Faida ya kutumia mkubwa wa jiko

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
Umuhimu wa matumizi ya chumvi kwa Binadamu


"Salt" Chumvi.



CHUMVI ni aina ya madini yenye umuhimu na faida nyingi, kwa mtumiaji, ikiwa atatumia kwa kiasi kinachotakiwa kwenye mlo wake.


Kwa maisha ya kawaida, huwezi kukosa madini hayo au kiungo hicho kwenye familia mbalimbali, mara nyingi utaikuta jikoni au hata mezani. Chumvi pamoja na muonekano
wake ni kiungo au madini ambayo hupatikana kwa urahisi na bei nafuu kuliko viungo vingine vya chakula au madini duniani.

Pamoja na umuhimu wake, lakini si rahisi ukasikia kesi au masuala ya chumvi kuibwa kama zilivyo bidhaa nyingine kwenye maduka mbalimbali. Mfano mdogo ni kiungo kama mafuta ya kula, hiyo ni bidhaa ambayo ukiiweka pamoja na chumvi, ukamwambia mtu achague bidhaa
moja aondoke nayo, wengi watachagua mafuta.

Lakini jamii inapaswa kufahamu kwamba, katika afya ya mwanadamu au hata mnyama chumvi ina umuhimu mkubwa, ingawa wengi wetu tunaona ni kiungo cha kawaida sana. Ni miaka mingi sasa chumvi (chloride), inatumika kuhifadhi vyakula, kuongeza ladha kwenye chakula na mara nyingine hutumika kusafisha vitu.

Kwa kawaida chumvi ni madini au tunaweza kuita rasilimali isiyoisha, ambayo hupatikana kwa urahisi na ili ifae kwa matumizi ya binadamu huhitaji kuongezwa madini joto.

Chumvi huzalishwa kwa njia mbalimbali, kuna chumvi iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya matumizi ya jikoni, mezani na pia ipo chumvi iliyoongezwa madini ya chuma ambayo ndiyo inayotumika kwa wingi katika jamii.

Kwa wale wasiofahamu manufaa ya chumvi na matumizi yake ni vyema wafahamu na kuchukua hatua kwani matumizi ya chumvi pia ni tiba kwa baadhi ya maradhi na pia hupunguza kero zitokanazo na kuumwa na wadudu mbalimbali.

Kwa matumizi jikoni Mbali na kutumika kwenye maabara kwa kuhifadhi vyakula, kuoka, chumvi hutumika jikoni kwa kuongeza ladha kwenye vyakula mbalimbali vipikwavyo.
Pia chumvi hutumika kuchunguza iwapo mayai ya kuku au bata kama ni mabovu au mazima.

Katika upimaji huo, tumia kijiko cha chai kupima, ambapo weka chumvi vijiko viwili, changanya na maji kwenye bakuli au chombo, kisha tumbukiza yai moja baada ya jingine.

Ikiwa yai ni bovu litaelea juu ya maji na kama ni bovu au lina muda mrefu tangu litagwe na kuku au bata litazama kwa kuwa kiwango cha hewa ndani ya seli ya yai huongezeka kadri yai linapokaa muda mrefu baada ya kutagwa.

Hata hivyo kama yai limeelea huenda sio bovu ila limekaa muda mrefu baada ya kutagwa na njia muafaka wa kubaini baada ya kulipima kwa njia ya chumvi ni kulipasua na kuona ndani kuna nini. Kadhalika yai kama ni zima litazama hadi chini kwenye chombo husika.

Kuhifadhi matunda yasiharibike rangi Matunda mengi duniani kama vile tufaa na peas huhifadhiwa kwa kutumia limau au siki kufanya matunda hayo yasibadilike rangi na kuwa ya udhurungi au kahawia.

Lakini chumvi nayo hutumika kwenye kazi hiyohiyo kwani sio wote wenye uwezo wa kununua siki au malimau ya kutosha kuhifadhi matunda, ila kiasi kidogo tu cha chumvi kilichochanganywa na maji hufanya matunda kuwa katika rangi yake ya kawaida kwa muda mrefu.

Usafi wa kinywa Chumvi hutumika pia kufanya mswaki wako udumu muda mrefu. Kabla ya kutumia mswaki mpya chukua kiasi kidogo cha chumvi changanya na maji kisha tumbukiza mswaki kwa muda kidogo halafu utoe.

Njia hiyo hufanya mswaki kudumu muda mrefu bila kuharibika, kukakamaa au kutengeneza umbo kama ua lililochanua. Kadhalika chumvi hutumika kusafisha meno, ambapo kiasi kidogo
cha chumvi huwekwa kwenye mswaki na mtumiaji kuswaki ambapo matokeo yake meno hung’aa na kuwa imara.

Wataalamu wa afya ya kinywa wanasema chumvi ni nzuri pia kwa kutunza kinywa dhidi ya harufu mbaya. Katika jamii wapo baadhi ya watu ambao midomo yao hutoa harufu. Ili kuzuia kero hiyo kiasi cha chumvi pamoja na maji ya uvuguvugu mtumiaji husukutua kinywa na hatimaye kuondoa harufu hiyo mbaya.

Kuumwa na wadudu Watabibu wanasema chumvi hutumika pia kutibu au kupunguza makali
ya kuumwa na wadudu kama vile nyuki na wadudu watambaao. Utafiti wa sayansi mbalimbali katika vyuo vya tiba na dawa nchini Marekani, na Uingereza wanasema kiasi cha chumvi husaidia kupunguza maumivu ya kuumwa na nyuki au wadudu wengine.

Kiasi kidogo cha chumvi huwekwa kwenye eneo lililoumwa na nyuki au wadudu na baada ya muda kidogo, maumivu hupungua kama sio kuisha. Pia kuna baadhi ya watu wakiumwa na mbu hubakia na vipele ambavyo vina maumivu, hivyo wataalamu wanashauri kwamba kiasi cha chumvi kilichochanganywa na mafuta ya mzeituni kitumike kutibu eneo hilo.

Kadhalika magonjwa ya koo kama vile muwasho wa mafua kiasi cha chumvi ilichochanganywa na maji ya uvuguvugu, mgonjwa akitumia kusukutua, huleta nafuu kwa mgonjwa. Chumvi hutumika pia kufukuza wadudu kama vile sisimizi na siafu nyumbani.

Kwa wapambaji kwenye maeneo mbalimbali kama vile kumbi za harusi na hata nyumbani, chumvi hutumika kufanya maua yadumu kwa muda mrefu bila kunyauka. Chumvi kiasi huchanganywa kwenye maji katika chombo cha maua na kisha kutumbukiza maua, ambayo
yatadumu kwa muda mrefu bila kunyauka.

Hayo ni baadhi tu ya matumizi ya chumvi kiafya na pia katika matumizi mengine, wataalamu wa afya wanashauri kwamba kiasi cha chumvi mwilini ni muhimu kwa afya na uhai wa binadamu. Hata hivyo wataalamu wa afya wanashauri kwamba chumvi itumike vizuri kwani itumikapo vibaya huwa na madhara mbalimbali.

Madhara hayo hutokana na jinsi chumvi hiyo ilivyotayarishwa yaani kutoka kuchimbwa ardhini hadi kufungashwa tayari kwenda kwa mlaji.

Mtu akipatwa na shinikizo la damu ana uwezekano mkubwa wa kuwa na magonjwa ya moyo, ambayo ni pamoja na moyo kushindwa kusukuma damu na mengineyo ambayo huweza kusababisha mtu akapatwa na mshtuko wa ghafla wa moyo na kisha akapoteza maisha.

Jambo hilo limegunduliwa na Watafiti wa masuala ya afya wa vyuo mbalimbali duniani wakiwemo wa Chuo Kikuu cha California, Marekani. Imebaikina kwamba kwa kila binadamu wenye umri mkubwa watatu, mmoja kati yao anasumbuliwa na shinikizo la damu.

Ushauri wa kitiba unasema ni vyema wanadamu wakapunguza matumizi ya chumvi yasiyo na lazima kwenye vyakula. Inashauriwa kwamba kwa siku moja kiasi cha miligramu 2,400 cha
chumvi ndicho kinahitajika mwilini na si zaidi.

Kiasi hicho ni sawa na kijiko cha chai kimoja, na kwa wale wenye tatizo la shinikizo la damu kiasi cha miligramu 1,500 sawa na nusu kijiko cha chai cha chumvi. Mtafiti katika chuo hicho,
Dk.Kirsten Bibbins-Domingo anasisitiza matumizi sahihi ya chumvi kiasi kwa ajili ya kupunguza uwezekano wa kupata maradhi yanayotokana na shinikizo la damu.

Kwa wale wanaopenda kula vyakula vilivyokwisha fungashwa ni vyema wakasoma maelekezo na kuona kiasi cha chumvi kilichowekwa, ili kuepuka matumizi mengi ya madini hayo mwilini.
Anasema chumvi ikitumiwa kwa kiasi haina madhara na pia ni dawa, lakini matumizi mabaya ya madini hayo huleta madhara makubwa kwa afya wa walaji, pasipo wao kufahamu.

Katika matokeo ya utafiti mmoja kuhusu matumizi ya chumvi kwa binadamu, wanasayansi wa tiba wamebaini kwamba matumizi madogo ya chumvi hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya mishipa ya moyo.

Kila mwaka magonjwa mapya ya moyo zaidi ya 120,000 hujitokeza, wanaopata kiharusi wakiwa zaidi ya 67,000 na mshuko wa moyo wagonjwa zaidi ya 100,000. Wagonjwa hao ni katika pembe mbalimbali za dunia na kwamba matumizi sahihi ya chumvi kwa waliozingatia yamesaidia kupunguza tatizo hilo kwa Bara la Afrika na Amerika.

Matumizi hayo sahihi wa watu wa mabara hayo mawili yamesaidia kuzuia vifo takribani 92,000 kwa mwaka.
DARASA HURU-SHULE YA BURE: Umuhimu wa matumizi ya chumvi kwa Binadamu

PAMOJA NA FAIDA YA CHUMVI KWA MWILI WA BINADAMU LAKINI USITUMIE CHUMVI KWA WINGI SIO NZURI WAWEZA KUPATA MARADHI YA PRESSURE UWE MUANGALIFU SANA.
 
Je ni kweli chunvi ile ya mawe ni nzuri kuliko hizi zingine za viwandani?
Kwa hakika, ila tu chumvi hii haina madini ya iodine ambayo ni mhimu sana mwilini, suala liko hivi, Ile ya unga ya mezani (iliyopita kiwandani) huondolewa madini madini (zaidi ya 80 tofautitofauti) na madini hayo kuuzwa peke yake katika maduka ya madawa! la kwanza, la pili ni kuwa ili chumvi hiyo ibaki kuwa katika hali ya unga unga hivyo huongeza 'aluminium silicate' ambayo ni sumu mbaya katika mfumo mkuu wa fahamu wa binadamu, inatajwa kuwa ni moja ya sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer). Ndiyo maana siku hizi watoto mashuleni hawakawii kusahau masomo wanayofundishwa kila siku!.

Ukweli ni kuwa tangu watu walipoanza kufundishwa kuwa chakula chenye kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho kizuri kwa afya, idadi ya watu wanaougua shinikizo la damu/BP imezidi kuongezeka siku hadi siku, inavyoonekana BP si ugonjwa unaoweza kupona kirahisi mahospitalini,watu wana ishi nao siku hadi siku!!! Utasoma post nyingine hapo chini itaeleza CHUMVI ni nini.

Mwanzo | maajabu ya maji
 

CHUMVI NI NINI?


Stori kuhusu chumvi:
Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.


Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.

Ukweli kuhusu chumvi:
Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya. Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.


Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela. Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa. Neno 'salary' (mshahara) linatokana na neno 'salt' (chumvi).

Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, 'Nimekula chumvi nyingi' kumaanisha kuishi miaka mingi.

Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula. Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.

Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao 'cerebrospinal fluid (csf)'. Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.

Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).

Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi. Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa. Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja. Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.

Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.

Chumvi imeundwa kwa Sodiamu na Klorini, kwa pamoja inaitwa; 'Sodiamu kloridi' (Na Ci).

Sodiamu ni metali laini yenye chaji chanya (+), wakati Klorini ni gesi yenye chaji hasi (-) ambayo hubadilika kuwa katika hali ya umajimaji inapoongezewa shinikizo.

Klorini ni gesi au umajimaji, lakini kwa namna fulani wakati dunia imeumbwa, klorini ilibadilika kuwa ngumu pamoja na sodiamu na madini mengine. Unaweza kuisaga chumvi na kuwa katika unga, klorini bado itabaki na sodiamu.

Klorini katika hali ya ugumuugumu, huitwa Kloridi.

Chumvi tutumiayo siku hizi inatoka katika bahari, maziwa, mito au katika migodi ya chumvi. Zaidi ya sodiamu na klorini, chumvi yote kwenye sayari yetu huja pamoja na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake!.


Kwa hiyo tunaweza kuona ni jinsi gani madini hayo yalivyo na umhimu kwetu, la sivyo yasingeshikamanishwa na chumvi. Kwa sababu ya thamani yake kibiashara, madini hayo huondolewa ili kutengeneza faida kubwa.
Mwili wa binadamu una uwezo wa kuienguwa klorini kutoka katika sodiamu kadiri inavyohitajika. Damu yetu huihitaji klorini kama zifanyavyo ogani zingine ndani ya miili yetu.

Tumbo huitumia klorini kutengeneza haidrokloriki asidi inayohitajika ili kuuwezesha mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanya kazi vizuri.

Miili yetu pia huitumia sodiamu kloridi kama chumvi kuufanya ubongo, uti wa mgongo, machozi, mifupa, tezi za jasho, ogani na damu kufunikwa na chumvi.

Mwili unanufaika pia kutoka katika madini mengine yaliyomo katika chumvi ili kuuweka katika hali ya ualikalini na afya.

Ni kama na vile kwa kunywa maji kuzidi kunaweza kumuua mtu (hyponatremia), vivyo hivyo kwa kutumia chumvi kuzidi, kunaweza sababisha; uvimbe, kuharisha na kifo.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile 'aluminium silicate' huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).


Sodiamu iliyozidi inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vingi vyenye viongezi (additives) vya sodiamu. Sodiamu siyo chumvi, chumvi ni sodiamu-kloridi. Sodiamu bikaboneti, sodiamu benzoeti na monosodiamu glutameti (msg) ni baadhi ya viongezi hivyo.

Sodiamu, potasiamu na kloridi ni elektrolaiti (madini maalumu) ambayo huyeyuka katika maji na kubeba chaji za kiumeme na kuzipeleka sehemu zozote za mwili kuliko na maji. Madini haya yenye chaji za kiumeme yana uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya seli kwa uhuru wote, huku yakipeleka lishe ndani na kubeba nje taka na maji yaliyozidi ili kuiacha seli katika hali yake ya usawa (balanced cell).

Wakati huo huo, kadiri elektrolaiti hizi zikitembea ndani na nje ya seli na kufanya mabadiliko yake, usawa maalumu wa Potasiamu ndani ya seli lazima utunzwe kwa kiasi maalumu cha sodiamu na kloridi ili kuishikilia potasiamu ndani katikati ya seli.

Elektrolaiti zinapatikana kwenye majimaji yote mwilini na hubeba mapigo (impulses) kwenye neva zetu. Kitendo hiki huusaidia moyo na kiwambo cha moyo (diaphragm) kusinyaa na kulegea.

Elektrolaiti hubeba Glukozi (damu yenye sukari) na kuipeleka ndani ya seli baada ya Insulini kufungua milango kwa ajili ya sukari kuchukuliwa.

Elektrolaiti pia huwasha pampu za kuzarishia nguvu ziitwazo kwa kitaalamu 'Cation pumps' ambazo huzarisha umeme ambao huifadhiwa kwenye beteri zijulikanazo kwa kitaalamu kama 'mg Adenosine Triphosphate (mgATP)' na 'mg Guanosine Triphosphate (mgGTP)' za mwili.

Ikiwa mtu atapungukiwa kwa kiasi kingi cha Elektrolaiti hizi kutokana na kuharisha au kwa sababu ya dawa za kukojosha (diuretics), anaweza kuwa mgonjwa sana na itamlazimu kwenda hospitali kupewa elektrolaiti hizi katika mfumo wa dripu (intraveneous fluid, IV), kama vile; maji chumvi (saline solution), maji sukari (dextrose fluid) na madini.

Siku hizi vinywaji vyetu vingi baridi vinaongezwa kafeina ambayo ni kikojoshi kinachoyalazimisha maji kutoka ndani ya mwili na kutusababishia upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, hakuna kinywaji ambacho ni mubadala wa maji.

Wanasayansi na madaktari bado hawaelewi ni kwa jinsi gani chumvi huyeyuka ndani ya maji au ni kwa vipi iwezavyo kuendelea kuwa na hali ya uchumvi na uchumvi. Wanasayansi na wanakemia wana baadhi za nadharia, lakini bado hawajaweza kuzithibitisha. Bado imebaki kuwa ni fumbo (mystery).

BAADHI YA KAZI ZINGINE MHIMU ZA CHUMVI MWILINI:



  • Chumvi huyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli. Inarekebisha uwiano sawa wa kiasi cha maji yaliyopo nje ya seli. kuna bahari mbili za maji ndani ya mwili, bahari moja imejishikiza NDANI ya seli, na bahari nyingine ya pili imejishikiza NJE ya seli. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa ujazo wa maji uliopo baina ya bahari hizi mbili, na usawa huu unawezeshwa pekee na chumvi, chumvi ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi.

  • Chumvi husaidia kuondoa dalili za mfadhaiko (stress).

  • Figo hazitaweza kufanya kazi zake vizuri bila chumvi.

  • Kukata tamaa na matatizo ya kisaikolojia, vitaondolewa kwa kuchukuwa chumvi zaidi, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya kutembea.

  • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kurudishwa katika hali yake ya kawaida kwa kuchukuwa kipande cha chumvi na kukiweka mwishoni mwa ulimi na kukifanya kiyeyuke.

  • Mifupa inapata uimara wake toka katika chumvi, na siyo katika kalisiamu pekee.

  • Je wewe ni mwanaume na unashindwa kuhimili kusimama? unahitaji chumvi zaidi na kunywa maji halisi zaidi.

  • Kuichukuwa chumvi na kunywa maji kabla ya mazoezi, kutakusaidia kupumua vizuri na kutokwa na jasho chache.

  • Matatizo ya kibofu cha mkojo na upotevu wa mkojo wa makusudi, vingeweza kurekebishwa kwa kuongeza chumvi zaidi kwenye mlo wako.

  • Dalili za maumivu ya jongo (Gout) zinaweza kuzuiwa kwa kutumia chumvi.

  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia kuvimba kwa mishipa na vena kwenye miguu.

  • Kwa sababu tunapata potasiamu karibu katika kila chakula tunachokula, chumvi inatakiwa kuongezwa katika milo yetu, hii itairuhusu miili yetu kuhimili usawa sahihi wa maji kati ya bahari ya ndani na ile ya nje ya seli.

  • Chumvi ni mhimu ili kuondoa asidi iliyozidi kwenye seli, hasa seli za ubongo.

  • Chumvi ni mhimu kwa ajili ya kusawazisha kiasi cha sukari kwenye damu, hivyo kuzuia ugonjwa wa kisukari.

  • Chumvi ni mhimu katika uzarishaji wa nguvu umeme itokanayo na maji katika seli zote za mwili.

  • Chumvi ni mhimu katika mawasiliano ya neva na ufanikishwaji wa taarifa wakati wote seli za ubongo zinapofanya kazi tangu kuzaliwa hadi kufa.

  • Chumvi ni mhimu katika umeng'enywaji wa chakula na madini kwenye utumbo mdogo (intestinal tract).

  • Chumvi ni mdhibiti madhubuti dhidi ya histamini.

  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia mikakamao ya mishipa (cramps).

  • Chumvi ni mhimu katika kusafisha makohozi na kubana kwa kifua.

  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia uzarishaji wa kuzidi wa mate katika kiwango kwamba yanatoka nje ya mdomo wakati umelala, kitendo hiki cha kutoa mate (udenda) wakati umelala ni dalili ya upungufu wa chumvi mwilini.

  • Chumvi ina umhimu mubwa katika uimarishaji wa mifupa. Ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya upungufu wa chumvi na maji mwilini.

  • Chumvi ni mhimu katika usafishaji wa makohozi mapafuni na maji yaliyogandamana hasa kwa watu wenye pumu, ikiwa inakulazimu kusafisha koo kila wakati, ni dalili kuwa umepungukiwa chumvi.


CHUMVI KIASI GANI:
Dr.Batmanghelidj anashauri; ¾ (robotatu) gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji (16 ounces), au nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji, au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji tunayokunywa. Hiki ni kiasi kizuri kwa kuanzia na siyo kanuni, tafadhari tumia aina ya kijiko kilichotajwa hapo juu kwa vipimo sahihi.

Ukiona viwiko, vidole au kope za macho zinavimba, usitumie chumvi kwa siku 2, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena.



NAMNA ZA KULA CHUMVI:



  • Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

  • Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.

  • Unaweza pia kunywa nusu ya maji unayotaka kunywa, kisha utamung'unya taratibu chumvi mdomoni kama ulavyo pipi, na kisha umalizie nusu ya maji iliyobaki.

kuichanganya chumvi pamoja na maji ya kunywa si wazo zuri sana.


Mhimu: Tumesema chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini madini mengine zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake, lakini hatuwezi kubeza umhimu wa madini joto (iodine) kwa afya ya mwili, ikiwa ni hivyo basi, tunashauri kwa wale ambao hawana vyanzo vingine vya madini hayo ya joto kutumia chumvi zote mbili yaani robo tatu ya matumizi yawe chumvi ambayo haijasafishwa na robo nyingine iwe ile iliyosafishwa ili kuepuka kupungukiwa madini hayo mhimu. Tunasisitiza katika chumvi hiyo iliyosafishwa hakuna kingine kilicho mhimu zaidi ya madini hayo joto ambayo yanaweza kupatikana pia kwa kula vyakula vingi vya baharini (sea foods).


Mchungaji Stan Moore wa kanisa la Woods of life fellowship la Pembrook Florida nchini Marekani anasema aliuona ukweli kuhusu tiba kwa kutumia maji aliposoma biblia wafalme wa pili 2:19-22.


Je chumvi husababisha shinikizo la damu?:
shinikizo la damu | maajabu ya maji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom