Faida ya matumizi ya tende katika kuongeza kinga ya mwili

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
1
FAIDA YA MATUMIZI YA TENDE KATIKA KUONGEZA KINGA YA MWILI NA TENDE ni chakula chenye hali ya juu ya sukari na huliwa zikiwa mbichi au mbivu. Katika kila gramu 100 (100gm) ndani yake mna lishe kwa asilimia ifuatayo:-
Moisture (Unyevunyevu)
15.3 %
Protein (hamirojo)
2.5%
Fat (mafuta)
0.4%
Carbohydrate (wanga)
75.8%
Fibre (kambakamba)
4%
Mineral matter (madini)
2.1 %


Baada ya funga ya muda mrefu kuanzia alfajiri hadi jioni (magharibi) ni bora kufungua saumu yako kwa kuanza kula tende kwa sababu ni chakula chepesi na husagwa tumboni kwa urahisi. Baada ya kusagika huleta nguvu mwilini haraka na pia hulipa tumbo nguvu ya kusaga

vyakula vitakavyofuatia baadae. Tende hutofautiana katika ubora kutokana na kutegemea zinatoka nchi gani. Pia hutegemea ikiwa tende hizo ni mpya kutoka shambani au ni za mavuno ya zamani. Tende bora zaidi huwa na faida

nyingi za kitiba lakini bei yake ni ghali na tende ya hali ya chini na ya zamani kuvunwa bei yake ni rahisi ukilinganisha na tende mpya lakini faida yake kimatibabu ni ndogo zaidi. Mimi kama Daktari nashauri watumiaji wa tende watumie

tende yenye kiwango cha juu ili wapate faida ya kitiba. Pia ni changamoto kwa wafanyabiashara wa tende watuletee na kutuuzia tende zenye ubora zaidi. Aidha wanunuzi nao wanunue tende zenye ubora wasijali ughali wa bei bali wajali

ubora. Kauli yangu ni kwamba "Tende rahisi faida ndogo kitiba" na "Tende ghali faida kubwa kitiba".
Lengo hapa ni kuelimisha jamii wala sio kuharibu biashara ya mtu. Nawahimiza tutumie tende katika miezi yote na wala si mwezi wa

Ramadhani tu; na wale wasiokuwa Waislamu nawafahamisha kuwa tende si chakula cha Waislamu pekee bali ni cha watu wote. FAIDA ZA TENDE KITIBA 1) Kifua, Mafua, Pumu: Saga kiasi cha tende kwenye blenda pamoja na asali na

samli safi ya ng'ombe kisha changanya ndani yake kijiko kimoja cha chakula cha unga wa habbat sauda na tangawizi.

Matumizi: Kula vijiko viwili vikubwa asubuhi na jioni. 2) Kutopata choo:- Tengeneza juisi ya tende na maji au maziwa, kunywa glasi moja asubuhi na jioni. 3) Kuipa mishipa ya fahamu nguvu na kuimarisha kumbukumbu:- Kula tende mara kwa mara huongeza kumbukumbu na fahamu. 4) Ni dawa ya kurejesha heshima nyumbani (Mujarrab):- Hutia kisu makali. Chukua tende robo kilo uondoe mbegu zake na

saga ndani ya brenda pamoja na maziwa ya ng'ombe ongeza ndani yake kijiko kimoja cha unga wa uwatu na hulinjan ya unga.

Matumizi: Kunywa glasi moja asubuhi na jioni kila siku. 5) Mwanamke anaenyonyesha:- Kunywa kila siku asubuhi na jioni mchanganyiko wa Tende, maziwa na uwatu. 6) Ukavu au kukauka kwa mdomo na koo:- Kunywa juisi ya mchanganyiko wa tende na maji asubuhi na jioni, hulainisha mdomo na koo. 7) Sperms Additive:- Huu ni mchanganyiko

maalum wa madawa ya Kiarabu yaliyochanganywa na tende na maziwa ya moto ili kuongeza au kuzidisha sperms (yaani manii) kwa wale ambao wanahisi kuwa sperms (manii) ni chache au kuna udhaifu. Ikiwa hupati mtoto nenda ukapime hospitalini sperms zako, kipimo hiki kinaitwa Sperms Counts au Sperms Analysis. Ikiwa ni chache au dhaifu itabidi

uongeze kwa kutumia dawa hii ya Sperms Additive. Dawa hii inapatikana katika ofisi zetu kwa kufanya oda maalum (special order). Angalia anuwani zetu nyuma ya kijitabu hiki. Na kwa mwanamke ambae hapati ujauzito alete vipimo vyake vya hospitali na tutampa ushauri au dawa. Inshallah.

HITIMISHO Baada ya kuona au kuelimika kuhusu faida za tende, nawashauri watu wote tuendelee kutumia tende hata baada ya mwezi wa Ramadhani sababu ndani yake mna lishe na faida kubwa za kitiba.
 
Wale akina mama waja wazito. Kuzuia upungufu wa damu. Kula tende tumba 3 pamoja na kila mlo. Kwenye 2.1% ambayo ni minerals kiasi kikubwa ni Iron na Zinc.

KEEP IT UP MM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom