FBME yajibu taarifa za benki kuu ya Cyprus

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Maamuzi yanayosemekana kwamba ni ya “Mwisho” yaliyochapishwa na FinCEN Ijumaa, Machi 25, 2016, sio kweli kabisa kwamba ni ya “mwisho”. Bado yapo chini ya amri ya zuio la awali la mahakama ya shirikisho ya Washington DC ambayo inazuia maamuzi haya kufanya kazi na kuleta athari ikisubiri uchunguzi zaidi wa mahakama hiyo katika masuala ya haki, usahihi na uhalali wa mchakato wa FinCEN. “Maamuzi ya Mwisho” pia yana masharti yake yenyewe, kwamba ni lazima yasubiri kipindi cha miezi mine baada ya kuchapishwa rasmi na tarehe ya utekelezaji wa maamuzi hayo. FBME ina haki zote na nia ya kupinga uhalali wa “Maamuzi ya Mwisho” ili mahakama ya Marekani iweze kuamua kama ni halali maamuzi hayo kufanya kazi.

Wala madai ya FinCEN kwenye “Maamuzi ya Mwisho” hayajabadili jambo lolote ukilinganisha na madai ya awali yaliyosababisha zuio la mahakama. FinCEN wamerudia makosa yaleyale na kuleta tena ushahidi wa kiujanja ujanja kwenye maamuzi yake ya Mwisho. Makosa haya – yanayoleta masikitiko lakini yaliyotarajiwa yanaipeleka FinCEN kwenye maamuzi potofu ya sheria maalum inayoitwa “Fifth Measure”. Tunadhani ni dhahiri kwamba kwa hatua hii FinCEN imeonyesha ukaidi mkubwa kwenye hitimisho lake lisilofuata taratibu za ushahidi, ukweli, sheria, maoni ya umma, au kusimama kwenye misingi ya usawa.

Pongezi kwa mfumo wa kimahakama, ratiba, na zuio la muda lililopo, hata hivyo, siku ya mahakama ya FBME inakaribia. Tunasisitiza kwamba tuna kila nia ya kuipinga FinCEN kwenye Maamuzi yake ya Mwisho kwani yana kasoro kubwa kimchakato na yasiyo na mantiki na tunaisubiri kwa hamu siku ya mahakama.

Maoni zaidi ya Umma kwa Mapendekezo Ya Hukumu ya FinCEN


Februari 9, 2016

Maoni ya Umma yamewasilishwa kwenye Idara ya Hazina ya Marekani FinCEN kufuatia Ilani yake ya Mapendekezo ya Hukumu dhidi ya Benki ya FBME. Haya yanafuatia ombi la FinCEN kutoka kwa jaji Cooper wa Mahakama ya Wilaya ya Columbia ya Marekani ili kuyapitia upya madai yake na mapendekezo ya hukumu.

Continue reading →

Maoni kutoka Kwa Profesa wa Chuo Kikuu cha Columbia
Februari 10, 2016

Maoni zaidi kwenye tovuti ya FinCEN kuhusu jinsi idara hiyo inavyoshughulikia kesi ya FBME, yamewasilishwa na Sharyn O’Halloran, Profesa wa George Blumenthal katika Chuo Kikuu cha Columbia jijini New York. Katika barua yake iliyotumwa kwa FinCEN na kuwekwa kwenye tuvuti ya umma, Profesa O’Halloran alieleza kuwa eneo lake la kitaalamu ni utafiti wa michakato ya utawala ya Marekani, mamlaka ya kisheria na majukumu ya usimamizi.

Continue reading →

Wanasheria wa FBME Watoa Taarifa kwa Umma kuhusu Maamuzi ya Mwisho ya FinCEN
Januari 27, 2016

Wanasheria wanaofanya kazi kwa niaba ya FBME wametoa Taarifa kwa Umma kuhusu mapendekezo ya maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na Idara ya Hazina ya Marekani – FinCEN. Inatarajiwa kwamba taarifa hiyo itaonekana kwenye tovuti ya FinCEN na nakala kamili inapatikana hapa.

Rais Ajibu Barua ya Mwenyekiti wa FBME
Januari 19, 2016

Rais wa Jamhuri ya Cyprus, Bw Nicos Anastasiades, ametuma jibu fupi kwa barua ya Desemba 27 kutoka kwa Mwenyekiti wa Benki ya FBME, Ayoub-Farid M Saab (ambayo inaweza kupatikana kwenye tovuti hii).

Akiijibu barua hiyo kutoka Mr Saab, Rais amesema kwamba kwa sababu suala lipo chini ya mahakama si yeye wala waziri yeyote anayeweza “… kuingilia kati, kuzungumzia au kushawishi maamuzi na utaratibu unaoendelea”

Mahakama ya Cyprus Yaizuia CBC Kubatilisha Leseni
Januari 19, 2016

Mahakama nchini Cyprus imeamuru kusimamisha hatua iliyochukuliwa na Mdhibiti wa benki yenye lengo la kuifilisi Benki ya FBME tawi la Cyprus. Hii inafuatia jaribio la kufutiwa leseni ya tawi lililotangwa kwa umma na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) tarehe 21 Desemba 2015.

Continue reading →

CBC Yateua Msimamizi Maalum Mpya
Januari 19, 2016

FBME imearifiwa kwamba Benki Kuu ya Cyprus (CBC) amemteua Msimamizi Maalum mpya kwa tawi la FBME Cyprus. Aliyeteuliwa Januari 11, 2016, akiwa msimamizi wa tatu tangu sakata hili lilipoanza Julai 2014, ni Bwana Chris Iacovides.

Continue reading →

Barua kwa Rais – Wito wa Kuanzishwa Upya Uchunguzi wa Maafisa wa CBC
Desemba 28, 2015

Mwenyekiti wa Benki ya FBME, Bwana Ayoub-Farid M Saab, ameandika Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Cyprus, Nicos Anatasiades, kuonyesha madhara makubwa yaliyosababishwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC). Vitendo vya karibuni vya CBC ni pamoja na jaribio la kuifutia leseni, si tu kwa tawi la FBME Cyprus, bali kwa Tanzania pia.

Continue reading →

Wenye Hatia Ni Nani?
Desemba 24, 2015

Tangia Julai 2014, mwanzo wa sakata lake dhidi ya Benki ya FBME, Benki Kuu ya Cyprus (CBC) imewapeleka wadau kwenye mlolongo wa kushangaza wa vitendo visivyo na mantiki vilivyoibua maswali muhimu kuhusu uaminifu wake kama chombo cha serikali katika siasa za kisasa za Ulaya. Kwa kipindi kirefu cha miezi hii 17, CBC ilikuwa kimya kueleza nia yake, na ni hivi karibuni tu ndio wameanza kuonyesha ukweli wa yale yaliokuwa yakiendelea nyuma ya pazia, na hii ni dalili ya kushindwa kwenye vita vya kisheria kwenye midani ya kimataifa.

Continue reading →

FBME Yapambana na CBC Kisheria dhidi ya Ubatilishaji wa Leseni Yake
21 Desemba 2015

FBME Limited imetangaza kuwa hatua za haraka za kisheria zitachukuliwa kupinga kusitishwa kwa leseni, kulikofanywa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) dhidi ya Benki ya FBME Tawi la Cyprus, na uamuzi huu kwenye mahakama ya Cyprus.

Tamko la ubatilishaji huo lenye kurasa 9 limewasilishwa leo Desemba 21, 2015, ikilaumu watendaji wengine kwa vitendo vilivyosababishwa na hatua zilizochukuliwa na Bodi ya CBC katika kipindi cha miezi 17, ambayo imetokana na CBC ilipofanya jaribio la uuzaji wa Benki ya FBME ya tawi Cyprus. FBME inapinga kabisa kubatilishwa kwa leseni hiyo.

Hatua hii ya kidhalimu ya CBC dhidi ya FBME, ambayo ni ya hivi karibuni, imesababisha kesi mbili nchini Cyprus na nje ya nchi, na kuziacha mamlaka za Cypruskwenye mlolongo wa madai ya uharibifu mkubwa na fidia.

