Familia ya Lowassa yapelelezwa London kwa Utakatishaji fedha

Habari njema hii kwa wapenda mageuzi na wazalendo wa nchi hii.
haya, endeleeni na vita yenu nyie panzi sie kunguru tuko tunasubiria taratibu....
 
Mkuu pasco.
Nimekutafuta sana toka jana kwenye thread hapa jf za maandamano na kupigwa makanjanja wenzako sijakuona ila imekuja thread ya laigwana umekimbilia fasta je kashfa ya lowasa na kupigwa waandishi wenzako ipi inakuadhiri zaidi?? Nilitegemea ungekuwa bega kwa bega na waandishi wenzako ila kimya hata comment hutupii kwenye thread zote ila hii ya mzee wa bahasha tena kubwa ya a4 umechepuka fasta.

Waandishi mnamuona mwenzenu pasco kawatosa huko yuko kwenye thread ya lowasa??

By the way nini msimamo wako kuhusu makanjanja wenzako na kipigo cha polisi?

Otherwise good morning
Mkuu Jiulize Kwanza, kwanza asante kwa kuniulizia, kuliko ungeendelea kujiuliza!. Kiukweli mimi likitokea tukio la kuniudhi au kunitibua, huwa sichangii!. Kwa kuanzia kanisome mchango wangu hapa!, https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nahabari-tef-chatoa-tamko-3.html#post10645322

Uandishi ni fani yangu, sisi sisi waandishi kuusema ukweli sometimes tunaudhi!, mimi kama mwandishi nimepigia kelele sana hii kitu inaitwa "Police Brutalities!" kanisome hapa [h=3]Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!,[/h]jinsi ninavyoumizwa na vitendo vya ukatili wa polisi, tena sisi waandishi ndio tukitumika kama vuvuzela wakati polisi wakifanya ukatili huo, lakini inapofikia ni zamu yetu ndio tunapiga kelele!. Kwangu mimi, kila binadamu anastahili utu na heshima!, human dignity has no class eti huyu ni mhalifu, na huyu ni mwandishi!, in a line of fire no one is spaired!.

Alipouliwa Mwangosi, kiukweli kabisa machozi yalinitoka!, nilipandisha uzi huu, [h=3]IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality!.[/h]kisha nikauliza [h=3]Emmanuel Nchimbi na IGP Saidi Mwema mnasubiri nini [/h]mpaka leo hivyo vyama vya waandishi vimefanya nini?, ukiondoa juhudi binafsi za Mjengwa?!.

Waandishi wakaamua eti wasusie habari za kipolisi!, kiukweli niliwakana!.

Mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea, naandika just for the love of it na sio kama ajira!, waaandishi tumekuwa tukijikomba komba sana kwa jeshi la polisi kumbe kwao sisi ni kama pe..au con.. wanatutumia tuu wakati wakituhitaji wao, tukiwaibukia wasipotuhitaji, sehemu stahiki kwetu ni kwenye dust bin au kwenye dampo!.

Sisi Tanzania tunafuata sheria za common, "not guilt until proven guilt beyond reasonable doubt!" ukiangalia media za wenzetu, huwezi kumuona mtuhumiwa amepigwa picha mahakamani, au mikononi mwa polisi!, hapa kila siku kamera zinapiga picha watuhumiwa mahakamani, au polisi kuwaparade watuhumiwa mbele ya waandishi na sisi tunachukua picha na kuzianika kwenye media!, picha za watuhumiwa sio tuu ni kinyume cha maadili ya uandishi bali ni kinyume cha sheria!, sisi ndio tunashirikiana na jeshi la polisi kuwavunjia watuhumiwa haki hiyo ya msingi, kila siku tunawapo polisi promo jinsi wanavyosambaratisha maandamano, leo tumegeuziwa kibao!, ndio tuna lalama!. OMG!.

Thanks.

Pasco
 
Ccm imara lazima ichuje makada wake kwenye vikao.tuwajue undani wao

kwa hawa wanaotajwa tajwa hakuna mtu msafi hata mmoja wasafi CCM wapo ila hawatajwi unaweza kumsikia anatajwa mara 1 kwa miezi sita hawana nafasi wana mikono mitupu
 
Hizi ripoti za uwongo na za kiji..nga Mods muwe nazo makini, zinaharibu reputation za Forum....juzi nilimnukuu moja wa wamiliki wa hili forum kuwa issues ya Lowassa kwa sasa ndio iko hot humu ndani so likija issue yoyote ya lowassa hata ripoti zinazoitaji uchunguzi wanazirusu ilimradi wapate ela...kwa mfano hili jambo ni uwongo ulio kubuhu kabisa
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Mheshimiwa Edward Lowassa muda huu amehojiwa na makachero wa TAKUKURU wakiongozana na makachero kutoka Uingereza wa kikosi cha Serious Fraud Office (SFO) kuhusiana na vyanzo vya fedha za ununuzi wa nyumba mbili anazomiliki Mheshimiwa Lowassa huko Uingereza.

Itakumbukwa kwamba mwezi Novemba 2010, Rais Kikwete aliwekwa chini ya shinikizo kubwa kumrudisha Mhe Lowassa kwenye Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, taarifa za umiliki wa nyumba hizi ambazo inasemekana zimenunuliwa kwa fedha chafu zilimfanya Rais Kikwete kuachana na fikra hizo.

Itakumbukwa kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika habari hii mwezi Novemba 2010 na kutoa picha ya nyumba hizo kwenye ukurasa wa mbele.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa Mahusiano ya Umma wa SFO, Mr. Stewart Johnston, amekiri kuwepo kwa uchunguzi huo kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania lakini akasema kwamba hawana utaratibu wa kutolea maelezo uchunguzi unaoendelea.

Kwa mujibu wa taratibu za Uingereza, mmiliki wa nyumba anapaswa kuelezea chanzo cha mapato ya ununuzi wa nyumba pamoja na kodi ya nyumba inayolipwa kila mwaka.

Inaaminika kwamba nyumba hizo zina thamani ya pauni milioni mbili na nusu au sawa na shilingi zaidi ya bilioni tano. Wadadisi wa mambo wanaamini kwamba chanzo cha fedha hizo ni malipo ya mkataba haramu wa ufisadi wa Richmond.

Haijaweza kueleweka kwanini Mhe Lowassa ameamua kununua nyumba mbili Uingereza. Watu wa karibu wa Mhe Lowassa wanaamini kwamba ni maandalizi ya kuondoka nchini pale lengo lake la kutaka Urais litakapokwama.

"Unajua Mzee kuna kipindi alikuwa amechoka kabisa na siasa za majitaka hapa nchini na alishaamua kuchukua familia yake na wajukuu na kujiondokea akaishi kwa amani na kula utajiri wake huko Uingereza", alikaririwa mmoja wa wapambe wake ambaye alikuwa ni Mbunge katika Bunge lililopita kutoka Kanda ya Ziwa.

Ukichanganya na suala la afya yake inayozorota, historia ya kukataliwa na Mwalimu Nyerere, ufisadi wa Richmond, na maelewano madogo na viongozi wakuu wa Chama, uchunguzi huu mpya ni pigo la ziada kwa Mhe Lowassa katika harakati zake za kutafuta Urais wa Tanzania kwa mwaka 2015.

ivi vyombo vya kimataifa kuna wakati napata tabu kuvielewa namna vinavyofanya kaz,i hii habari tangu 2010 ilikuwa inaelea kwanini waje sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi na kwanini EL tu na si wengine wakati viongozi wetu wameficha pesa nyingi nje na zinawafaidisha wao pesa za viongozi wa africa zote zimefichwa uko majuu kama ni uchunguzi ufanywe lakini usiishie kwa EL pekee wachunguzwe wote.
 
Richmond sio lowassa amekula hio hela. Hizo hela ndizo zilizomweka kikwete madarakan

Lowassa kawa chambo tu. Labda mlete tuhuma nyingine lakni sio ya richmond.
Richmond= kikwete

Umenena vyema mkuu ngoja muda ufike kila kitu kitawekwa wazi...hawa watoto wa joka la mdimu wamechanganyikiwa kabisa...jamaa yao hauziki hata kidogo watanzania wanakuambia bora tumpe Dovutwa kuliko huyu joka la mdimu
 
Waziri Mkuu
aliyejiuzulu Mheshimiwa Edward Lowassa muda huu amehojiwa na makachero
wa TAKUKURU wakiongozana na makachero kutoka Uingereza wa kikosi cha
Serious Fraud Office (SFO) kuhusiana na vyanzo vya fedha za ununuzi wa
nyumba mbili anazomiliki Mheshimiwa Lowassa huko Uingereza.

Itakumbukwa kwamba mwezi Novemba 2010, Rais Kikwete aliwekwa chini ya
shinikizo kubwa kumrudisha Mhe Lowassa kwenye Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, taarifa za umiliki wa nyumba hizi ambazo inasemekana
zimenunuliwa kwa fedha chafu zilimfanya Rais Kikwete kuachana na fikra
hizo.

Itakumbukwa kwamba gazeti la Raia Mwema liliandika habari hii mwezi
Novemba 2010 na kutoa picha ya nyumba hizo kwenye ukurasa wa mbele.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa Mahusiano ya Umma wa SFO, Mr.
Stewart Johnston, amekiri kuwepo kwa uchunguzi huo kwa kushirikiana na
taasisi za Tanzania lakini akasema kwamba hawana utaratibu wa kutolea
maelezo uchunguzi unaoendelea.

Kwa mujibu wa taratibu za Uingereza, mmiliki wa nyumba anapaswa kuelezea
chanzo cha mapato ya ununuzi wa nyumba pamoja na kodi ya nyumba
inayolipwa kila mwaka.

Inaaminika kwamba nyumba hizo zina thamani ya pauni milioni mbili na
nusu au sawa na shilingi zaidi ya bilioni tano. Wadadisi wa mambo
wanaamini kwamba chanzo cha fedha hizo ni malipo ya mkataba haramu wa
ufisadi wa Richmond.

Haijaweza kueleweka kwanini Mhe Lowassa ameamua kununua nyumba mbili
Uingereza. Watu wa karibu wa Mhe Lowassa wanaamini kwamba ni maandalizi
ya kuondoka nchini pale lengo lake la kutaka Urais litakapokwama.

"Unajua Mzee kuna kipindi alikuwa amechoka kabisa na siasa za majitaka
hapa nchini na alishaamua kuchukua familia yake na wajukuu na
kujiondokea akaishi kwa amani na kula utajiri wake huko Uingereza",
alikaririwa mmoja wa wapambe wake ambaye alikuwa ni Mbunge katika Bunge
lililopita kutoka Kanda ya Ziwa.

Ukichanganya na suala la afya yake inayozorota, historia ya kukataliwa
na Mwalimu Nyerere, ufisadi wa Richmond, na maelewano madogo na viongozi
wakuu wa Chama, uchunguzi huu mpya ni pigo la ziada kwa Mhe Lowassa
katika harakati zake za kutafuta Urais wa Tanzania kwa mwaka
2015.

chanzo cha taarifa? au kuchafuliana tu.
 
Mkuu nimefarijika sana kwa kunijibu maana nilikuwa najiuliza tuu...Niko very satisfied na comment yako hususani hiyo fupi niliyo ku quote nimefurahi kusikia kutoka kwa mwandishi kama wewe kuwa mmezidi kutumika ni matarajio yangu kuwa utawashawishi kama sio kuwaelimisha waandishi wengine ambao bado hawajagundua waendako au ambao hawajitambui wajitambue sasa. Pls be their ambassador watakutesa kwa njaa zao lakini watakukubali yakiwafika kama ya juzi.

Otherwise "I liked your comment"


kila siku tunawapo polisi promo jinsi wanavyosambaratisha maandamano, leo tumegeuziwa kibao!, ndio tuna lalama!. OMG!.

Thanks.

Pasco
 
Lowasa ni mtenda kazi mzuri asiye mwaminifu,hafai kupewa nchi hii labda akaombe kazi kule alikoficha mali zetu.
 
Uwe unatumia akili badala ya kukurupuka na kuandika pumba. Unadhani huyo kijana angeweza kuwapa maelezo yanayojitosheleza hao makachero toka UK wangeona umuhimu wowote wa kufunga safari mpaka Tanzania kuja kumuhoji fisadi Lowassa.

Mafisadi ndani ya Serikali ya mafisadi wanaficha mali zao chungu nzima walizozipata kwa njia haramu kwa kutumia majina ya watoto wao. Kuna mtoto wa miaka minane aliyegunduliwa eti ana nyumba yenye thamani ya bilioni moja!! Hii wanalifanya ili wanapopeleka information kuhusu utajiri wao kule kwenye Tume ya Maadili ya Mafisadi waonyeshe ni watu wa kawaida kabisa wasio na utajiri wowote kumbe mali zao zote zimeandikwa chini ya majina ya watoto wao na ndugu zao wa karibu.

Haya wewe mpiga debe maarufu wa fisadi Lowassa inaelekea unayajua mengi kuhusu utajiri wa familia yote ya fisadi Lowassa tuwekee hapa jamvini vyanzo vya mapato vya huyo mtoto wa fisadi Lowassa.

Hizo nyumba za kule sio sehemu ya utajiri wake, ni nyumba za kijana wake, zilizonunuliwa kwa fedha kutokana na biashara halali za kundi la makampuni ya Alfa!.

Amesema wazi yeye anamiliki ng'ombe 800!.

Tenganisha mali za kampuni ya Alfa na mali zake binafsi!. Hata mimi, ninamiliki kijikampuni kinaitwa PPR, mimi mwenyewe naishi pale Kwa Mtogole kwenye nyumba ya kupangisha nimechukua upande nzima, nalipa laki kila mwezi!, na usafiri ninaomiliki binafsi ni boda boda moja na iko juu ya mawe tangu ile ajali!. Lakini PPR imepanga jengo zima la NHC pale mtaa wa Mkwepu, inalipa kodi ya TZS. 3,000,000 kwa mwezi, inamiliki magari, inamiliki vifaa vya digital production, na imeajiri watu zaidi ya 10!.

Nikulizwa mimi nina nini, nasema ukweli, sina kitu!, kwa sababu vile vitu ni vya PPR!. Vivyo hivyo Mzee wetu anamiliki ng'ombe 800 tuu!, vingine vyote ni vya Alfa!.

Pasco
 
Uwe unatumia akili badala ya kukurupuka na kuandika pumba. Unadhani huyo kijana angeweza kuwapa maelezo yanayojitosheleza hao makachero toka UK wangeona umuhimu wowote wa kufunga safari mpaka Tanzania kuja kumuhoji fisadi Lowassa.

Mafisadi ndani ya Serikali ya mafisadi wanaficha mali zao chungu nzima walizozipata kwa njia haramu kwa kutumia majina ya watoto wao. Kuna mtoto wa miaka minane aliyegunduliwa eti ana nyumba yenye thamani ya bilioni moja!! Hii wanalifanya ili wanapopeleka information kuhusu utajiri wao kule kwenye Tume ya Maadili ya Mafisadi waonyeshe ni watu wa kawaida kabisa wasio na utajiri wowote kumbe mali zao zote zimeandikwa chini ya majina ya watoto wao na ndugu zao wa karibu.

Haya wewe mpiga debe maarufu wa fisadi Lowassa inaelekea unayajua mengi kuhusu utajiri wa familia yote ya fisadi Lowassa tuwekee hapa jamvini vyanzo vya mapato vya huyo mtoto wa fisadi Lowassa.

Mkuu BAK Nimependa tafakuri zako makini
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi Nyerere ndo nani mpaka kila neno lake liwe sheria?

He was just a failure.
 
Back
Top Bottom