Faraja Mlelwa, diwani mteule CHADEMA Mlangali/Ludewa analo la kutufundisha

Hongera zako mkuu
Atimize kile alichotumwa na wananchi waliompa kura na afanye kazi kwa uadilifu
 
Yani nafanya kazi kwa bidii ili mwakani nijiajiri nikaunganishe nguvu ya ukombozi SHINYANGA.
 
Hata mimi nampongeza sana Diwani Mteule Faraja Mlelwa kwa kuamua kwa dhati kutafuta nafasi ya kuwatumikia wananchi kwa nafasi ya udiwani bila kujali kiwango kikubwa cha elimu alicho nacho.
Kumekuwa na tabia za wasomi wengi wa siku hizi kwamba mtu akishakuwa na shahada moja tu yeye anawaza kuwa mbunge tu na si chini ya hapo.
Huko kwenye halmashauri zetu ndiko kuna matatizo makubwa kwahiyo tukipata wasomi wengi kwenye level ya udiwani basi hapo tunakuwa na mabaraza ya halmashauri yaliyo mahiri na makini, na bila shaka utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo hautakuwa wa kusuasua tena kama ilivyo sasahivi.

Hii ni changamoto kwa vijana wengi waliojiunga Chadema kila mmoja aanze kufikiria ni kata ipi inayomfaa kuwawakilisha wananchi kupitia Chadema na waanze maandalizi ili kufikia 2015 tusitarajie tena makapi ya ccm ambayo yamejidhihirisha kuwa hayana msaada wowote kwa ustawi wa chama na maendeleo ya wananchi.
 
nafikiri huyu jamaa ni wa mfano kwelikweli,ni kwakuwa mimi ni dr na napenda kazi hii ya udaktari kwani naamini pia ni kuwatumikia walipa kodi,wa tz vinginevyo 2015 ningeenda kugombea udiwani ktk kata ya kirongwe(usangi) au uenyekiti wa kijiji cha vuagha ili kusaidia kuleta maendeleo haraka zaidi
 
Na nyie akina Maiko Msafiri, akina Beda Mwang'onde na wasomi wengineo igeni mfano huo kule Milo.
 
Faraja Mlelwa amepiga penyewe, mimi nimefurahishwa na uamuzi wake, huyu kafungua ukurasa mpya wa siasa za tanzania ili baadae watu waondokane na tabia ya kusema ajira hakuna, wasomi wengi wanataka ajira ktk ofisi zenye viyoyozi tu ajira nje ya hapo wanaona bureeeeeeeeeeeeeee.

Leo mlelwa katoa somo, kwamba ajira zipo ila tatizo ni kuziibua, tulikuwa tumezoea kuacha nafasi za diwani kwa darasa la saba na la nne huku tukijua kwamba pesa nyingi za serikali zinapelekwa ktk halmashauri za wilaya ambapo wasimamizi ni madiwani ambao elimu zao ni tia maji tia maji.Leo Mlelwa kafungu bandora box akauonyesha umma kwamba HAKUNAGA KAMA UDIWANI.

cdm andaeni vijana kwa wazee wasomi waende kugombea udiwani ili tutokana na dhana ya kudharau diwani, diwani kwa sasa ananatakiwa awe msomi zaidi ya mbunge kwani huyu ndiyo anasimamia utekelezaji wa bajeti ya serikali, kwa kusimamia miradi yote ya maendeleo.KARIBU FARAJA UFARIJIKE NA KAZI YA UDIWANI
 
Huko kwenye halmashauri zetu ndiko kuna matatizo makubwa kwahiyo tukipata wasomi wengi kwenye level ya udiwani basi hapo tunakuwa na mabaraza ya halmashauri yaliyo mahiri na makini, na bila shaka utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo hautakuwa wa kusuasua tena kama ilivyo sasahivi.

Mkuu Mwita Maranya hapa umeongea kweli kabisa maana ili nyumba iwe imara lazima msingi wake uwe madhubuti pia...
 
Last edited by a moderator:
Hongera kijana, hata mimi nikimaliza ka-master kangu mwakani narudi Tz kwa nguvu mpya, kazi ni moja. nataka nifanye kitu kwa ajili ya nchi yangu, maneno matupu hayatusaidii, wee need to get into the game, walk the talk kama mdaau alivyosema.
 
Hata mimi nampongeza sana Diwani Mteule Faraja Mlelwa kwa kuamua kwa dhati kutafuta nafasi ya kuwatumikia wananchi kwa nafasi ya udiwani bila kujali kiwango kikubwa cha elimu alicho nacho.
Kumekuwa na tabia za wasomi wengi wa siku hizi kwamba mtu akishakuwa na shahada moja tu yeye anawaza kuwa mbunge tu na si chini ya hapo.
Huko kwenye halmashauri zetu ndiko kuna matatizo makubwa kwahiyo tukipata wasomi wengi kwenye level ya udiwani basi hapo tunakuwa na mabaraza ya halmashauri yaliyo mahiri na makini, na bila shaka utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo hautakuwa wa kusuasua tena kama ilivyo sasahivi.

Hii ni changamoto kwa vijana wengi waliojiunga Chadema kila mmoja aanze kufikiria ni kata ipi inayomfaa kuwawakilisha wananchi kupitia Chadema na waanze maandalizi ili kufikia 2015 tusitarajie tena makapi ya ccm ambayo yamejidhihirisha kuwa hayana msaada wowote kwa ustawi wa chama na maendeleo ya wananchi.

Umesema kweli mkuu... Mimi kama kijana nitahakikisha nasimamia msingi huu uliousema...
 
hongera Faraja!! amenikumbusha mbali sana,halafu jamaa wazazi wake wote ni Walimu,mama yake kanifundisha katika shule ya MSINGI ULONGE wakati huo babake akiwa HEADTEACHER katika kata ya luwana.kwa kuwa nilikuwa kichwa kila siku saa 4 na mchana nilikuwa naenda kula chakula kwa kuwa kwetu kulikuwa choka mbaya.kwa kweli hongera saana!na MUNGU AKUBARIKI.kama unapitia humu naomba namba yako tafadhali.
 
Hongera sana, watumikie wananchi wasaidie kutatua matatizo sugu ya wananchi ndo maana wamekupa ridhaa
 
ataongoza mapambano 2015 wakati wa kumkaribisha deo firikunjombeeeeeee
 
kwako faraja,
wewe ni Paka(figuratively) umeingia ndani ya shimo lenye panya wengi waliozoea kutafuna kwahiyo basi nakupa headup
kwenye vikao vya halmashauri mtu pekee watakayemtazama kwa jicho baya ni wewe pekee kwa sababu wanajua kazi yako
ni kupambana na panya waliozoea kutafuna kwahiyo kaza buti zako vizuri tegemea kuwa treated different from the beginning psychologically kwanini?? wewe ni paka kwahiyo hawatakuwa comfortable mbele yako. elimu yako pia ni kikwazo kwa watu waliozoea kuendesha mambo kimazoea kwahiyo tegemea upinzani kutoka kwa watu wasiopenda mabadiliko kwahiyo una challenge kubwa kuliko kwani wewe ndiye utakayeinua chadema wilaya hiyo au kuiua. wananchi wanakupima wewe ndiye utawaonyesha njia kuwa upinzani ni nini??

Hongera sana kwa uamuzi wako wa kutumikia umma.
once again hongera sana Diwani faraja
 
Back
Top Bottom