Fedha za EPA zilikorudishwa zaliwa tena; Peter Noni wa EPA, Simon Group wa UDA ndani..

Watu naona wana shida ya uelewa hapa! Noni anasema waliagizwa watoe pesa walizopokea kwa hao walitumwa na wakubwa..narudie waliambiwa watoe na sio wakopeshe!!!ninyi mnaouliza habari za colateral nani amewambia kuna colateral?ni huruma ya hao walopewa kutoa hizo pesa ama la!kama ilivyokuwa wakati wakurudisha za epa kwa hiari ndivyo ilivyo kwa sasa kwa wachukuaji kutoka TIB! Na huyu noni ni mpumbavu kama hakuhusija kwenye mchakato wa kuwakopesha/kwa nini anaongea habari za kuwadai???ndo shida ya watumishi wachafu aka mafisadi,confo zero kabisa...chukua hatua
 
Jamani mi nawaambieni siku nchi hii ikichukuliwa na viongozi wengine wenye uzalendo hii mifisadi yote itakimbia nchi akiwemo kaka yao yuleyule anayewakingia kifua..................

Kina mama wanajifungulia chini!!wanafunzi wanakosa mikopo kwa ajili ya masomo!! Tunasikia tu kila siku kuwa riz anamiliki hiki mara kile mi nasema ipo siku na umri wangu ni mdogo na imani mungu atanipa uhai ntayaona....

Kuna anayedhani kama gadafi na utajiri wake aliokuwa nao angepigwa kama kibaka!!!!???jibu ni moja tu watu tumechoka na its a matter of time! Mafisadi wote watakuwa wakimbizi kwenye nchi nyingine na ndo maana wanaanza kutaka kupitisha uraia wa nchi mbili,watu fumbukeni macho!!

Hawa chama chetu cha majizi wameshajua kuwa watanzania walimpenda nyerere na sio viongozi wengine na kwamba uko tuendako tamati yao inakaribia ndo maana wanaiba kila mtu kivyake ilimradi!!ila mungu yupo wanafunzi masikini wa kitanzania na wakina mama hawawezi kuendelea hivi!!mafisadi watasaga meno!!!
 
Vigogo watafuna marejesho ya EPA

Thursday, 03 November 2011 21:27


Leon Bahati na Furaha Maugo

KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mwingine wa mabilioni ya fedha kwenye marejesho ya zile zilizochotwa awali kifisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).Fedha hizo zaidi ya Sh50 bilioni zilizorejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa zitatumika kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo nchini, zinadaiwa kuchotwa kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa amri iliyotoka kwa vigogo serikalini.

Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.

"Mbaya zaidi, baadhi ya wafanyabiashara waliopewa mikopo hiyo wanaonekana kukwama kurejesha, huku wakitoa ahadi ambazo hawazitekelezi," Noni alisema.

Wabunge wengi wa POAC walionyesha kushangazwa na jinsi serikali ilivyoingilia kati TIB na kuchagua watu ambao wanapaswa kupatiwa mikopo.Huku miongoni mwa wabunge hao wakisema wana taarifa za vigogo walioingia mlango wa nyuma na kuchukua tena fedha hizo katika mazingira ya kifisadi, waliendelea kumbana Noni kwa maswali.

Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo.

Miongoni mwa wabunge waliotaka majina ya vigogo hao yawekwe hadharani ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya aliyesema, “Nina habari kuwa baadhi ya vigogo walihusika katika kupata mikopo hiyo… Naomba uyataje majina yao.”

Filikunjombe, alisema hakuna haja ya kutaja majina ya vigogo hao ambao alisema miongoni yamo kwenye taarifa waliyopatiwa kuhusu utendaji mzima wa TIB.

Lakini Noni ambaye alikuwa anasaidiwa pia na wasaidizi wake kujibu baadhi ya maswali mazito yaliyoulizwa na wabunge, alisema hakuna tatizo kutaja baadhi ya kampuni zilizohusika kwenye mikopo hiyo ambayo sasa inawatoa jasho TIB.

Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd.Nyingine ni kampuni tano za kuuza maua nje ya nchi zenye makao yake makuu mjini Arusha, zikiwepo Tengeru Flowers na Mount Meru Flowers.


Kuhusu Kampuni ya Simon Group, ambayo ilielezwa kuwa ilikopeshwa Sh5 bilioni Noni alisema; “Tumekutana nao mara kadhaa na kutoa ahadi lakini hawakuzitekeleza.”

Aliongoza kuwa kampuni za kuuza maua nje ya nchi zilieleza tatizo lililowafanya kushindwa kurejesha mikopo hiyo kulingana na makubaliano kwamba, ni hasara waliyoipata kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani.

Alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali iliwaonea huruma na kuwaongezea kipindi cha miaka miwili kulipa deni hilo, muda ambao pia umeonekana kutotosha.

Ila akaahidi kwamba TIB itaanza mchakato wa kuwabana wadeni hao kwa kunadi mali ambazo ziliwekwa rehani wakati wa kuchukua mikopo hiyo.

“Uandaaji na usafirishaji wa maua walisema unahitaji gharama kubwa… Walilazimika kupitia Nairobi (Kenya)… Serikali iliona huruma ikawaongezea kipindi cha kulipa deni hilo,” alisema Noni huku wabunge wengi wakionyesha shauku ya kuendelea kumbana kwa maswali.

Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa ni kwa nini TIB ilikubali kutoa mkopo kwa biashara ambazo hazitabiriki? Noni aliweka wazi kwamba, benki hiyo haikuhusika katika mchakato wa kuchambua na kuridhia mikopo kutolewa kwa kampuni hizo.

Filikunjombe ambaye ni Mbunge wa Ludewa, alishangazwa na jinsi Serikali ilivyoingilia uhuru wa TIB na kuweka wazi kwamba si mara ya kwanza Serikali kuingilia mashirika ya umma kiutendaji na kwamba, historia inaonyesha kila ilipofanya hivyo iliziingiza taasisi hizo kwenye mzozo.

“Serikali iliwahi kuingilia kati na kushawishi Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) kuingia mikataba (ya kuzalisha umeme wa dharura) na Richmond na Dowans na kusababisha mzozo,” alitoa mfano Filikonjombe.

Hivyo, akaonya TIB kuhusu kupokea maagizo holela Serikalini kwa sababu mzigo wa matatizo yatakayotokea, itajiweka kando na kuiachia taasisi hiyo ya umma lawama na vibano kutoka kwa wananchi.
Mapendekezo ya Kamati
Ili kuikoa benki hiyo, Filikunjombe alitoa mapendekezo sita ambayo miongoni mwake ni kuitaka TIB ijitegemee na kufanya kazi zake kama shirika la umme lenye uwezo wa kufanya maamuzi yake ya kiutendaji bila kuingiliwa na wanasiasa serikalini.

“Mhakikishe hamuingiliwi na Wizara ya Fedha au Serikali katika suala la utoaji wa mikopo,” alishauri Filikonjombe.
Mapendekezo mengine ni muundo wa manunuzi katika taasisi yao uendane na sheria ya manunuzi, kuwa ni mikakati ya kushindana kibiashara na benki nyingine na kuhakikisha kuwa mtaji unakua.

Katika hatua nyingine, POAC ilishangazwa kuona kuwa kati ya zaidi ya Sh50 bilioni zilizokusanywa kwenye marejesho ya fedha zilizochotwa EPA, ni Sh20 bilioni pekee zilizoifikia TIB.
Wabunge hao walielezea kushangazwa na kitendo cha Menejimenti ya TIB kupokea fedha hizo tu na kushindwa kuishinikiza Serikali itoe fedha zaidi.

Noni alisema kuwa TIB haikuwa na mamlaka ya kuishinikiza Serikali ili iipatie fedha zote za marejesho ya EPA.
“Sisi tulichopewa ndiyo hicho. Hatukuwa na sababu ya kudai fedha zaidi,” alisema huku akizidi kuzua mtafaruku wa maswali kwa wabunge hao.

Wabunge wengi walionyesha kuamini kuwa fedha zote zilipelekwa TIB baada ya Serikali kuahidi kuwa fedha za marejesho hayo zitapelekwa kwenye shughuli za kilimo.

TIB ndiyo benki iliyoanzishwa na Serikali kwa malengo ya kuinua kilimo nchini ambacho kinategemewa na asilimia 80 ya Watanzania.Wananchi wengi wanaojishughulisha na kilimo nchini ndio wanaogubikwa na wimbi la umasikini kuliko sekta nyingine.

Hata hivyo, Serikali imeamua kuanzisha kampeni ya Kilimo Kwanza, yenye lengo la kufanya sekta hiyo kuwa yenye manufaa na inayoweza kuleta utajiri tofauti na mwonekano wa sasa wa kuwa ni ya kundi la wasio na taaluma.
Taarifa nyingine zilizopatikana jana baada ya kamati hiyo kumaliza kikao chake ni kwamba sehemu ya marejesho ya fedha za EPA, mbali na zile Sh20 bilioni zilizopelekwa TIB, zilitolewa kwa moja kwa moja kwa kampuni za pembejeo za kilimo.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge walielezea kutokuwa na imani kama fedha hizo zilitumika kikamilifu kwa ajili ya pembejeo hizo za kilimo.

Mmoja wa wabunge kutoka CCM ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kuna uwezekano fedha hizo zimeliwa na wajanja.

“Hata ukiangalia suala la marejesho halikuwekwa wazi, maana Rais (Kikwete) mwenyewe alisema zimekusanywa Sh53 bilioni, mara wengine wakasema 60 bilioni na wengine 70 bilioni.Alisema kama ufisadi uliweza kupenya hadi fedha zilizotolewa kwenye taasisi makini ya benki (TIB) basi hakuna shaka hata zilizotolewa kimyakimya ziliingia kwenye mikono hiyo ya mafisadi.

Hata hivyo, gazeti la serikali liliwahi kumnukuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mohamed Muya, akisema katika mgawanyo wa fedha za EPA, wizara hiyo ilipewa Sh40 bilioni ambapo Sh30 bilioni zilitumika kwa ruzuku ya pembejeo ya mbolea hali ambayo imesaidia katika uzalishaji. 


“Kutokana na ruzuku hizi, hata idadi ya wakulima wanaopata vocha za ruzuku hiyo imeongezeka kutoka wakulima 500,000 hadi wakulima milioni 1.5 mwaka huu na kupitia Kamati ya Maafa na ya Usalama wa Chakula, hali ya chakula mwaka huu ni nzuri kuliko mwaka jana,” alisema Muya. 



Alisema katika fedha hizo za EPA, Sh10 bilioni zilizobaki zilitumika katika maeneo matatu ya kilimo ambayo ni Mfuko wa Pembejeo ambao ulipewa Sh3 bilioni, Wakala wa Mbegu wa Taifa Sh1 bilioni na kutatua matatizo ya visumbufu kama vile nzige, kweleakwelea na viwavijeshi Sh6 bilioni.

 
Kampuni za maua zilipewa mkopo na Serekali kupitia Bank Kuu chini ya usimamizi wa TIB miaka ya 2004/2005. Kampuni zilizopewa mkopo huo chini ya mfuko ulionzishwa na Mh Mramba wa kukuza export of high value crops/products with critical mass and employment creation (Export Guarantee Scheme) ni pamoja na Kiliflora, Tengeru Flowers, Tanzania Flowers Ltd, La Fleur d'Afrique Ltd (Hii ni kampuni ya Mheshimiwa Felix Mrema aliyekuwa mbunge wa CCM Arusha mjini) na Gomba Estate. Kampuni hizi zilipewa mabilioni ya fedha na toka wakati huo urudishwaji wa mikopo hii umekuwa wa kusua sua, nadhani LDF ya Mrema haijarudisha hata senti moja hadi leo
Kampuni zilijenga hoja kwa Serekali na BOT kuwa KIA imekuwa kama gofu kwa kuwa hakuna ndege za mizigo zinatua pale kwa kuwa hakuna mzigo wa kutosha. Zililalamika kuwa zinapeleka maua Nairobi na hivyo yanapoteza freshness kwa at leat 2 days. Hivyo zikaomba serekali izikopeshe ziweze kuongeza uzalashaji, kukuza ajira na kuufanya uwanja wa KIA UWE FUNCTIONAL. Hizi kampuni wakati zinaomba huu mkopo zilikuwa HOI na madeni makubwa ya ndani na nje ya nchi, zilikuwa hazikopeshekiki na wadeni walishaanza mchakato wa kuziflilsi. BOT ilizilipia madeni hayo kuzifanya ziwe bankable- restructuring, and yet zikawa sio bankable na BOT ikazipa fedha kwa mabilioni.

Kinachoniuma na kunishangaza ni kama serekali imeendelea kushindilia mikopo mingine mipya kwa kampuni hizi hata baada ya kushindwa kulipa mikopo ya awali ni ufisadi wa hali ya juu. TIB walipewa jukumu la kusimamia mikopo hiyo na wanajua fika uwezo wa kampuni hizi kiutendaji na kifedha, sasa iweje waendelee kuwachotea mabilioni hayo? Watanzania wenzangu tumuulize boss wa TIB ilikuwaje awape fedha wakati fedha za serekali mabilioni kw amabilioni hazijarejeshwa? LDF nadhani imekufa, je TIB imeishaifilisi kurecover fedha za walipa kodi? Hivi kwa nini viongozi wetu wamekosa uzalendo kiasi hiki. Ni vyema vyuo na shule vikaanza kufundisha kw alazima somo la uzalendo, it is getting out of control kwa hali hii ndugu zangu.

Mie nadhani hilo ni changa la macho, waandishi na wabunge msikubali jambo hilo, siamini kama TIB imetoa mikopo mipya kwa hizi kampuni, hata baada ya kushindwa kulipa mabilioni ya awali, si ajabu inatumia information za mikopo ya zamani iliyotolewa wakati huo kuficha ukweli. CHANGA LA MACHO HILO!!


Mkuu nakubaliana na wewe, hizi kampuni mfu zinzsingiziwa tu ili kuuficha ukweli wa mambo maana wameamua kutumia hizi kampuni ili ijulikane kuwa zimepata hasara ili tusiwe na nguvu ya kufatilia pesa hizo. Pesa za EPA zimepelekwa sehemu tofauti kabisa na wala si kwa makampuni haya. Noni akibanwa atanyosha maelezo tu. Haiwezekani kampuni iliyofirisika bado inarudi kwako unaikopesha tena hilo halipo. Nadhani kazi sasa waachiwe wenye uchungu na hii nchi wafatilie hela hizi pamoja na zile za sitimulas package ambazo PM mpaka leo anamungunya maneno hajawahi kutolea maelezo.
 
...

Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo. ...Mwananchi 03/11/2011​

du! naona filikunjombe amechomoa kiaina, hataki kubaki na siri ala mwakyembe, kisha aishi kwa
wasiwasi.
 
Kwani ni nani alithibitisha kuwa pesa ya EPA ilirudishwa? kama Gavana wa BOT anasema yeye hajui iliko sasa ni nani mwingine anayejua iliko pesa hiyo?
 
siku imeharibika, ndio maana wanataka kutufanya mashoga, hatuna akili nzuri. nimechoka na hii sanaa ya ufisadi Tanzania.
 
Izi kampuni za maua sio za EL kweli?
Filikunjombe ni wale wale tuu alikuwaga polisi ukimpiga na kama 100mil inatosha kumnyamzisha so atakuwa kawekwa sawa esabu zikapita!
Hii regime kwa kifupi yote inahusika na udokozi wa fedha za umma daily na kufanya watu waishi maisha magumu
 
Mjini wanasema Simon aliombwa akachukue pesa TIB kwa ajili ya kuwezesha kurudi madarakani kwa baba ritz,na yeye akatekeleza kwa ahadi kuwa baada ya uchaguzi atarudishiwa,

Sasa uchaguzi ukaisha na dola ikashikwa Kasena akaanza kudai maana na yeye alikuwa anapigwa pressure TIB, cha kurudisha kikawa hamna maana gentlemen agreement tena, basi uamuzi ukatoka atafute shirika lolote apewe aweze kurejesha mkopo na uda ndo ikaonekana ndio sahihi zaidi, the rest you know
 
Pengine naomba kama ntawakosea
mashoga wengi ukisikia walipotokea wameamua kujiingiza sabau ya shida yaani wengine wanakwambi wakiwa mashulen walikuwa wkaipata lift na wazee na jamaa sikunyingine awapeleki shule wanaenda maficho leo wako maofisini bright mbaya lakini ndio hivyo wasipotenguliwa kule ni ngumu....sasa basi ukiwa kama mtanzania angalia hapo juu watu wameiba billion 20 ndany ya miaka miwili jiulize je hii nchi ni ya kwenda kuomba omba ovyo uk na kweingineko...na hao walioiba bado wapo mbaya zaidi kama huyo mwizi wa tib peter nyoni amehusishwa na epa,,akapelekwa bank ya tib..waliporudisha hela billion 50 mafisadi ukaguzi umefanyika zile hela azijulikan alipew ana nani mbaya zaidi bilion 20 aziko kwenye maandishi na anajibu mi sijui kama mnajua zilipo tusaidieni kama kamati ya bunge..anachojua azina walikuja wakachota

hivi nchi kama hii kila siku wanaomba omba na sasa bwana wenu gadafi ameondolewa kabisa duniani anachosema cameroon unafikiri ni mijnga ??anaona mbali amemaanisha sasa imetosha vya bure enough is enogh sa sa kila mtu atakula kwa urefu wa kmba yake so na nyie watanzani mkae mkao wa kuliwa ndio misaada ije .....

Inasikitisha san san mungu aturehemu ila nahisi cameroon ameona hawa mabwabwa kweliii kila siku wanaaomba huku wamejaza uchumi nyuma na kugaiana mabiliions
 
Haya ndo mambo yanayotia hasira na kuchochea mapinduzi kwani hata raia wanona bora wafe kuliko kuishi katika nchi ya kifisadi namna hii. Yani inapotokea hali kama hii inachochea hasira na kupeleka raia kutaka serikali iliyoko marakani kuondoka. Hebu fikiria eti mtu 1 au 2 wanajichotea mabilioni ya shilingi afu wengine wakifa kwa kukosa dawa mseto.

Halafu utasikia eti serikali haina hela, mara utasikia serikali imekopa benki ili kuwalipa wafanyakazi wake halafu utasikia dowans ilipwe haraka... Ufisadi mtupu.

Tuwe na subira kidogo na kama serikali itaendelea Ku-intertain ufisadi huu hapa nchini basi mwisho wao kuwa madarakani unakuja.
 
Kwani ile taarifa katika sakata la UDA ya Kapuya kuhusika na Simon Group imesahaulika?
 
Msiwe na wasi wasi, picha nyiningine part 11 inaanza... ikiwa bunge litakuja juu kuhusu kama fedha hizo za EPA zilirejeshwa kama ilivyotambwa, kitakachofanyika ni rahisi tu:

  1. itaundwa kamati ya bunge, yenye wabunge ambao hawajai kuchangia au kuwa na mchango wowote, ikiongozwa na mwenyekiti aliyechaguliwa maalumu kutoka kundi maalumu la kuhakikisha kinachojadiliwa na kuwasilishwa ni kile tu wanachotaka walionyuma ya igizo zima.. watapewa script na hivyo kuigiza kama akina kanumba mstari kwa mstari
  2. serikali/ikulu nayo itamwambia Utto, kwamba chunguza pale, tupate majina ya vigogo walioshinikiza TIB ikopeshe iliowakopesha fedha hizo kiduchu za masalia ya EPA, achunguze ni kiasi gani kiliwafikia TIB kutokana na fedha za EPA, achunguze na kufanya upelelezi wa kiintelejensia kujua ni makampuni gani yalinufaika na fedha hizo na mwisho alete taarifa pale Habari maelezo kuhusu alichokibaini kutokana na utaalamu wake na timu yake, kwa sababu serikali/ikulu imeshutushwa na tetesi hizo kwamba yawezekana fedha ambazo imekuwa ikiwahahakikishia wananchi zilirejeshwa na Kagoda and co, hazikurejeshwa na kama zilirejeshwa sehemu kidogo tu, hazikupelekwa inakodai zilielekezwa na kama zilielekezwa huko, ziliwarua waliozirejesha! Hata hivyo, itakuwepo hadidu ya rejea (BCC) ambayo haitawekwa wazi kwa public ambayo ni kumtaka Utto, kucheza kama pele kuhakikisha anaweka mambo sawa sawa na ikibidi atoe onyo kwa wabunge kujipa kazi ya uodita wakati hawajahi kupata CPA na hata wakijaribu hawapati ng'o maana ufahuru wa mitihani hiyo haupaswi kuzidi 15% kwa mwaka
  3. vyombo vingine viwe macho na wanaotaka kuchonga kuhusu ishu hii wakati, tayari serikali imeshachukua jukumu la kumuagiza CAG achunguze na alete taarifa na ikibidi bunge nalo lisiruhusiwe kujadili ishu hii maana ilishafungwa na mbunge yeyete asimuulize swali waziri mkuu siku za alhamis kuhusiana na swala hili maana hiyo inaweza kuchochea mauaji ya kimbari kama yaliyotokea huko Rwanda ni bora fedha ipotee hata kama wananchi watakula nyasi lakini kuliko kuleta mauaji kwa kuuliza nani wanaokula fedha ya umma
  4. ikibidi, wanaolekea kujipendekeza kutafuta umaaru wa kisiasa, wapewe aina fulani ya vijimelea vya ugonjwa unaoweza kuwafanya walazwe hata miezi kadhaa huko india hadi hapo, hali itakapokuwa shwari,
  5. vinginevyo itengenezwe sinema kali zaidi kama kujivua koti ili umma uwe busy na hisshu hiyo, ikibidi, ili swali hili life kama lilivyosaahulishwa huko nyuma
 
KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imebaini ufisadi mwingine wa mabilioni ya fedha kwenye marejesho ya zile zilizochotwa awali kifisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Fedha hizo zaidi ya Sh50 bilioni zilizorejeshwa na Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuwa zitatumika kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo nchini, zinadaiwa kuchotwa kwenye Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) kwa amri iliyotoka kwa vigogo serikalini.

Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.Mkurugenzi wa TIB, Peter Noni alikiri jana mbele ya POAC kuwa sehemu ya Sh20 bilioni zilizotolewa na Hazina kwenda kwenye benki hiyo kwa ajili ya dirisha la kilimo, Serikali iliamuru zitolewe kama mkopo kwa wafanyabiashara ambao iliwataja kwa majina.

Ingawa baadhi ya wabunge walimtaka mkurugenzi huyo wa TIB awataje kwa majini vigogo hao, Makamu Mwenyekiti wa POAC, Deo Filikunjombe, alisita na kumtaka Noni asitaje majina hayo. Noni alitaja mbele ya kamati hiyo kuwa moja ya kampuni zilizochukua fedha hizo na sasa zinaonyesha wasiwasi katika kuzirejesha ni Simon Group Ltd. Nyingine ni kampuni tano za kuuza maua nje ya nchi zenye makao yake makuu mjini Arusha, zikiwepo Tengeru Flowers na Mount Meru Flowers.

Kwa kweli sakata la EPA ni ufisadi taslimu na linatia kichefuchefu sana. Toka Rais alipomteua Peter Noni kuwa Mkurugezi TIB nlijua lengo ilikuwa ni kufanya haya yaliyotokea. Peter Noni alihusika katika wizi wa fedha za EPA akiwa mfanyakazi BOT. Hivyo kuteuliwa kwakwe kuiongoza TIB ilikuwa ni kuhadaa wananchi na kuficha ukweli.

Kwa Rais kumteua mtuhumiwa wa wizi wa EPA kuiongoza TIB na Baadaye kutudanganya kuwa hizo hela keshazipeleka TIB na kumkabidhi Peter Noni ni kutufanya wananchi viazi, wapumbavu na mazezeta. Kimsingi hapa Rais amejipambanua kama mhusika ktk hili sakata la EPA. Ukichunguza kwa undani unaweza kukuta hizo fedha hazikupelekwa kabisa TIB, ila kwa kuwa TIB inaongozwa na mtuhumiwa wa huo ufisadi tumedanganywa tu.

Hivi nini hasa sababu ya sisi wananchi kufanywa wapumbavu??Hivi Rais hakuona mwingine wa kumweka TIB zaid ya huyu Peter Noni ambaye ni mtuhumiwa wa EPA pia???hivi kweli sisi wananchi hatuna cha kufanya katika ujinga kama huu???kwann tuliowaamini kutuongoza leo wamekuwa wanatuhujumu??Nini hasa sababu ya kuwa na serikali isiyoaminika kama hii? Kama inashindwa kuaminika kwa fedha ndogo kama hizi kwa nn tuwaamin kwa kuwaachia nchi na rasilimali zake?

Hivi hakuna utaratibu wa kuondoa viongozi wezi kama hawa? Nani aliyeiamuru TIB kukopesha hao walioshindwa kurudisha hizo fedha???Naomba tumjue aliye amuru, PCCB, wataalam wa Intellejensia (KOVA na Mwema) hamuoni kama kunaharufu ya Rushwa hapo???Hakuna kitu mnaweza fanya hapo kwa Kiongozi aliyeagiza hela ya wananchi zitoke kienyeji?

Kwa utaratibu huu wa kutoa mikopo kwa kujuana, TIB itasurvive? Tunapoelekea naona Serikali itatutia kidole jichoni, nadhani inatosha.................................Nakaribisha mawazo yenu wanaJF nn kifanyike kukomesha hii hali.

Mwananchi 03/11/2011
 
Back
Top Bottom