FBME Yaja na Mpango Wa Kuwafungulia Milango Wateja Wake


Oktoba 31, 2015

Benki ya FBME imeanzisha mipango ya kuhamisha amana zilizoko katika tawi la Cyprus kwenda kwenye ofisi za makao Makuu nchini Tanzania, ambapo kwa njia hii itawawezesha wateja wake kupata fedha zao. Hii inafuatia hali ambapo wateja wamekuwa na vikwazo vya kuchukua kiasi kidogo cha EUR 1,000 kwa wiki na wakati mwingine wamekuwa wakiwekewa Ukomo kwenye akaunti zao kwa amri ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC), ambayo walichukua udhibiti wa FBME tawi la Cyprus mwezi Julai 2014.

Continue reading →

Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ICC inaona inayo mamlaka Kusuluhisha Kesi kati ya Wamiliki wa Benki ya FBME na Jamhuri ya Cyprus
Septemba 16, 2015

Kwenye maamuzi yake yaliyosainiwa tarehe 10 Septemba 2015, Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris aliamua kwamba ina mamlaka juu ya madai ya wamiliki wa FBME Limited (Wadai) dhidi ya Jamhuri ya Cyprus (Washtakiwa) kuhusu Mkataba wa Lebanon-Cyprus unaosimamia ulinzi wa haki za mwekezaji.

Continue reading →

Mahakama ya Wilaya ya Marekani Yaweka Zuio la Mwanzo dhidi ya FinCEN na Maamuzi yake ya Mwisho.
Agosti 28, 2015

Mnamo Agosti 27, Mahakama ya Wilaya ya Columbia, wamekubali kuweka pingamizi la awali dhidi ya FinCEN na washitakiwa wengine wa Marekani na kuzuia Maamuzi ya Mwisho ya FinCEN yasifanye kazi hadi hapo Mahakama itakapotoa humumu yake ya mwisho, kama ilivyoombwa na FBME Limited na Benki ya FBME Limited. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye amri ya mahakama kwakubofya hapa.

Continue reading →

Uamuzi wa FinCEN Una Makosa Mengi ya Ukweli na Kisheria
Julai 27 2015

FBME Limited imeisoma hukumu ya mwisho ya Taasisi ya Kuangalia Makosa ya Kifedha ya Idara ya Hazina ya Mrekani (FinCEN) iliyotolewa tarehe 23 Julai 2015, na kutoa taarifa ifuatayo:

Uamuzi wa FinCEN hauwezi kuachwa kukosolewa. Ingawaje Benki na washauri wake walifanya juhudi kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuelezea mifumo ya kupambana na fedha chafu AML na uendeshaji, miamala na shughuli nyingine, makosa makubwa ya kisheria na upotoshaji wa ukweli yaliyomo kwenye hukumu hiyo ya mwisho inaonyesha kwamba iliandikwa na watu bila kutilia maanani maelezo muhimu tuliyowapelekea sambamba na nyaraka nyingine walizokwisha kuwa nazo.

Benki inakusudia kutafuta njia yoyote inayowezekana kujilinda ipasavyo dhidi ya udhalimi huu kwa kufungua kesi kwenye mahakama ya Washington DC dhidi ya Idara ya Hazina ya Marekani.

Taarifa zaidi zitatolewa katika wakati muafaka kupitia tuvuti hii ya www.fbmeltd.com

Kila Mmoja Anaathirika na Sakata hili
19 Julai 2015

Tarehe 17 Julai 2014, mlolongo wa matendo ulianzishwa ambao ulikuwa na madhara makubwa kwa wateja, wafanyakazi na washirika wa Benki ya FBME, ndani na nje ya nchi. Watu wamepoteza kazi zao na makampuni yamefungwa. Aidha, kuna waathirika wengine ambao wameanza kuhisi athari kwa sasa – walipa kodi, serikali, mamlaka ya benki na mfumo wa haki wa kisiwa cha Cyprus. Katika ujumbe huu, Benki ya FBME inatoa maoni yake juu ya nini kimetokea.

Continue reading →
 
Back
Top Bottom