Fedha Nyingi Kutumika Kuhifadhi Ziwa Victoria

Ipole

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
294
10
Habari kutoka gazeti la Standard la Kenya tarehe 26 zinasema nchi 5 wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki zimepata dola za kimarekani milioni 230 ili kutumika kwa ajili ya kuhifadhi Ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa kabisa la maji baridi barani Afrika.

Katibu mtendaji wa kamati ya bonde la Ziwa Victoria Bw. Tom Okurut alisema fedha hizo zinatolewa na Benki ya Dunia, Mfuko wa mazingira duniani na serikali ya Sweden. Ruwanda na Burundi zinapata msaada wa dola za kimarekani milioni 25 kwa kila upande, Kenya Uganda na Tanzania zinapata mikopo ya dola za kimarekani milioni 60, 55 na 65 kwa nyakati tofauti.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom