Fear for criticism

Nxt Millionaire

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
406
89
Moja ya vitu ambavyo ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia mafanikio yake au ndoto na maono WOGA (FEAR FOR CRITICISM) ni namba moja.

Woga ni adui mkubwa sana wa kuifikia ndoto/maono zetu, Ni kibinadamu kuwa waoga, ni maumbile. Ili mtu aweze kufanikiwa na kufikia ndoto zake unabudi kuushinda woga.

Nimejisikia leo kuzungumzia juu ya mada hii kutokana na uzoefu nay ale niliokutana nayo katika juhudi za kufikia mafanikio ama ndoto/maono.

Dr Napaleon Hill anasema:

“Every person comes into this world cursed, to some extent, with six Basic Fears, all of which must be mastered before one may develop sufficient self-Confidence to attain outstanding success.”

Dr Hill amechukulia woga kama ni laana ya aina fulani inayozuia mtu kufikia ndoto ama malengo yake, hiki ni kiwazo kikubwa sana, anasema sote tumezaliwa na aina sita za woga ambazo hatuna budi kuzishinda iwapo twataka kufikia malengo ama ndoto zetu maishani, haijalishi ni ndoto gani ulionayo ni muhimu kwanza uushinde woga.

Dr Hill anasema:

These Basic six Fears are:

1. The fear of Criticism

2. The fear of ill health,

3. The fear of poverty

4. The fear of old age

5. The fear of the loss of love of someone (ordinarily called jealousy)

6. The fear of death

The Fear of Criticism (Uoga wa kulaumiwa/kuchekwa/kudharauliwa/kukosolewa) ndio namba moja, wengi wetu tunaogopa kuelezea ndoto, maono au malengo yetu kwa kuogopa kuchekwa au kudharauliwa iwapo tutashindwa zetu.

Huu ni uoga mbaya sana hatuna budi kuushinda ikiwa tunataka kuona maono/ndoto zetu zinakuwa kweli.

Pindi utakapoweza kuushinda woga huu itakuwa ni rahisi kwako kuushinda woga mwingine na hivyo kuwa katika njia sahihi kuelekea mafanikio, maono ama ndoto zako.

“Most great people have attained their greatest success just one step beyond their greatest failure.” Dr Hill

Kila mmoja katika nafsi yake anayo labda picha au ndoto ya wapi au vipi anataka kuwa siku za usoni, pengine wengine wamekubali woga kufuta ndoto zao na hivyo kutakuwa na maono tena, hii ni hatari, kwani pasipo maono/ndoto ya nani au nini wataka kuwa maishani ni sawa na chombo kung’oa nanga bandarini pasipo kujua wapi kinapaswa kuelekea, matokea yake upepo utakipeleka popote na kitapotea bila shaka.

“Man, alone, has the power to transform his thoughts into physical reality; man, alone, can dream and make his dreams come true.” Dr Hill

Ndoto yangu ni kufikia Uhuru wa Kipato (Financial Freedom) ili niweze kuwa na uhuru wa kufanya kazi pale nitakapo na niwatakao, lakini pia niweze kwenda popote nitakapo duniani kwa wakati niutakao nikiwa na muda mrefu wa kuwa na familia yangu huku pato likizidi kila uchao, ni ndoto ambayo nataka iwe kweli, nashukuru Mungu kwa kunionesha njia ya kufikia ndoto hii.

“Success consists of going from failure to failure without loss of enthusiasm.”Winston Churchhill

BOFYA HAPA KWA MAWASILIANO ZAIDI
 
Mkuu nashukuru sana, Binafsi natafuta sana materials ya self Motivation ili niweze kujijenga zaidi kisaikolojia,,, Kama unaweza kunipatia Reference wapi naweza kuyapata nitashukuru sana Ndugu.

Stay Blessed.
 
Mkuu nashukuru sana, Binafsi natafuta sana materials ya self Motivation ili niweze kujijenga zaidi kisaikolojia,,, Kama unaweza kunipatia Reference wapi naweza kuyapata nitashukuru sana Ndugu.

Stay Blessed.

www. Selfconvidence.com
 
www. Selfconvidence.com

Asante mkuu Ivuga kwa Link hiyo, ni nzuri sana na ni moja wapo ya links za kufaa kwa kujenga kujiamini, kwa self motivation tembelea link iliyo chini ya hiyo thread utakuta links mbalimbali, pia tafuta vitabu vya kina Napoleon Hill, Robert Kiyosaki, Paul Zane pilzer, NK ni vizuri sana.

Be Blessed.
 
Back
Top Bottom