Familia ya Mkapa kwenye kashfa nyingine

Wazanzibari? Mwinyi alitufanyaje alipokuwa Ikulu?

Mwinyi tatizo lake ilikuwa hana la kusema mbele ya mkewe mama Sitti, ambaye inaonyesha alikuwa si tu anatumia nafasi yake ya kuwa Ikulu vibaya, bali pia alihusudu sana Wahindi na Waarabu.
 
Hivi hatuna jeshi, litusaidie kwenye hiki kipengele kwa mwaka mmoja, Mh, lakini hata jeshi lenyewe, "mpe mchawi mwanao akulele"
Mkuu jeshi lenyewe lipo corrupted kwa hiyo itakuwa kazi bure tu kwa kufanya hivyo. Ndani ya jeshi kuna makada wengi sana wa CCM. Angalia ufisadi wa Abrahaman Nshimbo na wakuu wengi tu wa ngazi za juu katika jeshi ni mafisadi.

Pia hao wakuu wa majeshi yetu huwa wakimaliza utumishi wa umma basi wanakuwa makada wa ccm. Kuwapa jeshi ni sawa na kuwakabidhi ccm bila kujijua umefanya nini.
 
Inatia uchungu watanganyika wezi sana!
suluhisho ni kuwapa uongozi wazanzibar tu.
Mwizi mwenyewe! ila suluhisho sio kuwapa uongozi wa- ZNZ bali kufikiria kuweka madarakani chama makini chenye dira na uelekeo unahitajika na kizazi cha sasa na kijacho (sio kizazi kilichopita), na kisha kumsimamisha mtu anayeweza kutekeleza dira na ilani ya chama hicho makini, wewe unakijua chama hicho na unaweza kujaza hapa..................
 
nashindwa kujua nini maana ya mjadara ni wengi tunakoswa point kama hauna si unasoma na unaacha kuchangia au usipochangia utaonekana hajapitia? haya yote sio ya usiku waliotajwa si wapo kama wanaona wanaonewa si waende mahakamani tutatoa ushahidi na vielelezo si vipo? naomba tusipende kuleta ushabiki pengine hii isue ina inakukusa sana unayoenda kinyume na huyu mleta maada.
 
NAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA ANAJIBU MAOMBI. Ukweli utabaki kuwa kweli daima. Analaumiwa sana Rais wa awamu ya nne kuwa amesababisha maisha ya wataz kuwa magumu lkn wanashau/ hawajui chanzo ni nini? Ikafikia Mkapa anajivuna MTANIKUMBUKA kumbe aliwapumbaza wananchi kipindi alichotawala kwa udiktekta wake na ujanja wa ukweli na uwazi kumbe anawaua taratibu.

Leo Taifa linalalamikia lilipoangukia lakini limesahau lilipojikwaa. Lakini kinachotakiwa watanzania tubadilike kimawazo na tuondokewe hofu na kuacha kutukana ovyo na kuongea ovyo tuweni watendaji kwa pamoja. Pia tatizo kubwa tunalo tuwabinafsi kupita maelezo kiasi kinatufanya kuwa zaidi ya wachawi. Kuchukiana na wivu usiyo na sababu TUPAMBANENI KWA UHALISIA!
 
Kazi ninayo tena kubwa tu. Mimi siendi kwenye internet cafe kubrowse bali ofisini kwangu kila nipatapo fursa namwaga vitu. Isitoshe kwa mtafiti kama mimi hii ni sehemu ya kazi yangu. Kwa hiyo adobe usiwe na shaka juu ya mke na watoto wangu watakula nini. Ukitaka kujua mie ni nani tembelea blog yangu utajua vizuri. Siandikii shida wala kukosa kazi.

Mie nadhani uliweka thread hii kutujulisha kuhusu kitu kipya. Suala unalolizungumzia lilishasemwa mwaka ule wa kwanza baada ya Mkapa kuondoka madarakani. Waliosema walisema kabla ya huo ukaguzi wa CAG. Waliosema walikuwa wanajua wakatuambia. Huenda hatukuamini. Jitahidi kuzungumzia vitu vipya bwana mtafiti. Umeanza kwa kusema kashfa nyingine, mbona sioni kipya hapa?
 
Kazi ninayo tena kubwa tu. Mimi siendi kwenye internet cafe kubrowse bali ofisini kwangu kila nipatapo fursa namwaga vitu. Isitoshe kwa mtafiti kama mimi hii ni sehemu ya kazi yangu. Kwa hiyo adobe usiwe na shaka juu ya mke na watoto wangu watakula nini. Ukitaka kujua mie ni nani tembelea blog yangu utajua vizuri. Siandikii shida wala kukosa kazi.

Sitegemea mtu aingie Internet Cafe kujadili mada za JF, sana sana huko muda kidogo anaopata baada ya kusoma na kutuma mails ni facebook. Hapa wengi wenye mijadala mirefu si wa kiwango cha kwenda cafe, bali makazini na majumbani. Online ni gharama na akisiye na nafasi vigumu kuipangia bajeti.
 
Back
Top Bottom