FaizaFoxy, Mwita25, MalariaSugu, Freedom Is coming... I am out of CCM

Ni jambo jema kubadilisha mwelekeo baada ya kutafakari kwa kina. Hii nchi inahitaji mabadiliko makubwa ya kimwelekeo na kiutawala.
 
Hiyo ndio CCM tunaojivunia Tanzania, unakwenda unakopenda, ndio demokrasia, hata Mbowe babake na Mkwewe si walikuwa Serikalini?

Ngoja tumtafute waziri mchaga ni yupi kwa sasa tutamjuwa baba'ko.
Hili ndilo tatizo kubwa la hawa vibaraka wa CCM kama Faizafoxy, Malariasugu na wenzao. Wanakimbilia kwenye ukabila mara tu wanapobanwa kwenye hoja nzito.
Thread hii ya Uhuru1 ni ya kusisimua na ni changamoto kwa wanaCCM endapo kweli wangekuwa wanasimamia maslahi ya nchi na si matumbo yao. Kujibu hoja hii kihunihuni kama anavyofanya huyu faizafoxy ni uthibitisho wa CCM kuishiwa kabisa hoja na kubakia na moja tu ya ukabila na wakati mwingine udini.
Mimi si mchaga lakini siuoni hapo uhusiano wa uchaga na hii hoja wala uchaga na CHADEMA. Ama kweli aliyewaroga CCM....! Yaani kwao kuwa mchaga ni dhambi isiyosameheka inayomvua mtu haki zote kuanzia ya kutoa maoni hadi kuongoza! Sijui hawa CCM wanataka kutupeleka wapi sasa. Wamesahau nasaha za Hayati Baba wa Taifa wanayedai wanamuenzi alipowaambia bayana kwamba moja ya dalili za kukitambua chama au kiongozi aliyefilisika kisera ni kukimbilia kwenye udini na ukabila.
Kwa Great Thinkers wa kweli kiongozi bora ni anayekidhi sifa na vigezo vya nafasi husika bila kujali kabila au imani yake kwani hatuchagui mtu wa kutuswalisha bali kutuongoza. Haijalishi kuwa ni mkutu, mluguru, mngoreme, msukuma, msagara, mnyamwezi, mnyiramba, mvidunda au kabila lolote hata kama litavumbuliwa mwaka kesho kutwa. Kwa hili la ukabila na udini unaopaliliwa na Mwenyekiti wenu, Historia itawahukumu na kuwaadhibu CCM na nyinyi vibaraka wake.
 
Hoja yako imesimama. Mtu anahitaji akili ya mwendawazimu kukanusha hali ya kukatisha tamaa uliyoielezea. CCM inaweza kuzinduka usingizini kwa kufanya maamuzi magumu ili kionekane kinajali maslahi ya wanyonge. Wasingekuwa wanakwenda mbele na kurudi nyuma katika mkakati waliousanifu wenyewe wa magamba huenda matumain ya wengi yangekuwa yamerejea, Ni hatari kuwa na chama kinachoongoza serikali kikiwa kimepoteza dira na welekeo kama hali inavyoashiria kwa sasa. Wazalendo wa kweli wa nchi hii ama wakisaidie chama cha mapinduzi kurejesha matumaini ya wananchi ama waviimarishe vyama vyenye upinzani wa kweli na makini ili kuinusuru nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Dalili zinaonesha kuwa wazazi wako hawakujali. Sijui kwanini. Ww kama umeamua kwenda Arusha kutafuta posho, nenda zako salama. Usilazimishe watu wafatishe mawazo yako.
 
sidhani kama ni uamuzi mzuri kuondoka CCM.kwa mtazamo wangu nadhani mapambano mazuri ya kuwaondoa viongozi wasiofaa yataanzia ndani ya chama chenyewe hasa ktk mchakato wa kura za maoni.Ilipofikia CCM sasa hivi si rahisi kuachia madaraka kwa upinzani kwani wanajua kuwa viongozi wengi wataishia jela.

Nashauri vijana wengi wajiunge CCM mapema ili kuleta mabadiliko ndani ya chama sivyo utawala wa kurithishana ndani ya ccm utaendelea milele.

Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake! Sidhani kama change zaweza toka ndani ya CCM. Maana wote mmo ndani ya square no one is thinking out of it!!!
 
Back
Top Bottom