Faida ya tunda la Apple

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
"Apple" kwa kiswahili nafikiri linaitwa tunda damu, Tunda hili liko la aina tofauti yako ya kijani yako mekundu na haya mekundu ndio yaliyo mazuri zaidi na pia yanasemakana matunda mazuri zaidi ni yale ya Europe au yale ya Kashmir.

Tunda origin yake ni sehemu za Mashariki mwa Europe na pia Magharibi mwa Asia, na tunda hili linajulikana kwa miaka ya zamani mno katika miji ya Old China, Babulon na Egypt. Tunda hili limetajwa hata katika Quraan na Kitabu cha Nabii Issa A.s

Minerals na viwango vilivyomo katika tunda hilo:
Moisture 84.6% - Calcium 10mg
Protein 0.2% - Phosphorous 14mg
Fat 0.5% - Iron 1mg
Minerals 0/3% - Vitamins A 40 IU
Fibre 1.0% - kiwango kidogo cha Vitamin E,H na B complex
Carbohydrates 13.4%


Tunda hili hutimiwa na lina faida kubwa katika mwili wa mwanaadamu. Lina dawa ya maradhi tofauti:

Anaemia: Apple lina wingi wa iron, arsenic na phosphorus, kwa mtu mwenywe ugonjwa huu inafaa kufanya juice ya apple iwe fresh. Ni vizuri kunywa juice hiyo glass moja kabla kula chakula (nusu saa kabla) na pia kabla ya kwenda kulala usiku.

Kuharisha na kutapika: Mwenye kutokezewa na ugonjwa huu ni vizuri sana kutumia tunda hili (iwe bivu). Kila siku ale 2 pia kama yatapikwa au kuchomwa ni mazuri zaidi kwani hulainisha cellulose.

Dysentery: Kwa watoto aghlabu maradhi haya huwakumba watoto, ni vizuri mtoto akitokezewa na ugonjwa huu kumpa kila wakati kipande cha apple kwani huzuia hali ya ugonjwa huo.

Matatizo ya tumbo: Kuna matatizo tofauti ya tumbo, kwahivo tunda hili limekusanya matatizo yote ya tumbo na kuondoa matatizo hayo. Changanya apple, asali kidogo na ufura kidogo na kula kabla chakula hii husaidia kuondoa matatizo ya tumbo kama vile usagaji mdogo wa chakula na mengine.

Kuumwa na kichwa: Tunda hili lina faida katika maradhi yote ya kichwa. Apple lilowiva limenye maganda yake, halafu ule kwa kutia chumvi kidogo kila siku asubugi kabla ya kula kitu chochote, na uendelee kufanya hivi kwa muda wa wiki 2.

Matatizo ya moyo:Apple ya wingi wa potassium na phosphorus lakini sodium inapatikana kidogo sana.Kwa wakai wa zamani watu walikuwa wakila matunda haya na asali, kwa ajili ya maradhi ya moyo na research imefanyika imeonekana kwa wale watu wanotumia vyakula venye potassium kwa wingi huepukana na maradhi ya moyo. Kwahili ni uzuri kula tunda hili pamoja na asali.

High Blood Pressure:Apple linasaidia katika kuongeza kutoa (secreation) mkojo ambayo hii inasaidia kurudisha blood pressure katika hali ya kawaida, pia inasaidia kupungua kwa sodium chloride katika figo.

Kifua kikavu na kidney stones: 250 grams apple ule kwa muda wa week nzima.

Meno:Matunda haya yanasaidia sana meno katika kuyasafisha na kuyaepusha na vijidudu na kuoza, kila baada chakula kula apple moja.

Source:MziziMkavu

'' An Apple a day keeps a doctor away..!!''
 
Urembo:Ganda la ‘Apple’ kujenga misuli, ngozi


APPLE’ ni tunda linalopendwa na watu wengi na mbali na kutumiwa kama chakula, lina uwezo mkubwa katika kuboresha urembo wako.


Utafiti wa masuala ya urembo unaonyesha kuwa tunda hili husaidia kujenga misuli ya mwili na kulainisha ngozi yako.

Katika uchunguzi wa Dk Christopher Adams anasema ganda la tunda hilo ambalo watu wengi huliondoa mara wanapokula, lina faida nyingi likiliwa. Baadhi ya faida alizozitaja ni pamoja na kujenga misuli imara, kuimarisha ngozi na kuifanya nyororo pamoja na kupunguza uzito.

Pia ganda la Apple linasaidia kushusha kiwango cha sukari katika damu kwa wale wenye tatizo la kisukari, pamoja na kuondosha magonjwa yote yanayosababishwa na kujaa kwa mafuta mwilini.

Matatizo ya kujaa mafuta kwenye Ini na sumu mbalimbali katika kiungo hicho cha mwili vinaweza kuondolewa na kemikali zinazopatikana kwenye ganda la apple ikiwa tunda hilo litaliwa mara kwa mara.


Tunda la apple pia linatumika na watu wengi wanaohitaji kufanya mlo maalum kwa ajili ya kupunguza uzito. Lakini inashauriwa kabla ya kula tunda hilo hakikisha umeliosha vema na kulila pamoja na ganda lake ili kupata matokeo mazuri.

Apple limetajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kurekebisha mfumo wa homoni.
 
Na hilo neno Tufaa ni neno la kiarabu sio la Kiswahili.

تفاحة





Ni neno la Kiswahili kwa sababu utalikuta kwenye kamusi la Kiswahili

Si ajabu kuwa asili yake ni Kiarabu Kama maneno mengi mno ya Kiswahili.

Shukrani, Kalamu, daftari, mistari, lakini, ghira, samaki, samawi, kitabu, bahari na mengineyo

Note by: Apple si neno la Kiswahili lakini Tufaa ni neno la Kiswahili ambalo asili yake ni neno la Kiarabu
 
Na hilo neno Tufaa ni neno la kiarabu sio la Kiswahili.

تفاحة

Shukrani kwa kutuelimisha zaidi ya kutuhabarisha. Sahihisho dogo ni kwamba apple si tunda damu kwani tangu utotoni naanza pata akili wazazi wangu walikuwa na bustani ya matunda mbalimbali yakiwemo miti mitatu ya apple ambayo tulizoea kuita kwa jina kama hilo, na tulikuwa na miti kadhaa ya matunda damu. Ukitaka kupata picha nzuri nenda kule milima ya Uluguru kunakotoka matunda mengi, Lushoto, na kusini nyanda za juu utayakuta matunda yote hayo apples na matunda damu yanastawishwa.

Endelea kutujuza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom