falsafa ya rais kikwete kukemea rushwa na kuacha kukemea ufisadi.

Ndulungu

Member
Oct 22, 2011
87
49
najiuliza hivi ni kwa nini?rais kikwete sijamsikia hata siku moja akikemea na kuonesha kukerwa na ufisadi.nasikitika sana mheshiwa rais anaposhindwa kupampana na masula ya rushwa na ufisadi.

rushwa na ufisadi imeonekana kukithiri ndani ya chama anachokiongoza licha ya yeye kuonekana anawafahamu watoaji na wapokeaji rushwa ndani ya ccm lakini ajifanya hawafahamu kabisa na kuwasukumia eti wanachama wa ccm na wananchi wawataje na suala la ufisadi hataki kulizungumzia kabisa.

katika suala zima la ufisadi wananchi wamekuwa wakihoji juu ya utajiri mkubwa wa mwanawe ridhiwani na tumekuwa hatupati majibu yeyote kwa mh.rais wala kwa yeye ridhiwani ambapo kwa kaisi kikubwa utajiri alionao ridhiwani haulingani na kipato chake hapa wananchi tueleweje

pamoja na mawaziri na mkatibu wakuu kadhaa kujiuzulu na wengine kusimamishwa kazi kwa tuhuma za kuthibitika za ufisadi lakini hakuna hatua zozote za kisheria zilizo chukuliwa juu yao hapa pia tueleweje?
mh.rais tumekuchagua utuongoze na tumekupa dhamana ya kulinda rasilimali ya nchi yetu inakuaje watu waibe wathibitike wamefanya hivyo kisha ushauriwe uwafuze kazi nawe ujibu ni upepo wa kisiasa tu utapita na hapa je tueleweje?

mwl nyerere aliwahi kusema watanzania hatuendelei kwa sababu tunatoa majibu mepesi katika masuala mazito
ni hato tu naomba tujadili kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom