Zifahamu faida ya kutumia tangawizi katika mwili wa binadamu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Tangawizi ina faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo :
ginger.jpg

1. Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni,.
2. Kutibu tatizo la gesi tumboni
3. Kuondoa tatizo la msokoto wa tumbo (bila kuharisha)
4. Husaidia kuzuia kutapika.
5. Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),
6. Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.

Jam ya tangawizi
Unaweza kutumia Jam ya Tangawizi kujitibu magonjwa mbalimbali kama ilivyo onyeshwa hapo juu.

Jinsi ya kutengeneza Jam ya tangawizi
Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.

Muongozo wa kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia tangawizi
Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao la Tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo :

Kujitibu tatizo la kuvimbiwa na kukosa hamu ya kula
Changanya Juice ya Tangawizi, Juice ya Limau na Chumvi ya mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.

Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.

Kujitibu tatizo la maumivu ya koo na kukauka sauti
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.

Kujitibu tatizo la kuharisha
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.

Kichefuchefu na kuharisha
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.

Maumivu ya kichwa na wasiwasi
Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.

Maumivu makali ya tumbo
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.

Baridi yabisi sugu
Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.

Maumivu ya jino na kichwa
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.

==========

1581662876209.png

Tangawizi ni zao ambalo hustawi sehemu mbalimbali duniani na hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, dawa kwa tiba ya magonjwa ya binadamu na wanyama na pia kiambato muhimu kwenye vinywaji mbalimbali.

Zao hili lilianza kulimwa katika nchi za Asia, Afrika Magharibi na katika visiwa vya Caribbean. Tangawizi ni zao linalotumiwa na walaji wote ulimwenguni, hii inatokana na baadhi ya watu kutambua faida zake ki-lishe na kitiba.

Faida za tangawizi
  • Katika lishe
    Tangawizi ikichemshwa na maji na kuongezwa sukari hutoa kinywaji ambacho ni kitamu na chenye ladha nzuri sana. Baadhi ya watumiaji hupendelea kuongeza asali, vipande vya machungwa au limao ili kuweza kupata ladha nzuri zaidi. Vilevile hutumika katika utayarishwaji wa vinywaji vingine viwandani kama soda, chai, kahawa nakadhalika.
  • Hutumika kama kiungo muhimu cha kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali kama biskuti, mikate, keki, nyama na vingine vingi.

CHAI YA TANGAWIZI

Kitiba
  • Utomvu unaotokana na zao hili umeonekana kusaidia sana katika kuondosha maumivu ya sehemu mbalimbali za viungo vya binaadamu. Unapochua utomvu huu mara mbili kwa siku sehemu zenye maumivu huweza kuondosha maumivu mbalimbali haraka, kwa mfano maumivu ya misuli, magoti, maumivu ya kichwa nakadhalika.
  • Hukinga na kutibu kuwashwa na kukereketwa koo (Sore throat) na ugonjwa wa mafua ya sehemu ya juu (Upper respiratory truck infection).
  • Tafiti mbalimbali ulimwenguni zimethibitisha tangawizi kuwa na uwezo mkubwa katika kuondosha homa za kutapika na kizunguzungu (motion fever) kwa wasafiri wa vyombo mbalimbali baharini na nchi kavu.
  • Pia huondosha kichefuchefu na kutapika kwa akinamama wajawazito na hata kwa wagonjwa wanaofanyiwa operesheni. Inasadikika kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa kinatosha kumuondolea kichefuchefu na kutapika mgonjwa baada ya kufanyika operesheni.

SUPU YA TANGAWIZI

  • Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu jambo ambalo linazaweza kusababisha maradhi ya moyo na kupooza kwa viungo vya mwili.
  • Tangawizi pia imegundulika kuwa dawa muhimu kupunguza au kuondosha kabisa maumivu wanawapata kinamama wengi wakati wa hedhi.
  • Vilevile tangawizi imedhihirisha kuwa na uwezo mkubwa kuponya haraka maumivu makali ya tumbo yanayowapata mara kwa mara watoto wadogo.
  • Katika baadhi ya nchi tangawizi inatumika katika kuhifadhi chakula kwa muda mrefu, hii inatokana na ukweli kwamba ina uwezo mkubwa wa kuua aina nyingi za bakteria kama vile E.coli, Salmonella na wengine wengi ambao huharibu vyakula vyetu.
  • Tangawizi hukiamasisha kimengenyo mwilini kilichopo mwetu kiitwacho Gastric juice kufanya kazi ipasavyo na hivyo husaidia kuzalisha joto la mwili ambalo huwapa nafuu wagonjwa wengi wa mafua na maumivu ya tumbo.
  • Watu wengi ulimwenguni hutumia mmea huu kama dawa ya kuondoa harufu mbaya kinywani.
  • Hutumika katika utengenezaji wa siki (vinegar) ambayo huhamasisha hamu ya kula
  • Nchini China wanawake wengi wajawazito hutumia juisi ya tangawizi ili kujiepusha na adha ya kutapika mara kwa mara (Morning sickness).
  • Tangawizi pia hutumika kama dawa ya kushusha joto la mwili na homa za mara kwa mara zinazosababishwa na malaria au mashambulizi ya bakteria na fangasi ambayo mara nyingi huchochea joto la mwili kupanda zaidi ya kiwango cha kawaida.
  • Pia husaidia kushusha presha ya damu mwilini (hypertension) kwa watu wanaosumbuliwa na presha ya kupanda.
  • Tangawizi pia hutumika kupunguza maumivu yanayosababishwa na matatizo ya mawe kwenye figo, vilevile hupunguza maumivu ya kibofu cha mkojo iwapo itatumika kuchuliwa kwa nje sehemu za mwili zilizo karibu na kiungo hiki.
  • Virutubisho vilivyomo kwenye zao hili pia huhamasisha utendaji mzima wa vimengenyo mbalimbali katika usagaji wa chakula mwilini
    na pia kutuongezea hamu ya kula chakula.
Lakini itabidi izingatiwe kwamba isitumiwe kwa watoto chini ya miaka 2, itumiwe kwa watoto zaidi ya umri huo kuwaondolea adha kama vile za kuumwa vichwa, kichefuchefu na kuumwa matumbo.

Dozi ya tangawizi itolewe kulingana na uzito wa mtoto husika. Dozi nyingi za dawa za mitishamba hutolewa kwa kulinganishwa na dozi ya mtu mzima wa kilo 70, hivyo mtoto wa kilo 20 hadi 25 hupatiwa 1/3 ya dozi ya mtu mzima. Kwa ujumla kwa dozi ya mtu mzima huwa isizidi gramu 4 kila siku.

Ni vyema tukajenga mazoea ya kutumia dawa zitokanazo na mimea kama tangawizi kwa ajili ya kinga na tiba mbalimbali za miili yetu kwa sababu licha ya kuwa zinapatikana kirahisi pia si ghali na hazina madhara yeyote kwa afya zetu kama zilivyo dawa nyingi za viwandani.

==
Michango iliyotolewa na wadau

View attachment 342835

Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi.

Mmea huu unafanana sana na binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa ya kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.

Tangawizi inatumikaje?
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutegenezwa unga.

Je, faida ya tangawiz ni nini?
Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu. Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.

Pia kiungo hiki kina faida zaidi kwa wagonjwa hasa walioathirika na ugonjwa wa ukimwi. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya maajabu ya mmea huu wa tangawizi.

Jinsi ya kuitumia kama dawa:
Tangawizi ikiwa imesagwa au mbichi iliyopondwa inaweza kutumika kama kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mbadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffenia ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini. Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na miboga mingine, inaweza kuongezwa katia freshi pia na kuleta ladha nzuri ambayo ni dawa pia.

Je, tangawizi hutibu magonjwa gani?
Tangawizi husaidia yafuatayo: Kuongeza hamu ya kula, Kupunguza kichefuchefu, Kutapika, kuharisha Kisukari, Shinikizo la damu, Kuongeza msukumo wa damu, Kutoa sumu mwilini, Maumivu ya tumbo na gesi tumboni, unyeyushwaji tumboni, mafua na magonjwa mengine mengi.
----
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi

4. Huondoa uvimbe mwilini

5. Huondoa msongamano mapafuni

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake

7. Huondoa maumivu ya koo

8. Huua virusi wa homa

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi

19. Huongeza msukumo wa damu

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha kolesto

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa

25. Hutibu shinikizo la juu la damu

26. Husafisha utumbo mpana

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

34. Husaidia kuzuia kuharisha

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto

37. Hutibu homa ya kichwa

38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

41. Huimarisha afya ya figo

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi

43. Ina madini ya potassium ya kutosha

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
----
Faida 48 za Juisi ya Tangawizi ambazo ulikuwa huzijuwi bado.

Huwa inanishangaza sana ninapoutafakari ukuu wa Mungu kwa namna ambayo ametupa mimea mbalimbali mhimu kwa ajili ya afya zetu – Mwanzo 1:29. Maelezo yafuatayo kuhusu tangawizi yatakupa wewe ujuzi wa mmea mwingine wa asili usio na madhara ya kikemikali na kusaidia mwili wako kuwa na afya nzuri na ya kupendeza.

Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa mhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kudili na aina mbalimbali za kansa mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.

Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza radha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadharika. Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.

Tangawizi ni zao la kibiashara na ni rahisi kutoka kimaisha kama utaamua kulima tangawizi ingawa ni zao la miezi mingi lakini ukivumilia utakula bata tu, gunia moja linauzwa kati ya laki 3 hadi 6 wakati wa msimu mzuri.

Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.Leo nimekuletea hii juisi ya tangawizi, nimetumia tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Kazi 48 za tangawizi mwilini;

Huondoa sumu mwilini haraka sana.

Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngoziKuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi.

Huondoa uvimbe mwilini.

Huondoa msongamano mapafuni.

Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake.

Huondoa maumivu ya koo

Huua virusi wa homa.

Huondoa maumivu mbalimbali mwilini.

Huondoa homa hata homa ya baridi (chills).

Hutibu saratani ya tezi dume.

Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia) ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini,

Pia hutibu kiungulia, na kansa mbalimbali za tumbo.

Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi.

Hutibu kanza za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi.

Huongeza msukumo wa damu husaidia kuzuia shambulio la moyo.

Huzuia damu kuganda.

Hushusha kolesto.

Husafisha damu.

Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa.

Hutibu shinikizo la juu la damu husafisha utumbo mpana.

Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma.

Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI.

Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Dawa nzuri ya kuondoa uchovu.

Husaidia kuzuia kutapika.

Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa.

Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

Husaidia kuzuia kuharisha husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu.

Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto.

Hutibu homa ya kichwa.

Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.

Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito.

Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

Huimarisha afya ya figo.

Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi na madini ya potassium ya kutosha.

Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha.

Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium.

Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki, magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene.

Hulinda kuta za moyo.

Hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita.

Chanzo: MUUNGWANA BLOG
---
TANGAWIZI ni zao ambalo humea katika sehemu mbalimbali duniani na hutumika kama kiungo katika vyakula, kama dawa kwa tiba ya magonjwa na pia kiambato muhimu kwenye vinywaji mbalimbali.

Kilimo cha tangawizi kilianzia katika nchi za Bara Asia, Afrika Magharibi na katika visiwa vya Caribbean. Ili uweze kuwa na afya bora, unashauriwa kunywa chai ya tangawizi kwa wingi ili uweze kujikinga na kutibu magonjwa mbalimbali.

Zifutazo ndizo faida za kunywa chai ya tangawizi:
Huondoa harufu mbaya ya kinywa
Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu saumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri unapopumua na kufanya maeneo ya kinywa chako kuwa safi.
- Tangawizi husaidia msukumo wa damu
- Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwilini kwa sababu huupa mwili joto ambalo mara nyingi mwili huhitaji wakati wa usukumwaji wa damu mwilini.
- Huondoa mwilini baadhi ya magonjwa au hali mbaya za kiafya
- Tangawizi hupunguza na kuondoa kabisa hali mbaya za kiafya kama kikohozi na mafua. Tangawizi pia husaidia kuondosha uchovu hasa asubuhi.
- Kwa akina mama wajawazito, tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka; na vilevile hutumika kama kichocheo cha utulivu.
- Tangawizi husaidia mfumo wa chakula
- Husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula. Hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu.
- Kurekebisha sukari ya mwili
- Tangawizi husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu. Wagonjwa wa Kisukari wanashauriwa kutumia Tangawizi kwa wingi.
- Tangawizi huongeza hamu ya kula (appetizer)
- Huongeza hamu ya kula chakula. Kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula, wanashauriwa kutumia tangawizi ili - - - -kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.
- Kuyeyusha mafuta mwilini
- Tangawizi husaidia kupunguza kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa; hasa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu.
- Husaidia kuondoa sumu mwilini
- Tangawizi husaidia kupunguza kichefuchefu na hali ya kuhisi kutapika. Pia huwasadia sana wale watu waliotumia sana dawa ama za tiba au za kulevya na kuwa na sumu nyingi mwilini.
- Tangawizi husaidia kutibu vidonda vya tumbo

Kwa asilimia kubwa tangawizi humsaidia mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu na hata kuponya vidonda hivyo kama vitakuwa kwenye hatua za mwanzomwanzo.View attachment 1481974View attachment 1481975
 
33.jpg

Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi.

