Familia ya teketea kwa moto

JosM

JF-Expert Member
Oct 11, 2008
679
17
wanaJF


Nimepata simu kutoka kwa rafiki yangu mmoja ananiambia nyumba imeungua
maeneo ya Magomeni Kagera pia inasadikiwa kuwa familia imeteketea na moto
huo. Chanzo cha moto huo inasemekana ni shoti ya umeme.

Kama kuna mwanaJF ambaye yupo eneo la tukio atusaidie kutupa habari
kamili
 
Duh Mungu awarehemu..
Jamani tunasubili news zaidi kwa wale wa migo migo mnaweza kutupa updates zaidi.
 
Naomba uthibitisho kaka, maana hiyo ni hatari sana kwakweli.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU PEMA PEPONI, AMINAA....
 
Ni kweli nyumba imeungua na familia ya watu watano waliokuwemo wote wameteketea kwa moto huo. Mama, Baba wajukuu wawili na housegirl na hata Kova amaethibitisha kutokea kwa tukio.

Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu.

Tiba
 
Very sad indeed! Mmoja wa mtoto wa familia hiyo,ambaye hakuwepo kwenye tukio anafanya kazi Zain Customer care operation na anaitwa Aneth. Pole sana Aneth Mungu akupe nguvu ya kuweza kukabiliana na msiba huu mzito.
 
Hii ni habari mbaya kuisikia. Nyumba zetu nyingi zimejengwa bila kukidhi mahitaji ya emergency na hivyo vitu kama moto vikitokea kusalimika kwake ni kitu kigumu sana. Kuna changamoto ya kutosha sasa kuangalia mifumo ya moto kwenye makazi na majengo tunayojenga. Hizi habari zinaleta simanzi kubwa kuzisikia.
 
Back
Top Bottom