Fani za kiufundi

Kitia

JF-Expert Member
Dec 2, 2006
418
74
Ningependa kuuliza kuwa ni fani gani za kiufundi (vocational skills) ambazo zina haja sana ya kufundishwa vijana wetu wanaomaliza vidato vya nne na sita ili kuweza kuwapa stadi mbali mbali za kuweza kuajiriwa na vizuri zaidi kujiajiri wenyewe?
 
Kama lengo lako ni kusaidia vijana hao wajitegemee wajiaajiri au waajiriwe (hata kwa muda), nitazipanga kwa uzito
1. Ujenzi yaani Uashi na ikifuatiwa na Useremala.(kila siku ujenzi upo, aidha nyumba mpya au matengenezo, mijini na vijijini, mtaji (vifaa ni bei rahisi, workshop iko site huhitaji ofisi.

2. Ufundi umeme - kama ujenzi unaendelea, basi kwenye umeme nako watahitajika mafundi.

3. Fitters (samahani sijui kiswahili chake) kumeanza maendeleo ya viwanda vidogovidogo ambapo vitu vinaunganishwa hapahapa nadhani unaona DVD players,

Nyingine zinategemea sana mazingira aishio mtu,
 
Nionavyo ni kuwa mining na construction ni eneo ambalo linakua kiasi. Lina hitaji wataalamu wa levels zote kuanzia chini mpaka juu kabisa. Vijana wengi wakijifunza masomo haya ya ufundi na kuweka mikakati ya life time learning to keep themselves with the pace of technological advancement kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza ajira.
 
Hapa ufundi ulenge saana mazingira tuliyopo na uwezekano wa kupata azi pale mhitimu anapomaliza,.Fani zifuatazo zinafaa kwa cheti cha ftc au kwa cheti cha veta.
Umeme,uashi,ujenzi,kutengeneza computer na vifaa vingine vya electronics na uchoraji.
Kwa veta.kuna kushona nguo,kufuma,kupika,kupamba,ujenga,fundi uashi na mengine. Ni bora mtu asome kulingana na maisha ya mtanzania na kazi zinazotuzunguka na ambazo tuna uwezo wa kuzipata au kuzifanya kwa urahisi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom