Fedha mpya haziendani na mfumo wa muamala wa TANZANIA

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Kuna vikao kati vya ma-CEOO wa mabenki na uongozi wa BOT nini kifanyike ili fedha walizotengeneza ziweze kutumika katika miamala yetu yaani ATM machines. Fedha hizi mpya ni tofauti kwa size na za zamani. Swali ni Je kama hizo fedha hazita fit kutumika/wa na ATMs zetu zitarudiwa kuchapishwa? au watang'oa ATMs zote na kuweka mpya?

Nitajitahidi kuwapa update za noti mpya kadiri nitakavyozipata.

UPDATE

BOT walikubaliana na mabenki nchini kutoa chip maalumu zitakazo fungwa kwenye ATM ili ziendane na size ya noti mpya. Kampuni inayosambaza na kufunga hizo chip tutaifahamu hivi punde.
 
Kuna vikao kati vya ma-CEOO wa mabenki na uongozi wa BOT nini kifanyike ili fedha walizotengeneza ziweze kutumika katika miamala yetu yaani ATM machines. Fedha hizi mpya ni tofauti kwa size na za zamani. Swali ni Je kama hizo fedha hazita fit kutumika/wa na ATMs zetu zitarudiwa kuchapishwa? au watang'oa ATMs zote na kuweka mpya?

Nitajitahidi kuwapa update za noti mpya kadiri nitakavyozipata.

kama ni kweli wote waliohusika na mpango huo wanyongwe, fikiria hiyo gharama iliyotumika kuprint hizo pesa mpya,
 
Uchafu wa CCM ni mwingi. Kwanza haijaelezwa vema ni kwa nini waliamua kubadilisha hizi noti baada tu ya uchaguzi mkuu. Nilipata kusikia tetesi kuwa waliprint note nyingi feki kwa ajiri ya kuyadanganya majuha yawapigie kura, niliposikia wamezibadili nikajua huenda ni kwa sababu hizi feki note zimekuwa nyingi mtaani hivyo ilikuwa njia ya kuzi-flush out.

Wana JF makini naomba ufafanuzi wenu katika hili!
 
Thanks for info.
Inaonekana BOT walifanya uamuzi wa kutengeneza notes mpya bila hata kufikiria mambo mengine kama ya ATM.
Ila ndugu mtoa mada, naomba urekebishe title. Ninavyofahamu mimi neno Muamala ni kiswahili cha Transaction. Of course I stand to be corrected.
 
Mkubwa asante hata hivyo mm sijui kiswahili fasaha cha mashine ya kutolea fedha nilishtushwa na vikao na posho za kuwalipa hao wakaaji kwa ajili ya kujadili kitu ambacho kingekuwa kimejadiliwa kabla ya kutendeka. Sijui wasomi wetu wako wapi na wanafanya nini?
 
Yaani inamaana safari hii BOT wametengeneza noti bandia? mbona ATM zinazotumika kwa noti duniani kote ni hizo hizo, (iwe ni Yen, Yuan, Rand, USh, Ksh, Rubbles)...
 
BoT kwa mara nyingine tena wamekurupuka na hivyo wataliingizia Taifa hasara kubwa maana inabidi pesa hizi zenye thamani ya mabilioni zitengezwe upya. Yeyote yule katika management ya BoT anayedhani kwa namna moja au nyingine amehusika na uzembe huu anyooshe kidole/mkono juu. Hakuna anayenyoosha mkono/kidole juu?
 
Duniani kote, ni kweli wanatumia ATM kutoa pesa za aina mbalimbali. Lakini je, kuna ATM gani bongo inatoa fedha za kigeni? Maana wageni wamekuwa wakilalamika kuwa ukifika Tanzania kama unahitaji foreign currency lazima ubadili kwenda kwenye Tshs. Nchi nyingine machine za sehem za kusafiria kama airport zina options za currency tofauti.
Ukweli ni kwamba BOT wamebadili size ya note ili ziweze kuhifadhika zaidi na kuachana na size zile za zamani. Lengo lao lilikuwa jema ila walitakiwa wawataarifu wenye mabenki juu ya hili na huenda wangekuwa wamejiandaa zaidi. Kwa nchi yetu sekta binafsi imekuwa ikidharaulika lakini ingepewa nafasi inayostahili huenda uchumi wetu ungefika mbali zaidi.
 
Mkuu nadhani si lazima watengeze pesa upya. hapo ni kuangalia cost-benefit analysis. Kwani Tanzania kuna ATM ngapi? Gharama ya kuadjust hizo ATM zinafanana na kuchapisha notes? Wanaweza kuziadjust na kazi ikaendelea.
 
Haya lakini hata kama ATM machines ndizo zitakazokuwa adjusted kwa gharama za BoT, lakini kilichofanyika ni uzembe wa hali ya juu na mtu/watu (w)anastahili kuwajibishwa. Utafanyaje maamuzi ya kutengeneza noti mpya bila kufikiria ukubwa wa noti hizo ili ziweze kupita bila matatizo katika hizo ATM machines?

Well inawezekana kukawa kuna uzembe. Lakini tatizo ni kuwa hawakuwataarifu wenye mabenki au wametengeneza size tofauti na za zamani? Kwanini unadhani BOT ndio inawajibika kununua au kutengeneza mashine ili ziendane na hiyo pesa? Wenye mabenki wanahitaji kufuata hitajio la nchi au nchi inahitaji kufuata hitajio la mabenki? Naomba nieleweke nahitaji nguvu katika sekta binafsi lakini maswali haya niliyouliza yanatufanya tufikiri responsibly zaidi.
 
Duniani kote, ni kweli wanatumia ATM kutoa pesa za aina mbalimbali. Lakini je, kuna ATM gani bongo inatoa fedha za kigeni? Maana wageni wamekuwa wakilalamika kuwa ukifika Tanzania kama unahitaji foreign currency lazima ubadili kwenda kwenye Tshs. Nchi nyingine machine za sehem za kusafiria kama airport zina options za currency tofauti.
Ukweli ni kwamba BOT wamebadili size ya note ili ziweze kuhifadhika zaidi na kuachana na size zile za zamani. Lengo lao lilikuwa jema ila walitakiwa wawataarifu wenye mabenki juu ya hili na huenda wangekuwa wamejiandaa zaidi. Kwa nchi yetu sekta binafsi imekuwa ikidharaulika lakini ingepewa nafasi inayostahili huenda uchumi wetu ungefika mbali zaidi.

Mkuu Anfaal,

Wachapishaji wote wa noti duniani (wala hawako wengi wanahesabika) wanajua stardard measurements zinazotumika katika ATMs. Ni kama vile watengenezaji wa simu za mkononi na wale wa SIMcards au USB slots kwenye Kompyuta, au printers na USB sticks, au Memory cards...

Suala la kutoa pesa za kigeni kwenye ATM za bongo badala ya foreign currencies ni lingine (labda ni policy tu za BOT) na wala halihusiani na vipimo vya noti au ATM zenyewe..

Nadhani kuna hata ATM nyingine zilizong'olewa South Africa (mitumba) sasa hivi zinatumika Bongo..
 
ATM hazishindwi kupokea fedha hizi ila kuna mchezo mchafu unaotaka kutokea usisahau wakati kama huu wa kubadili fedha ndiyo unaweza kuingiza fedha chafu subiri uone itakuwa kama Zimbabwe unakwenda dukani na begi la hela kununua sukari:A S 465:
 
Muro,tuombe lisitokee hili!
 
Mkuu Anfaal,

Wachapishaji wote wa noti duniani (wala hawako wengi wanahesabika) wanajua stardard measurements zinazotumika katika ATMs. Ni kama vile watengenezaji wa simu za mkononi na wale wa SIMcards au USB slots kwenye Kompyuta, au printers na USB sticks, au Memory cards...

Suala la kutoa pesa za kigeni kwenye ATM za bongo badala ya foreign currencies ni lingine (labda ni policy tu za BOT) na wala halihusiani na vipimo vya noti au ATM zenyewe..

Nadhani kuna hata ATM nyingine zilizong'olewa South Africa (mitumba) sasa hivi zinatumika Bongo..
Kwahiyo thread hii inaweza kuwa ya kizushi
 
Back
Top Bottom