Mmea huu unafanana sana na binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa ya kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.

Tangawizi inatumikaje?
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutegenezwa unga.

Je, faida ya tangawiz ni nini?
Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu. Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.

Pia kiungo hiki kina faida zaidi kwa wagonjwa hasa walioathirika na ugonjwa wa ukimwi. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya maajabu ya mmea huu wa tangawizi.

22.png

Jinsi ya kuitumia kama dawa:

Tangawizi ikiwa imesagwa au mbichi iliyopondwa inaweza kutumika kama kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mbadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffenia ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini. Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na miboga mingine, inaweza kuongezwa katia freshi pia na kuleta ladha nzuri ambayo ni dawa pia.

Je, tangawizi hutibu magonjwa gani?
Tangawizi husaidia yafuatayo: Kuongeza hamu ya kula, Kupunguza kichefuchefu, Kutapika, kuharisha Kisukari, Shinikizo la damu, Kuongeza msukumo wa damu, Kutoa sumu mwilini, Maumivu ya tumbo na gesi tumboni, unyeyushwaji tumboni, mafua na magonjwa mengine mengi.
 
1. Huondoa sumu mwilini haraka sana

2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi

3. Kuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi

4. Huondoa uvimbe mwilini

5. Huondoa msongamano mapafuni

6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake

7. Huondoa maumivu ya koo

8. Huua virusi wa homa

9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini

10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)

11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

12. Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)

15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kanza mbalimbali za tumbo

17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kanza za kwenye kizazi na kanza za kwenye mirija ya uzazi

19. Huongeza msukumo wa damu

20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo

21. Huzuia damu kuganda

22. Hushusha kolesto

23. Husafisha damu

24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa

25. Hutibu shinikizo la juu la damu

26. Husafisha utumbo mpana

27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma

28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI

29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu

31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa

33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

34. Husaidia kuzuia kuharisha

35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu

36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto

37. Hutibu homa ya kichwa

38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi

39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito

40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

41. Huimarisha afya ya figo

42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi

43. Ina madini ya potassium ya kutosha

44. Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha

46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium

47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene

48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
 
Faida 48 za Juisi ya Tangawizi ambazo ulikuwa huzijuwi bado.

Huwa inanishangaza sana ninapoutafakari ukuu wa Mungu kwa namna ambayo ametupa mimea mbalimbali mhimu kwa ajili ya afya zetu – Mwanzo 1:29. Maelezo yafuatayo kuhusu tangawizi yatakupa wewe ujuzi wa mmea mwingine wa asili usio na madhara ya kikemikali na kusaidia mwili wako kuwa na afya nzuri na ya kupendeza.

Tafiti mpya zinazidi kuonyesha namna mmea huu ulivyo wa mhimu kwa afya ya binadamu ikihusisha uwezo wake wa kudili na aina mbalimbali za kansa mwilini na tafiti nyingine zinaendelea kufanyika.

Tangawizi inaweza kuwekwa karibu kwenye kila chakula, iwe ni katika kuilainisha nyama nyekundu, kuongeza radha katika nyama au samaki, kama chai, kwenye juisi na kadharika. Binafsi napenda ikiwa kwenye juisi ya matunda ndiyo inakuwa tamu zaidi na inaenda kufanya kazi mwilini haraka zaidi.

Tangawizi ni zao la kibiashara na ni rahisi kutoka kimaisha kama utaamua kulima tangawizi ingawa ni zao la miezi mingi lakini ukivumilia utakula bata tu, gunia moja linauzwa kati ya laki 3 hadi 6 wakati wa msimu mzuri.

Tangawizi iliorodheshwa kwa mara ya kwanza na serikali ya Marekani kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.Tangawizi huongezwa pia katika vinywaji vingi vya viwandani zikiwemo soda ili kupata radha nzuri zaidi.Leo nimekuletea hii juisi ya tangawizi, nimetumia tangawizi mbichi za ukubwa wa kati nne, parachichi moja na asali mbichi vijiko vikubwa saba na na maji lita moja na nusu.

Kazi 48 za tangawizi mwilini;

Huondoa sumu mwilini haraka sana.

Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngoziKuna viua vijasumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi.

Huondoa uvimbe mwilini.

Huondoa msongamano mapafuni.

Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake.

Huondoa maumivu ya koo

Huua virusi wa homa.

Huondoa maumivu mbalimbali mwilini.

Huondoa homa hata homa ya baridi (chills).

Hutibu saratani ya tezi dume.

Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.

Tangawizi ina kiinilishe mhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”

Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-related cancer)

Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia) ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)

Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini,

Pia hutibu kiungulia, na kansa mbalimbali za tumbo.

Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi.

Hutibu kanza za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi.

Huongeza msukumo wa damu husaidia kuzuia shambulio la moyo.

Huzuia damu kuganda.

Hushusha kolesto.

Husafisha damu.

Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa.

Hutibu shinikizo la juu la damu husafisha utumbo mpana.

Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma.

Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI.

Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Dawa nzuri ya kuondoa uchovu.

Husaidia kuzuia kutapika.

Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu

Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa.

Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula

Husaidia kuzuia kuharisha husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu.

Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto.

Hutibu homa ya kichwa.

Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi.

Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito.

Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)

Huimarisha afya ya figo.

Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi na madini ya potassium ya kutosha.

Ina madini ya manganese ambayo ni mhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha.

Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium.

Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki, magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene.

Hulinda kuta za moyo.

Hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita.

Chanzo: MUUNGWANA BLOG
 
Wakuu habari,
Mafua ndiyo,hatuwezi kuyaweka miongoni mwa maradhi 'hatari' kwa binadamu kama kisukari na malaria, LAKINI ni miongoni mwa madhaifu yanayokera na kusumbua sana watu.

Jinsi unavyovuja kamasi mda wote,sauti kubadilika,kupiga chafya za ghafra,kutoa machozi,kupumulia mdomo usiku baada ya kubanwa pua! Hakika mafua si ya kubezwa!

TANGAWIZI
Ni miongoni mwa viungo,lakini ni kati ya tiba za nyumbani(home remedy) mhimu sana kwa madhaifu mengi ikiwemo MAFUA!

Mafua huletwa na virusi vinavyoingia njia ya utekamasi kichwani(sinuses) na kuleta mafua
Tangawizi inayo madini mhimu(Potassium na Manganese) kwa kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizi ya virusi na bacteria,pia tangawizi inayo curcumin inayopandisha viwango vya protein inayolinda kinga ya mwilini dhidi ya virusi na bacteria

1.Njia ya kwanza ya maandalizi;
Kwakuwa tangawizi ikichanganywa na maji/chai n.k hujitenga (low-bioavailability) basi ili itumike yote vizuri changanya na MAZIWA(ya ng'ombe,tui la nazi au maziwa ya soya) mhimu ni yale mafuta ktk maziwa ndiyo HUIFYONZA vizuri tangawizi!
UNGA WA MDALASINI, huu pia ni mhimu ktk kudhibiti vimelea kama virusi na bacteria mwilini
ASALI MBICHI,huongeza kinga ya mwili na kudhibiti vimelea.

Maandalizi
Chemsha maziwa/tui la nazi kikombe kimoja yaliyochanganywa na kijiko cha chai cha unga wa tangawizi.
Ukiipua changanya na kijiko kimoja kikubwa cha asali mbichi na nusu kijiko cha chai cha unga wa mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni mchanganyiko huu baada ya kupatwa mafua kwa siku tatu.
HUTASUMBULIWA NA KIKOHOZI,MAFUA HUTAZIBA PUA NA KERO ZINGINE BALI YATANYWEA NA KUTOWEKA NDANI YA SIKU3

Maandalizi mbadala.
Kama lengo lako ni kudhibiti tu mafua na si kuimarisha kinga ya mwili mzima BASI TANGAWIZI NA ASALI VINATOSHA! Pondaponda/twanga tangawizi mbichi
Chukua asali mbichi kijiko cha mezani changanya halafu kula asubuhi na jioni!
UTADHIBITI KIKOHOZI,MAFUA(hutaziba pua,utadhibiti chafya,mafua yatakuwa laini sana hatimaye kukata baada ya siku mbili au tatu!

Kama ukigundua dalili za mafua kabla hayajaanza(chafya mfululizo na pua kitekenya,mafua kulengalenga) UKILA TANGAWIZI HATA YENYEWE TU,YANAKATA!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom