Fedha (jairo) zimetumika kuwahonga wabunge wa CCM, CUF na TLP kupitisha muswada wa katiba haraka

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Inafahamika kuwa CCM imekuwa ikitumia fedha kama kishawishi cha kupitishwa kwa mambo yake mbali mbali ikiwemo chaguzi zake za ndani, uchaguzi mkuu n.k. Aidha zimekuwepo tuhuma za muda mrefu kuwa Serikali ya CCM hutumia fedha kuwahonga wabunge kupitisha bajei na miswada ya mbali mbali ya sheria.

Ushahidi wa hilo hiyo ni tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg David Jairo pale alipochangisha fedha ktoka taasisi zilizo chini ya wizara aliyokuwa akiiongoza kwa lengo la kuwahonga wabunge kupitisha bajeti ya wizara yake. Vile taasisi mbali mbali ambazo huwasilisha miswada ya sheria bungeni hulazimka kuandaa semina na kuwaatia wabunge posha kubwa kubwa ndipo miswada hiyo hupitishwa kama ilivyo bila ya kujali itawaathiri vipi wananchi.

Kwa kutazama jinsi ambavyo wabunge wale wale wa CCM, CUF na TLP walivyokengeuka na kushabikia muswada wa katiba walioukataa miezi michache upitishwe kwa pupa ilihali ukiwa na mapungufu kibao. Ni dhahiri kuwa safari hii Serikali ya CCM itakuwa imetekeleza yale iliyowazoesha wabunge wake pamoja na wenzao kutoka upinzani wasio na maadili, yaani kuwahonga fedha ili wakubali kupitisha muswada kama walivyozoea bila ya kujali athri zake kwa mustakabali wa nchi.

Ikumbukwe kuwa wakati bunge lilipoukataa muswada wa awali Aprili 2011, ilikuwa ni miezi michache tokea wabunge watoke katika uchaguzi mkuu ambapo walitumia fedha nyingi ili kushinda. Hivyo basi kilichowasukuma wabunge wa CCM,CUF na TLP kuukataa muswada wa katiba wa Aprili 2011 sio mapungufu yake bali ni kitendo cha Serikali kuwasilisha muswada bila (JAIRO yoyote), yaani uwezeshaji kwa upande wa wabunge?

kwa mujibu wa mijadala ya wabunge wengi wa CCM, CUF na TLP haionyeshi hata kama wanafahamu nini kimo ndani ya muswada huo ndio maana huchukua muda mwingi kuisema CDM na Tundu Lissu; hii ni kiutokana JAIRO iliyotolewa kwao.
Naomba kuwasilisha!!
 
Uko sawa, na huo ndio mwendo wenyewe siku zote....hata Jairo alifanyiwa roho mbaya na aliyekosa bahasha siku hiyo.
 
Back
Top Bottom