Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,076
- 2,443
Wana MMU
Kuna rafiki yangu amekuwa kwenye ndoa karibia miaka 10 sasa .. Hivi majuzi ndoa yao imeanza kupata migogoro ambayo yeye binafsi hajui chanzo chake nini.. Mwazoni alihisi labda mkewe amepata "kidumu", kwahiyo akafanya uchunguzi lakini hajafanikiwa kuhakiki kama ndivyo au sivyo.
Kadri siku zinavyokwenda pale nyumbani panazidi kuwa pagumu kuishi.. Na hivi sasa ameaanza kuwa anakaa kwenye mabaa muda mrefu sana kuliko ilivyokuwa hapo awali maana ananiambia kuwa ni heri amkute mkewe ameshalala vinginevyo inakuwa na maneno ya kuudhi tu..
Jana tulikuwa baa moja mitaa ya Tegeta - Why Not PUB - tunapata biya na baada ya kuchangamka tukaanza kuongelea mahusiano ya ndoa - tulikuwa wanaume kama 8 hivi hapo kaunta na mmoja kati yetu ni mzee wa miaka karibia 60. Baada ya kutusikiliza kwa muda mrefu alitwambia sentensi moja halafu akaondoka. Hapa ninanukuu kauli ya mzee "..vijana sikilizeni..kuna familia ambazo haziolewi wala hazioi.."
Rafiki yangu alipofanya mahesabu ya haraka haraka upande wa familia ya mke wake aligundua kuwa katika watoto wa kike sita wa familia ya mke wake (mke wake ni nne), wote waliolewa na kuachika na wengine wawili wamezaa njee ya ndoa!
Je, ni kweli kuwa kuwa familia ambazo wazawa wa familia hizo ni lazima mahusiano yao ya ndoa hayawezi kudumu? (genetic/coincident/??)
Naomba kuwasilisha...