mwanasheria wa taasisi ili kujiridhisha kama sheria niliyorejea ndo usahihi...
Je sheria hyo inahusika katika hilo maana najua inahusu kila kitu cha ajira ila sina uhakika kama inahusika na hyo posho
 
Back
Top Bottom