Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,408
- 31,392
Kenya wamefanya hivyo, je kuna afadhali? Asilimia 10 ya Wakenya wanamiliki 90% ya ardhi. Mahindi na chakula kinaingia Kenya kupitia Namanga, Horohoro, Taveta n.k. Afadhali ipo wapi?Babu kawalostisha. Wakati wenzetu walifanya juhudi za kumilikisha watu ardhi, Tanzania ilifanya ardhi mali ya serikali.
Nenda sehemu inayoitwa Kisii hadi Kerako uangalie umasikini wa hali na ardhi.
Uganda ardhi ilikuwa ya Kabaka Mutesa, kuna tofauti gani ya masikini wa Arua na yule wa Mtwara?
Nenda Rwanda uone hali ilivyo. Hivi unafikiri agenda ya ardhi kwanini inaleta mzozo ndani ya EAC?
Mkulima anapolima mahindi na kukosa soko, au mkulima anapolima nyanya na kuuza tenga sh 1500, tatizo unadhani ni nini?
Njaa yetu si kwasababu ya matumizi ya ardhi, ni ukosefu wa mipango ya kuwmendeleza mkulima, ukusanyaji wa chakula na hifadhi ya chakula. Huwezi kuacha mahindi yauzwe Malawi Zambia, Kenya, Uganda na Rwanda halafu udhani kuwa ukitoa ardhi hovyo utakuwa umepata suluhu ya njaa.
Kwanini Wasonjo na Wamasai wanagombana hadi FFU ingilie kati! sasa ukiacha asilimia 5 imiliki unadahni kitatokea nini.
Angalia vision ya Nyerere in wide spectrum, sio mashamba tu.