Favourite Drinks: Kinywaji Kipi Unakizimia Sana...(Alcoholic & Non-alcoholic)

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
TGIF:

--WanaJF, ni drink gani mnazimia sana?!! Tuelezane tafadhali nasi tupate kujaribu kama tunakutana navyo! :)

--Kwa vinywaji baridi, mimi napendelea Fanta Tropical - yenye baridi kwa sanaa, chupa ukiitikisa vi-ice vinalenga lenga ndani! ;) ....hiki kinywaji kiboko hasa kwa hapa Bongo jua linapokuwa liko utosini!

--Kwa vinywaji moto, mimi napendelea brandy yenye mwonjo wa apricot... drink hii ni poa sana, unaweza ukanywa kavu kavu au ukaweka mix yako uijuayo bado inashuka kooni kilaini tu. Miye nina 'secret' ingredient hutumia na kupata cocktail moja - usipime! (nime weka patent samahani siwezi ku-reveal kirahisi)

--Kwenye mambo ya beer, Stella, Becks, Heineken, Grolsch, Carlsberg Export zinanitosha kama chaguo popote nizikutapo. Budweiser saa nyingine hunichefua kwa radha yake ambayo huonekana kama artificial vile....

Naomba maoni yenu, ahsante.

SteveD.
 
Kama siginecha yangu mie hupenda Bia badala ya maji....

Katika bia hupendelea bia
Karhu
karhu_A1.png

Karjala
394_Karjala.JPG

Kilimanjaro, stella na Carlsberg
 
Nikiwa Zenj...Kinywaji moto ni Tende, asusa Vibua,katiresi, embe mbichi na mapera
 
---Kibunango, signature yako kiboko!!..... lol, BTW, hiyo beer hapo juu ni zile za kutoka India au?

Nikiwa Zenj...Kinywaji moto ni Tende, asusa Vibua,katiresi, embe mbichi na mapera
---aaah, mimi nikiwa huko sichezi mbali na maji ya dafu..... hapo nakuwa siwezi kwenda wrong na kuingia kwenye cultural bish bash!!
 
Kibunango, signature yako kiboko!!..... lol, BTW, hiyo beer hapo juu ni zile za kutoka India au?
Kamanda, Ni bia toka Finland.... Jamaa wa mitaa ya huku wanapenda sana kunywa... Na Serikali yao inathibitisha hilo kwa kutoa ruhusa siku ya Ijumaa na Jumamosi ni ruska kunywa bia ndani ya public bus(daladala)
 
---Kibunango, signature yako kiboko!!..... lol, BTW, hiyo beer hapo juu ni zile za kutoka India au?

---aaah, mimi nikiwa huko sichezi mbali na maji ya dafu..... hapo nakuwa siwezi kwenda wrong na kuingia kwenye cultural bish bash!!

Maji ya dafu ni hatari shauri yako usiyazoee sana!yanaaminika kusababisha ugonjwa wa mabusha
 
Maji ya dafu ni hatari shauri yako usiyazoee sana!yanaaminika kusababisha ugonjwa wa mabusha
Hollo, miye naamini kuwa kila kitu ukitumia in moderation hakina madhara sana.... unless hicho kitu ni sumu tayari at its natural state.... natumaini unanipata.
 
Fanta pinneaple na ulanzi, vikikosekana hivyo nakunywa maji!

Mama, mimi nilifikiri wewe ni teetotaler .... ;) kumbe nawe ulanzi unapanda.... ha ha ha.. Je ni ule wa Kihesa, Makanyagio au wa kutoka Tosamaganga?!.... lol
 
Mama, mimi nilifikiri wewe ni teetotaler .... ;) kumbe nawe ulanzi unapanda.... ha ha ha.. Je ni ule wa Kihesa, Makanyagio au wa kutoka Tosamaganga?!.... lol

wa tosamaganga bwana kihesa rahisi kupata mkangafu, kwi kwi kwi
 
wa tosamaganga bwana kihesa rahisi kupata mkangafu, kwi kwi kwi
......maana unakuwa adulterated beyond imagination!... Kule Kawe na Mikoroshoni tembo lao haliaminiki pia...
 
......maana unakuwa adulterated beyond imagination!... Kule Kawe na Mikoroshoni tembo lao haliaminiki pia...

kwi kwi kwi, tembo ndio unalizimia sio! lizy yeye na wanzuki ha ha haaaa, yaani sina mbavu hapa. Kuna kinywaji kinaitwa dadiii (kinatengenezwa na mahindi) maeneo ya Arusha na kingine maeneo ya Mbulu kule jina nimelisahau (kinatengenezwa kwa mtama) hivi navyo sio vya kipole pole.
 
Maji na Chai ya rangi.

Kilevi napendelea WANZUKI.

--Lizy, chai ya rangi ina kajina kengine "chai ya strungi"..... neno strungi nadhani limetokana na neno la kiingereza 'strong tea', am i right?

--btw, wanzuki si ndiyo ile inayotumia asali kama main ingredient... au?
 
Yote tisa, ngoja ije Julai. Bei juuu. Kwa hio anzeni kuandaa mbege, ulanzi , gongo n.k kwa wingi.
 
Yote tisa, ngoja ije Julai. Bei juuu. Kwa hio anzeni kuandaa mbege, ulanzi , gongo n.k kwa wingi.

Mfamaji, usitahamaki kukuta vileo vinashuka chini, ila bei za mchele, mahindi , ndizi na uwele ndizo zinapanda zaidi ya hivi ilivyo sasa.....
 
Back
Top Bottom