Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

mfano...............
acha uchokozi mdau.
wacha msiba upite bana.
hakuna anayemwombea mwanadamu mwenzake mauti mkuu.
hata kama viongozi wetu ni wabaya,wabovu na wala rushwa.
kuwaombea mauti si utu.
 
Sikumfahamu Regia personally. Ni mfuatiliaji tu wa this and that.But my heart is in unbearable pain to lose her. For us believing in future, there was something in this young lady. We will miss her!!
 
The hidden wounds of the heart and soul are often more difficult to diagnose and harder to heal R.I.P HON REGIA MTEMA
GOD GIVES AND GOD TAKES
 
Mwanakijiji, tumepoteza hazina kubwa sana, mpiganaji na mwakilishi wa watu.Kwa lugha ya kuazima " she was open like a newspaper and louder than a public address system".Ndio maana maelfu ya members hapa tunajificha nyuma ya pazia lakini yeye all along ametoka open from day one, wachache Wana moyo huo wa ushujaa Tuna mengi ya kujifunza toka kwake, tutalia sana, tutaandika sana, tutasema sana. Lakini Regia amemaliza kazi aliyotumwa kuifanya na mwenyezi mungu, tuliobaki inabidi tujiulize ni vipi tutamuenzi Regia?
 
Nyota iliyozimika ghafla.
ni mlemavu ambae alisimama imara ktk mstari wa mbele wa mapambano,alijulikana pembe zote kwa kazi zake,ushupavu na ujasiri mkubwa,mara ya mwisho Ruvuma alituamsha vibaya ktk kongamano la katiba,
rest in peace Regia.
 
Goodbye our rose
May you ever grow in our hearts
You were the grace that placed itself
Where lives were torn apart
You called out to our country
And you whispered to those in pain
Now you belong to heaven
And the stars spell out your name
And it seems to me you lived your life
Like a candle in the wind
Never fading with the sunset
When the rain set in
And your footsteps will always fall here
Along Tanzania's greenest hills
Your candle's burned out long before
Your legend ever will
Loveliness we've lost
These empty days without your smile
This torch we'll always carry
For our nation's golden child
And even though we try
The truth brings us to tears
All our words cannot express
The joy you brought us here in JF
And it seems to me you lived your life
Like a candle in the wind
Never fading with the sunset
When the rain set in
And your footsteps will always fall here
Along Tanzania's greenest hills
Your candle's burned our long before
Your legend ever will
Goodbye our rose
May you ever grow in our hearts
You were the grace that placed itself
Where lives were torn apart
Goodbye our rose
From a country lost without your soul
Who'll miss the wings of your compassion
More than you'll ever know
And it seems to me you lived your life
Like a candle in the wind
Never fading with the sunset
When the rain set in
And you footsteps will always fall here
Along Tanzania's greenest hills
Your candle's burned out long before
Your legend ever will

Hata sijui cha kusema,macho yangu yamejaa machozi,
roho inaniuma,natamani niwe niko kwenye ndoto,
naiona jf imepooza sana leo,eeh Mungu tutie nguvu maaana hili ni pigo kubwa sana kwetu.Poleni ndugu zangu kwa msiba huu uliotufika,pia tusisahau kuwaombea familia ya marehemu.
 
..kwa kweli nikiangalia hiyo picha yake hapo machozi yananitoka.

..kifo chake kimenigusa, pamoja na kwamba sikuwahi kuonana naye zaidi ya michango yake hapa JF.

..kama kuna mwanasiasa au mbunge ambaye nilikuwa nikimuombea afanikiwe katika harakati zake basi ni huyu Regia Mtema.

..It is really hard to accept that she is no more.
 
Huu msiba umeuma sana... Ni pigo kubwa kwa wapenda maendeleo wote Tanzania.

Inna Lillaah Wainna Illaihi Raajiun.
 
Inna liLlahi wa Inna iLlahi Rajiun.

Moja katika siku ambayo sitoisahau katika maisha yangu ni leo. Baada ya kufunguwa JF kama kawaida yangu na kukutana na habari za kututoka Regia haikuwa kama kawaida yangu tena. Nna uhakika haitokuwa kawaida kwangu tena.

Regia na mimi binafsi tumeshakuwa na "heated debates" za kutosha humu jamvini za kutufanya tuwe na "invisible bond" somehow, lakini nna uhakika yote si katika kubomoa, yote ni katika kujenga kwa kila mmoja wetu kwa muono wake.

Kweli kifo ni kwa kila mmoja wetu na hakuna atakae kiepuka, ukweli ni kwamba kifo hiki kimenistuwa sana kupita kiasi. Nilipofiwa na mama yangu mzazi ilinichukuwa wiki nzima, baada ya kumaliza msiba na kusafirisha wageni waliokuja msibani, kuanza kuona upweke na "gap" aliyoiacha maishani mwangu, cha kusikitisha ni kuwa, kifo cha Regia kimenitia upweke na "gap" kubwa nnaiona immediately. Kila ntapofunguwa kurasa za JF ntamkumbuka Regia.

Nashindwa kuandika zaidi jamani, ni msiba mzito sana, si kwa wana CHADEMA pekee bali kwa Taifa zima. Kuondokewa na kijana mdogo ambae alikuwa ana uhakika wa kuleta mabadiliko ni pigo kubwa sana, nnatumai ataemrithi wadhifa wake atapigania, kuheshimu na kuyaendeleza yote mema aliyoyadhamiria Regia.

Poleni sana ndugu, jamaa na marafiki wa Regia, Poleni sana Taifa, Poleni sana CHADEMA, Poleni sana wana JF wote.
Pole FF, tumeguswa wengi!.

Mode nawaombeni for the sake of Regia, msiziunganishe hizi thread kwa sababu kila moja inabeba ujumbe tofauti hata zikifika 100!. Baada ya Mazishi ndipo mziconsolidate!.

Pole tena FF na wengine wote.
RIP Regia!.
 
Kwa wana JF na Watanzania she was too young to die kwa kuwa tulimpenda lakini Mungu alimpenda sana R.I.P Regia binti wa Nchi.
 
tunashukuru kwa pole zako.mwenyezi mungu amlaze mahali pema.r.i.p Regia hakika ulikua mpambanaji.
 
:lol::lol:nimestushwa, nimesikitika, nimehuzunika na sasa nimeduwaa na sina la kufanya kwa chadema na tanzania kuondokewa na mwanamapinduzi huyu kijana mbichi, regia. regia mtemanenda kwa amani, lala salama, nasi tupo njiani tunakuja kwani hiyo uliyokwenda ndiyo njia yetu sote kama siyo leo basi ni kesho au kesho kutwa. sote tupo safarini. tunamshukuru mungu kwa hizo siku chache tulizoishi nawe duniani.
aamen
 
Personally, sijawahi kukutana uso kwa uso na Regia. Lakini nimekutana nae sana kwenye mijadala mingi hapa JF na Facebook, kitu ambacho kimenifanya nijihisi kama vile namfahamu. Mara ya mwisho ku-debate nae hapa ilikuwa kwenye ile thread yake ya "Kwa hili Rostam Aziz hatasameheka" (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/179304-kwa-hili-rostam-aziz-hutasameheka.html).

Labda niseme tofauti na baadhi ya waheshimiwa wengine, alikuwa ni mtu wa kijichanganya. Alikuwa anachangia majukwaa almost yote mpaka kwenye michezo. Hata kule Facebook Regia hakuwa kama wale wengine wanaweka tuu status kwenye profile zao na kuishia bila hata kujibu hoja za wachangia wa status zao.

Regia alikuwa anachachangia kwenye status za watu wengine regardless of their status. Mara ya mwisho kumsoma Facebook, hakufurahishwa na picha moja iliyokata kichwa cha Rais Kikwete na kukiweka kwenye kiwiliwili cha picha ya mwanamke. Regia alisema that was too much labda sio tuu kwa vile victim alikuwa mkuu wa nchi bali pia hiyo picha ilikuwa inadharau jinsia ya kike.

Regia ametuacha kimwili lakini kiroho bado tutakuwa nae. Hivyo basi, tuyatukuze, tuyatangaze, na kuyatekeleza kwa niaba yake yale yote mema aliyokuwa amekusudia kuyafanya kwa manufaa ya jamii ya Tanzania. Thread yake ya mwisho hapa JF ilikuwa ni ya kukusanya kero, maoni, ushauri na chochote kutoka kwa WanaJF ambazo tungependa zisemewe bungeni na nje ya bunge (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ge-na-viongozi-wa-chadema-12.html#post3124894). Kama walivyosema wengine, ni kama vile alikuwa mbunge wetu hapa JF.

Rest in Peace Regia.
 
Wt can I say, kiukweli tumepoteza kiongozi, mwanamke shujaa anayejitambua ambaye ni mpigania haki za wanyonge wa nchi hii iliyochakachuliwa, pumzika kwa amani kipenzi. tutakukumbuka daima
 
Inaumiza sana kumpoteza dada mstaarabu kama Regia,sikumfahamu kwa kuonana nae zaidi ya michango yake na maada zake za dhati hapa JF.
Machozi yananitoaka kila nifikiriapo kua sitoyapata tena mawazo yake wala kuona akileta maada,update za mikutano ya chadema.machozi yananitililika.
Nawapa pole za dhati Ndugu zake wa karibu na wale wote waliokua karibu nae kama MMM,Kwani najua wao wanawakati mgumu zaidi maana walikua nae muda mwingi zaidi yangu na wanaJF wengine tuliomfahamu kupita hapa na Bungeni.RIP dada yetu mpendwa.
 
Back
Top Bottom