Fainali za Bongo Star Search (Season 8, 2015)

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,666
22,674
12074485_1539501336340352_2956528410347238960_n.jpg

Ikiwa leo ni fainali ya mashindano haya. Washiriki wapo 6, anahitajika mshindi mmoja atakayeibuka na kitita cha shilingi milioni 50 Usiku huu.

==============

Mchuano umeanza, ushindani mkali sana .

Wapo washiriki sita, wanahitajika watano waweze kuingia top 5.

Kila mshiriki ataimba wimbo mmoja ili mchujo upite wabakie watano.
=================

- Waimbaji wote sita mpaka sasa wameshaimba nyimbo mojamoja. Majaji wanachuja majina sita yapatikane matano.
- Kampuni ya Huawei kupitia wawakilishi wake wanagawa zawadi ya simu kwa washiriki wote sita.

TOP 5:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia 5 bora;

1.Kayumba Juma
2.Angel Marry Kato
3.Nasib Fenabo
4.Frida Amani
5.Kevin Gerson

- Mshiriki aliyeshindwa kufuzu ni Jackline, anatoka katika mashindano.

==================

MC wa BSS, Ceasar Daniel azua gumzo!
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mtangazaji muongozaji wa Bongo Star Search Caesar Daniel amekuja na Msemo wa #HapaKaziTu.

Hali imebadilika ghafla ukumbi ukalipuka mabadiliko, huku wahdhuriaji wakionesha vidole viwili kuashiria alama ya chama cha siasa na wengine wakizungusha mikono kuonesha Mabadilikoooooo..

Kazi kweli kweli!
===========

TOP 3:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia kwenye 3 bora;

1. Nasib Fenabo
2. Frida Amani
3. Kayumba Juma

- Walioshindwa kuingia kwenye awamu hii ni Kevin Gerson na Angel Marry Kato.
===============

TOP 2:
- Waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye 2 bora ni;

1. Kayumba Juma
2. Nasib Fenabo..

- Burudani zinaendelea kabla ya kuingia kwenye awamu ya mwisho kumpata Bongo Super Star - 2015

- Jukwaani anapanda Christian Bella na Malaika Band.

- Si mchezo! Show anayoifanya Bella inamfanya kutuzwa pesa nyingi mno.. Amekonga nyoyo za waliohudhuria hapa!
===========

- Na sasa ni wakati wa msanii Runtown kutoka Nigeria kutumbuiza. Anapanda na dancers wake jukwaani.

RunT.jpg

Kumbuka: Huyu ndiye msanii wa mwisho 'kupafomu' kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mwisho kumpata mshindi wa BSS 2015.
===========================

Naam, na sasa ule muda uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu umewadia!

- Chief Judge, Madam Rittah amepanda jukwaani kuungana na washereheshaji Caesar Daniel na Penny kumtangaza Mshindi. Je, ni Kayumba au Fonabo?

Madam Rittah
: Kwa kweli najisikia faraja sana kufikia hatua hii. Napenda kutoa shukrani kwa tulioshirikiana kulifanikisha hili (anataja timu ya BSS, Majaji wenza, Wadhamini na wadau mbalimbali).

- Na Mshindi wa BSS 2015 (Season 8) ni.....

Kayumba winner.jpg

MWISHO!
 
RED CARPET APPEARANCES

attachment.php

Wasanii wa Bongofleva, Navy Kenzo nao wamo!

attachment.php

Ndege Mnana, Linnah Sanga..

Runtow.jpg
Msanii wa Kimataifa Runtown kutoka NIgeria (Muimbaji wa Gallardo) atakuwepo kutoa burudani.

Chege slm.jpg
Chegge Chigunda akiwa na Salaam (Meneja wa msanii Diamond Platnumz)

ChegeMwanaFa.jpg
Mwana FA na Chegge

attachment.php

Romy Jones akiwahoji kwenye Red Carpet washiriki wa BSS waliotoka.
 

Attachments

  • 12141810_1539650586325427_1869456140707988339_n.jpg
    12141810_1539650586325427_1869456140707988339_n.jpg
    68.3 KB · Views: 15,605
  • 10410316_1539467453010407_6241827310964038123_n.jpg
    10410316_1539467453010407_6241827310964038123_n.jpg
    17.5 KB · Views: 1,663
  • 12112131_1539651236325362_6593315989798043567_n.jpg
    12112131_1539651236325362_6593315989798043567_n.jpg
    13.4 KB · Views: 19,914
  • 10472690_1539646766325809_7490716966372322730_n.jpg
    10472690_1539646766325809_7490716966372322730_n.jpg
    9.7 KB · Views: 14,274
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi mtangazaji muongozaji wa Bongo Star Search Siza Daniel amekuja na Msemo wa #HapaKaziTu.

Hali imebadilika ghafla ukumbi ukalipuka mabadiliko, huku waudhuriaji wakionesha vidole viwili kuashilia alama ya chama cha siasa na wengine wakizungusha mikono kuonesha Mabadilikoooooo..

Kazi kweli kweli!
 
Sizya alijisahau akasema eti hapa kazi tu wacha akumbane na nguvu ya umma mle ndani, watu wakazungusha vidole wakimaanisha sijui nn vile
 
dah

kayumba anaimba hit song

ila fonabo anaimba mziki,na anaandika nyimbo zake

kayumba akishnda atapotea

fonabo either ashnde au asishnde
ANA HAZINA KUBWA INAHTAJI MSIMAMIZI TU tangu arusha nimeona hli

all the best fonabo
 
Nimeshangazwa Na Mc Wa BSS 2015 Bw.Sizya kuleta Ushabiki Wa Siasa wakati shughuli nzima ya kufanikisha shindano hilo limejumuisha watu tofauti tofauti Na wenye itikadi tofauti.Tunashauri BSS acheni kuingiza siasa.Sio kila kituko ni siasa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom