Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,799
- 59,263
Watu hawaishi kuuliza kama inawezekana kuwa na mtu ambae yuko mbali nae na mahusiano yao yakasurvive.
Jibu ni NDIO, ila kuna mambo ambayo mnatakiwa mzingatie ili mfanikishe mahusiano yenu.
First things first...
1.Kama wewe ni mtu ambae una "commitment issues" this is not for you.Kuweza kuvumilia kutokuwepo kwa mwenzio karibu kunahitaji kujitoa kwa hali ya juu na dhamira iliyonyooka.
2.Kama humpendi mwenzako (unamtamani tu) this is not for you. Ukiwa unatamani kitu ambacho hukipati kwa wakati ni rahisi kuangalia kile kilichopo karibu yako.
3.Kama humwamini mwenzi wako/mwenzi wako hakuamini wewe au wewe mwenyewe hujiamini this is not for you. Bila kuaminiana mtakua na mtafaruku kila siku. Umbali utasababisha maneno/kuwekana hatiani na kuhisiana vibaya kuwepo sana.Kitu ambacho kitasababisha ugomvi mara kwa mara na kusababisha mrudi nyuma kimahusiano badala ya kusonga mbele.
4.Kama huna malengo ya mbali na mwenzako this is not for you. Ikiwa huoni ukiwa na huyo mwenzako miaka miwili mitatu mbeleni mwache aende tu. Hamna haja ya kumfunga mwenzako na mahusiano ya mbali wakati hana umuhimu sana kwako.
5.Kama ni mwepesi wa kuchukua maneno ya watu bila kuyafanyia kazi this is not for you.Utaishia kupata presha bure na kugombana na mwenzio kila siku.
6.Kama ni mvivu wa mawasiliano this is not for you. Kitu pekee kinachoweza kukuweka karibu na mwenzako wakati mko mbali mbali ni mawasiliano.E-mail, Simu, Texting, Skype n.k ndivyo vinavyoweza kupunguza umbali uliopo kati yenu walau kidogo.Hivyo kama hili huliwezi basi jua fika ni muda tu haujafika wa mahusiano yenu kuanguka.
Kwa wale ambao wanafikiria kujiingiza kwenye mahusiano ya mbali jua inawezekana ikiwa tu una nia ya kuyawezesha mahusiano yenu.Kama huna bora uende uendako siku ukarudi na kumkuta mwenzako bado yuko yuko ndio ujaribu.
Kwa wale ambae ndio wanahangaika nayo sasa hivi muhimu ni uwe mwaminifu,uwe na imani na mwenzako,ujitume kwenye swala zima la mawasiliano na msisahau kuongelea "them good times".Hii inasaidia kukumbushana umuhimu wenu kwa kila mmoja na kwamba japo mnakosana kwa muda, mtakapoweza kuwa karibu tena maisha yenu yatapendeza. Mjali mwenzako kwa maneno mazuri, epuka kuanzisha maugomvi yasiyo na pembe wala mkia, usimpe sababu ya kufurahia umbali wako.
Mwisho. . . kama ni kucheat hata unaelala nae kitanda kimoja kila siku, unaekunywa nae chai kila asubuhi na kubebana kazini kila jioni anaweza kucheat, hivyo hili haliletwi na umbali bali tabia binafsi. Hivyo kama wewe ni mvumilivu go ahead and give it a try huku ukiomba na kuamini kwamba mwenzako nae yuko hivyo hivyo pia kama hajakupa sababu ya kufikiria vingenevyo.
Nawatakieni LDS(s) zitakazovuka na kukwepa vikwazo. Kila la heri wote mnaohusika.
PS
Mawazo zaidi na experience zinakaribishwa.