Falsafa ya CHADEMA nguvu ya "umma" na wabunge wao 23

Huyu ndio mpiga ramli wa ccm, halafu unasema haupo kwenye maombolezo? chunga kijana angalia usije ukaondolewa kwenye payroll ukakimbia mji kijana. hata kama unalipwa per post ukiwa JF, si vibaya posho za leo ukazisamehe ili ungaane na wenzako ambao wana msiba mzito wa huyu mchawi Sheikh ubwabwa.
Hahahahaha naona unaangaika kila thread wewe na huyu mchawi au ulikuwa mteja wake nini, jibu hoja kama una endelea kuombeleza sisi tupu huku tunajadili Wabunge 23 wa Chadema kama unaweza :welcome:
 
Ndugu Ridhiwani Kikwete,

Mbona umechelewa hivi?? Haya yooote ungetuambia tangu mwaka juzi kabla baba yako hajaporomosha zaidi uchumi wetu kwa kukutumia wewe kama CAHIER wa fedha zooote za ufisadi. Hivi sasa Tanzania kumekucha kiasi kwamba sijui haya unayoyazungunmza kama kweli kuna yeyote atakayekusikiliza.

Isitoshe, idadi ya wabunge wa CHADEMA kuwa ni 23 wala isikupe taabu maana kila kiti cha ubunge kitakachoanguka wazi tangu sasa ujue ni mali ya CHADEMA. Vile vile, baada ya uchaguzi wa 2015 sina uhakika ka CCM kitaweza kweli kufikisha idadi kama hiyo ya wabunge hapa nchini.

Mwisho, hata mti wa mbuyu unaoufahamu kokote kule nao ULIANZA KUOTA KAMA MCHICHA TU hivyo usije ukadhani vyama vilivyoridhiwa na CCM vilianzishwa vikiwa vikubwa na yenye raha, ubabe na ufisadi kila kona;

wapo watu walifanya saaaaaaaaaaaaana kazi kama ambavyo tunavyofanya hivi sasa ndipo na wewe ukajirithishia NG'OMBE WA WA MAZIWA unaoukamwa kila siku biola huruma.
Hahahahah jamani kumbe SHEIKH YAHAYA, A.KA UWEZO TUNAO, mzima anaendelea na kazi zake za Utabiri
 
Hahahahaha naona unaangaika kila thread wewe na huyu mchawi au ulikuwa mteja wake nini, jibu hoja kama una endelea kuombeleza sisi tupu huku tunajadili Wabunge 23 wa Chadema kama unaweza :welcome:

Angalia taarifa ya habari ya ITV muda huu uone ccm wenzako wa Arusha wanavyoumbuana, kwamba ni njaa ndio zinawasumbuwa ndio maana mnakubali kutumiwa kama condom ukimaliza kazi yako unaitupa. aibu kweli kweli, kama usipoangalia muda huu jitahidi uangalia ya saa nne usiku. yaani mnatia aibu kwa jamii.
 
Yaani hata mngefanya nini inakula kwenu mtasena weeeeeeeeeeee sijui chadema wana wabunge 23 lakini haita saidia hata kidogo sasa mamkubwa muyatarajie 2015 kama tukiwepo kama sio itakuwa upside down.ccm sasa hali mbayaaaaa ni kama mfa maji kutapatapa kwake kawaida sna ccma wana haha yaani mh huwa najisikia kucheka wanavo jitahidi kujifariji lakini ndi mjue kimoja kimoja huzaa vingi, halafu pili nayashangaa majinga yanayo taka kufananisha eti chadema na magamba hawana hata akili unatakiwa kujua mwanzo wa kupungua ni kuelekea kwisha eti ohhh chadema wabunge 23 lakini mjue ndo wanazidi kuongezeka ivi mtakali hayo hayo badae mtakua ccm mmebakiwa ka wabunge watatu.ccm kushnehi
 
Unajua ukiona mtu anashangilia hali ngumu ya maisha ya mtanzania lazima ujue kuwa huyo ni mmoja wao..

Rits huyu ni mmoja wa mafisadi na anashabikia ufisadi.. Ccm kuwa na wabunge wengi siyo tija wala halina msingi wowote. Wewe angalia kwa miaka zaidi ya 40 wamefanya nini... Achana na mambo ya chadema hayakuhusu.. Ila utakuja juta siku moja ccm ikipigwa mweleka.. 2015..
 
Watanzania wenzangu tunapoteza pesa nyingi kutokana na hawa Wabunge viti maalumu Katiba mpya tupambane tutoe huu upuuzi wa Wabunge viti maalum, Chadema sijui watatoa wapi pesa za Maandamano na nchi yetu ni kubwa sana mpaka uimalize kwa Maandamano na Uchaguzi Mkuu utakuwa umefika, na ndio mwisho wa Chadema, badala wafanye mambo ya msingi wao Maandamano tu kila kikicha nchi aijengwi na Maandamano

CCM imetawala kwa miaka 50 lakini hakuna maendeleo ya maana zaidi ya maisha kuwa magumu kila kukicha, imekuwa inavuta ruzuku ya mamia ya mamilioni kila mwezi lakini hakuna cha maana zaidi ya kuiba zingine BOT. Hata CHADEMA hawajamaliza mwaka mmeanza kulalamika? Heli CHADEMA inayotumia pesa hizo kuwahamasisha wananchi wajue haki zao kuliko za CCM hata hatujui zinafanya kazi gani!

CHADEMA-Aluta continua, hakuna kulala mpaka kieleweke. Mkama na Nape mikutano yao ina watu kiduchu utafikiri wako kwenye hitma ya mchawi wao! Yaani mpaka aibu!

Avatar yako Riz1 inafanana na hisia zako-ni masikitiko tu-hali mbaya!
 
umelipwa bei gani toka magamba?je wewe upo camp gani ktk micamp yenu ya huko magambani?duuu kumbe roho inakuuma kuona ule umati wa nguvu ya umma eeeh?masikini weeee umeshachelewa,sasa hivi kibarua chako kItaota manyoya kwani umma ushachoshwa na magamba...

Alaa, kumbe huwa mnakodiwa ku-sponsor thread humu JF. Haya tuambie na wewe mshiko wako kiasi gani? Ndiyo maana kuna thread za kikanjanja humu, kwa sababu ya mishiko? Umetufumbua macho.
 
Wingi sio hoja; unaweza kuwa na kikundi kidogo lakini chenye kuongoza. CDM leo ni wachache lakini ndio chama kiongozi hapa nchini. CCM kimebebaki kuwa chama tawala. CDM wanaongoza 'public opinion' ya waTZ, na wanaongoza mijadala mikubwa ya kitaifa!
 
WANANCHI wanatakiwa kutobabaishwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Chadema kutokana na chama hicho kutokuwa na nguvu ya UMMA, na badala wajikite zaidi katika kuijenga nchi kwa mshikamano bilia kubagua itikadi za vyama.
Chadema wanatakiwa kushukuru angalau kwa kuambulia majimbo 23 kati ya majimbo 239, sasa wewe umepata majimbo 23 eti unataka upewe nchi aiwezekani kabisa, Watanzania hawa Wabunge wa viti Maalumu wa kupewa 25 ndio wanaleta matatizo yote haya ya Maandamano, Chadema kila mwezi wanapata 300 Milioni, kutokana na hawa Wabunge 25 wa kupewa ni mtaji wa Mandamano ndio maana Wabunge wenye majimbo ni vigumu sana kuona kwenye Maandamano yasio na tija yoyote kwa taifa.
Watanzania wenzangu tunapoteza pesa nyingi kutokana na hawa Wabunge viti maalumu Katiba mpya tupambane tutoe huu upuuzi wa Wabunge viti maalum, Chadema sijui watatoa wapi pesa za Maandamano na nchi yetu ni kubwa sana mpaka uimalize kwa Maandamano na Uchaguzi Mkuu utakuwa umefika, na ndio mwisho wa Chadema, badala wafanye mambo ya msingi wao Maandamano tu kila kikicha nchi aijengwi na Maandamano

Formula ya ruzuku is based kwenye total votes za presidential candidate na sio idadi ya wabunge. Similarly, number ya wabunge wa viti maalum inapatikana based on the presidential votes. Kwa hiyo hata kama kusingekuwa na wabunge maalaum CDM wangepata exactly what they are getting at the moment.
 
Hahahahaha naona unaangaika kila thread wewe na huyu mchawi au ulikuwa mteja wake nini, jibu hoja kama una endelea kuombeleza sisi tupu huku tunajadili Wabunge 23 wa Chadema kama unaweza :welcome:

Okay, CCM ina Wabunge karibu 300, ina maRaisi wawili, ina Makamu wa Raisi, ina Waziri Mkuu, ina waziri Kiongozi , ina Spika wa Bunge, ina Mawaziri wote, ina Wakuu wote wa Mikoa, ina Wakuu wote wa Wilaya, inawateua Wakuu wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, inawateua Wakuu wote wa Mashirika ya Umma, inamteua Jaji Mkuu, inateua majaji wote, ina Mahakama zote, ina magereza yote, inamiliki karibu Viwanja vyote vya Umma vya Michezo, inatoza na kukusanya kodi, inamiliki hata katiba ya sasa, ina.........................

Cha ajabu Chadema ina Wabunge 23 tu, haina Raisi hata moja, haina makamu wa Raisi, haina Waizri Kiongozi, haina Spika, haina Waizri hata moja, haina Mkuu wa Mkoa, haina Mkuu wa Wilaya, haina Mkuu kwenye chombo chochote cha Usalama, haiteui Wakuu wa Mashirika, haimteui Jaji Mkuu, haimteui Jaji hata moja, haiendeshi Mahakama, haiendeshi Magereza, haimiliki hata kiwanja kimoja cha Umma cha Michezo, haitozi wala kukusanya kodi, inakandamizwa na katiba, haina...........................................

Sasa Mkuu ritz, kwa nini unawaomba wananchi Wananchi kutobabaishwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Chadema kutokana na chama hicho kutokuwa na nguvu ya UMMA ? Hofu yako kwa Chadema inatokana na nini ? Kwa nini Wananchi wakishabikie Chadema, chama kisichokuwa na chochote cha kuwapa, chama ambacho hakiko madarakani na hivyo kukosa meno ? Woga na hofu yako ritz inatokana na nini huku wewe ndiye umekamata mpini, je unaogopa kuumbuliwa kuwa uko uchi ? (na uko uchi kikwelikweli !)
 
Formula ya ruzuku is based kwenye total votes za presidential candidate na sio idadi ya wabunge. Similarly, number ya wabunge wa viti maalum inapatikana based on the presidential votes. Kwa hiyo hata kama kusingekuwa na wabunge maalaum CDM wangepata exactly what they are getting at the moment.

Mkuu ngoja nikukumbushe jinsi Chama chako kinavyopata Ruzuku, kwa mujibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwe, Chadema inapata Ruzuku kwa mwezi milioni 203.6 kutokana na kupata asilimia 24 ya kura za Urais (Sawa na Sh. milioni 146) na asilimia 9.62 ya Wabunge (Sawa na Sh. milioni 56)
 
Hahaaaa!! umenifuraisha sana, kwani awo wabunge wa CCM walioshinda kwa uwalali ni wangapi? je uwezowao mjengoni si unauona mwenyewe? kwa taharifa yako Mbunge Mmoja(1) wa CDM ni sawa na wabunge kumi(10) wa CCM izo ni statistic za mjengoni kulingana na mchango wao ktk bunge na jinsi ya kusimamia hoja zao.
Mkuu inabidi ufikiri kwanza kabla ya kuleta mada apa janvini some times mada nyingine zina kera. Nathani umenipata.
 
Na CCM inapata ruzuku kiasi gani?
 
Mkuu Chadema ina Wabunge halali 23, wengine wamepewa na CCM

Na bado wanasema wameshinda wamesusia hotuba ya Rais? ama kweli tuna makalulu wengi Tanzania yetu hii. Wananchekesha, heheeee, ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.
 
Na bado wanasema wameshinda wamesusia hotuba ya Rais? ama kweli tuna makalulu wengi Tanzania yetu hii. Wananchekesha, heheeee, ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.

Hii ni misemo ya kina dada wakiwa wanasukana salon, au mtoto wa kiume ambae si riziki, anaependa afanane jinsia na dada zake.
 
Hahaaaa!! umenifuraisha sana, kwani awo wabunge wa CCM walioshinda kwa uwalali ni wangapi? je uwezowao mjengoni si unauona mwenyewe? kwa taharifa yako Mbunge Mmoja(1) wa CDM ni sawa na wabunge kumi(10) wa CCM izo ni statistic za mjengoni kulingana na mchango wao ktk bunge na jinsi ya kusimamia hoja zao.
Mkuu inabidi ufikiri kwanza kabla ya kuleta mada apa janvini some times mada nyingine zina kera. Nathani umenipata.

Unanchekesha, wizi huwajuwi weye, weye weye! haa, mtu yu aiba mpaka mke wa watu, halafu wajifanya hujui wizi wako wapi? haa, mtu ayauzia chama chake (eti kwa kuwa mwenyekiti) mafuso matatu kwa zaidi millioni mia nne (400,000,000). Halafu wasema wizi huwajui? unanchekesha mwaya. Ama kweli, ukipenda chongo utaliona kengeza! heeeeeeeeeeeeee!
 
Aveta hiyo ni ushuhuda kwamba CCM imevuliwa nguo hadharani na Chama Cha Chadema:A S-confused1:
 
Na bado wanasema wameshinda wamesusia hotuba ya Rais? ama kweli tuna makalulu wengi Tanzania yetu hii. Wananchekesha, heheeee, ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.

Hii misemo imekaa kishoga shoga na kipwani pwani vile!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom