Faraja Mlelwa, diwani mteule CHADEMA Mlangali/Ludewa analo la kutufundisha

This is new ideology. Anatoa wigo mpana wa kuwafikia wananchi wa chini kabisa na atajenga chama sana.

Naomba mmoja wetu atangaze nia ya kugombea udiwani. Ubunge tumewasikia.
 
Poa sana Kamanda hongeara kwa kushinda sasa nenda kawakimbize hao madiwani wa Ccm waliomaliza darasa la saba pia nakuomba uwafundishe atleast kwani pia itasaidia kwa taifa zima waelewe nini wafanye na sio ndio mzee
 
Dah hadi raha...wengine tuige mfano wa huyu jamaa.Tuondoke kwenye sifa za hapa JF na kwenda kwenye utekelezaji
 
Nimefarijika sana. Hivi ndivyo siasa inavyotaka na ndio njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani. Madiwani wengi walioenda shule watasaidia kuwaamsha wananchi katika maeneo ya vijijini ambako ufahamu badi ni tatizo, vitisho na uongo bado vinapokelewa na kuaminiwa.
Kijana amenikumbusha mwaka 1994 nikiwa mgombea kupitia NCCR kwenye kata kijijini ambako ilisaidia kuamsha ari ya vijana kwa kiasi kikubwa. Amkeni vijana. Maneno matupu hayalambwi!!!!!!
 
Well done Faraja Mlelwa! Wako wengi wanao-comment kiunafiki, lakini kiukweli kijana Faraja ulichokifanya ni mfano wa kuigwa kwa vijana wengi wanaodhani kuwa na elimu ya juu ni lazima upate kazi katika ngazi za juu. Hujakosea njia, cha msingi ni kukomaa. Pia ingendeza sana kama ungekuwa member wa humu ndani, ili uwe una-share experience za vikao vya mabaraza, na changamoto unazoziona kwa nia njema tu.

Waweza kutufungulia ukurasa mpya wa ulimwengu wa siasa kwa tz kama ambavyo mwingine kasema hapo juu. Pia ikawavutia vijana wengine wenye uwezo kama wako na juu zaidi kuweza kupanua uwezo wao wa kufikiri. Not necessarirly na wao wakawa madiwani wa CDM pia wanaweza kuwa wa CCM. Kwani tunahitaji ni mabadiliko na maendeleo ya kweli.

Natumaini uamuzi huu umeufanya kwa nia ya kuleta maendeleo, kila la heri Faraja Mlelwa, Mungu akuepushe na tamaa mbaya.
 
Faraja ni Hazina na mwanzo mzuri kwa chama na yeye mwenyewe.Tengeneza mikakati kwa ajili ya political growth na muda huu ni mzuri kwajili ya kuangalia nafasi ya Ubunge au baadaye Uenyekiti wa Hlamshauri.Kwa ELIMU YAKO YA IDS najua mambo ya rural poverty,development,social services umebobea. Kila la heri
 
Sawa mkuu nakupongeza sana kwa hilo ni changamoto kwetu sisi, najipanga T2015CDM
 
Mimi nampongeza sana kwa kufuata nyayo zangu japo mimi walinichakachua, ila 2015 ninao!!!
 
Nimeipenda hii, juzi nimebishana sana na watu wanaoamini chadema inakuwa taratibu kulinganisha na umaarufu wake, mi nasema hapana chadema inakuwa kwa kasi sana kuliko inavyoonekana lakini ina tatizo la wagombea wenye uwezo wa ushawishi na hasa hawa wa chini
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom