Falsfa ya kujivua gamba imeishia wapi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Hivi ule mpango wa kujivua gamba ulikuwa ni mchezo wa kuigiza?

Alafu kituko ni kwamba, naona wale watuhumiwa wa kujivua gamba baada ya kuchafuliwa na falsfa hii wamelipwa fadhila kwa kupewa uenyeviti wa kamati za bunge ili kukinisuru chama.

Wadau hili wazo mnalionaje?
 
Kukujibu swali lako kwa ufasaha kama ulivyouliza kuwa imeishia wapi. Jibu ni imeishia kulekule ilikoanzia na kumalizwa na walewale walioianzisha. Hakuna la zaidi.

Wait for new single which is on pipe line. Na kwa kadri siku zinavyosonga mbele ndoo wanavyozidi kupiga hesabu za jinsi gani wamrudishe Rostam kundini. Just wait
 
ha haa haaaa

Rostam Aziz alisema hizi ni gutter politics .... nape hajawahi kujibu hili hata siku moja

kweli nimeamini alichosema Rosti-tamu nikweli
 
They were propagating themselves, The bad thing is those propagaters were not doing propagations from there heart but for money now the propaganda is ova.

Zilikua ni propaganda za mpito. Gudbye CCM
 
UNAOTA MKUU!
CHADEMA+CHATO+5.jpg


CHADEMA+CHATO+7.jpg


JIMBO LA CCM CHATO. Kwa magufuli.
 
Lowasa alisema kama wanamuona yeye ni gamba basi na boss wake JK ni gamba pia maana issue za dowans zilipata baraka zake yeye rais so ka ni kuvuliwa uanachama basi wavuliwe wote akiwemo na yeye JK ndo mana wote wapo havuliwi mtu gamba hapo
 
Kwanini CCM imshindwa kufanikisha programme yake ya kujivua gamba mara baada ya kuianzisha,programme iliyoaminiwa na wananchi pamoja na wanachama watiifu kuwa ingeleta heshima ndani ya chama na kutoa dhana kuwa CCM kichaka cha wahuni.Kushindwa kwa falsafa hii ya kujivua gamba kumedhihirisha udhaifu na ombwe la uongozi ndani ya nchi na CCM kwa ujumla.

Ikiwa M/KITI ana kiri kuwa rushwa imekigubika chama chake haitoshi kuishia kutoa kauli,nilitegemea angefanya maamuzi magumu na kufuta uchaguzi na kuivunja taasisi ya kuzuia rushwa kwa kushindwa kuwajibika.Haitaji elimu ya chuo kikuu kubaini rushwa ambayo imetolewa hadharani na kila mtu ana jua kilichofanyika.

Udhaifu wa M/kiti ambaye ndiye Amiri jeshi mkuu wa majeshi yetu kwa kushindwa kufanya maamuzi magumu ndiko kunakopelekea maadili ya uongozi wa umma kushuka na nidhamu ya uwajibikaji kupotea.Serikali itajivunia nini kuhusu kupinga rushwa ilihali viongozi wa chama kinachotawala wana patikana kwa misingi ya rushwa.

Kwa mantiki hii basi hakuna haja ya kuwa na TAKUKURU ikiwa imeonyesha udhaifu wa makusudi kwa kushindwa kuwajibika kama sheria na kanuni ilivyo waongoza.Aibu hii kwa serikali haitoshi kuitwa udhaifu bali ikibidi uwajibikaji wa pamoja wa kisiasa na kiutendaji ufanyike mara moja,hapo ndipo tutakapoamini serikali ya CCM inachukia rushwa kwa vitendo.Kuendele kugharamia uendeshaji wa TAKUKURU ni uhuni na uhujumu uchumi ambao unafanyika kwa misingi ya kuilinda taasisi hiyo kisheria.

Nachukua fursa hii kukaribisha michango mbali mbali tujadili ni kwa nini falsafa hii ya kujivua gamba imeshindwa na kuwafumba midomo wapiga debe wake na kuwaacha mayatima kwa KITENDO CHA M/KITI kuwageuka na kuiona falsafa hiyo kama adui wa kukiua chama,ilihali maamuzi hayo yaliafikiwa kwenye vikao halali vya CCM.NDUGU WAKUU WA BODI YETU NAWASILISHA KWA HESHIMA NA UTIIFU MADA HII ILI KUINUSURU NCHI YETU KUTOKANA NA JANGA HILI LA KITAIFA LA RUSHWA KUITAFUNA NCHI NA WASHEREHESHAJI WAKE KUACHIWA HIVI HIVI WAKIENDELEA KUMWAGILIA MAJI RUSHWA IZIDI KUSHIKA MIZIZI YAKE VIZURI
 
Kwasababu mpaka mwenyekiti wa chama nae ni gamba,nape nae ni gamba so wameona waipotezee ina kiua na kugawa chama cha magamba
 
Kwasababu mpaka mwenyekiti wa chama nae ni gamba,nape nae ni gamba so wameona waipotezee ina kiua na kugawa chama cha magamba

Nimekupata,kumbe basi kushamirisha rushwa nadni ya chama ndiyo falsafa na stratergy nzuri ya kukiimarisha chama hiki?lakini mpaka lini ikiwa waathirika wakubwa ni wananchi ambao hawapewi haki yao ya kikatiba wanapo hangaika kupata huduma za kijamii kama huduma za afya,elimu nk huku wakiminywa mpaka tone la mwisho kuchangia kodi ya mapato ambayo wanasema kodi ya mapato kwa maendeleo ya taifa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom