Fedha za BAE ziongeze mishahara kwa wafanyakazi wa serikali

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,167
79,330
Wajameni mei naomba kusema haya, ile 3% ya nyongeza za mishahara haina tija kwa wafanyakazi na ningeshauri hizo 29 mio. pounds zingeelekezwa katika kuboresha mishahara ya wafanyakazi! maana hiyo ndiyo njia pekee ya kuwekeza katika uchumi wa nchi hii kwa sasa! ikumbukwe itasisimua uchumi maana matumizi yataongezeka na kodi zaidi itakusanywa (wafanyakazi ndio walipa kodi nchi hii)!
 
Mkuu, na mwakani itakuaje itabidi mishahara ushuke kutakuwa hakuna tena nyongeza ya pesa! Baada ya hizo milion 29 £, hizo pesa wangezipeleka kwenye miradi ya umeme
 
Aliyeshiba hamjali mwenye njaa. Suala la nyongeza ya mishahara haliwagusi wao, na ndo maana wala hawajakomaa sana wakati bajeti inasomwa na hawa ghasia. Tazama umeme, ndiyo ni muhimu kwetu sote...lakini kwa mtazamo wangu naona walikomaa sana wakati wa bajeti ya nishati na madini kwani umeme unawagusa wao pia kwa ukaribu zaidi, wanapokuwa hotelini, familia zao....
 
unatumia tumbo kifikiri wewe? Kwan hzo hela tunapewa kila mwaka?
natumia economics baada ya kupewa wafanyakazi kama makusanyo ya kodi yatakuwa mazuri basi kutakuwa na njia ya ku-regulate that increase hata mwezi unaokuja! Fikiria unapoongezwa mshahara hata kodi inaongezeka na makusanyo yanaongozeka hata toka ununuzi wa bidhaa! nasema bora wapewe wafanyakazi kwa vile at least database yao iko secured kuna uwezekano wa kodi kukusanywa kuliko kupewa makampuni binafsi kupitia tenda za ujenzi au miradi yeyote! Kwa vile tunafahamu tenda hizo zitaenda kwa makampuni ya mafisadi papa ambao hawalipi kodi au wanapata misamaha kila mwaka!
 
GEZA, Naomba nikupinge

ile pesa si sustainable... ti should be used to support one time investiment unders very close scrutiny (ili tuepuke mabilioni ya JK kashfa)
 
Back
Top Bottom