Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

TUFAHA, TANGO NA FIGILI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TANGO CHUNGU,

ImportanceofFruitsInDiet1.jpg


TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI'
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu'.

PEASI NA NDIZI

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

PAPAI, NANASI NA MAZIWA
Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.

fruits22.jpg


NDIZI, NANASI NA MAZIWA

Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya'.

Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.
 
Mkuu nipenda sana juisi mpaka basi lakini ngozi yangu hasa usoni ninapata chunusi saanaa why?
 
Mkuu nipenda sana juisi mpaka basi lakini ngozi yangu hasa usoni ninapata chunusi saanaa why?

Jaribu kutumia dawa hii ya Chunusi:
Chukua unga wa habbasouda kwa kiingereza unaitwa (Nigella sativa seed)ukande katika mafuta ya ufuta (simsim) pamoja na kijiko kimoja cha unga wa ngano, jipake usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu osha kwa maji yenye uvuguvugu na sabuni. Endelea kufanya hivo kwa muda wa wiki moja. Na uwe unakunywa mafuta ya habbasouda(Nigella sativa oil) ndani ya maji ya Uvuguvugu.
 
Juisi ni kinywaji bora, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali.


Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki.


Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini:


KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO
Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo (apple) husafisha sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.


EPO+TANGO+FIGILI
Juisi ya mchanganyiko wa tunda la epo, tango na mboga ya majani aina ya Figili (celery) hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.


NYANYA+KAROTI+EPO
Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na epo huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.


CHUNGWA+TANGAWIZI+TANGO
Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.


NANASI+EPO+TIKITI MAJI
Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.


KAROTI+EPO+PEASI+EMBE
Juisi ya mchangayiko wa karoti, epo, peasi na embe hushusha joto la mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na matatizo ya kupumua.



PAPAI+NANASI+MAZIWA
Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).


NDIZI+NANASI+MAZIWA
Nao mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa una vitamin nyingi na virutubisho vingi na huondoa tatizo la ukosefu wa choo.


Kwa ujumla, juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo ukitumiwa kama ipasavyo hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili na huweza pia kuwa tiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo awali. Ili uone faida za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi.
 
Ni somo zuri lakini kwa wasiojua kusoma wakiamua kutumia PICHA hizi wameumia, maana yake vitu vingine watakuwa hawajawahi hata kuviona. Hivi ulikosa picha za hivyo ulivyoviandika (picha kubwa inayoonekana vizuri)????? yaani vitu kama tangawizi, chungwa, karoti,papai, na mengineyo.
 
Ni somo zuri lakini kwa wasiojua kusoma wakiamua kutumia PICHA hizi wameumia, maana yake vitu vingine watakuwa hawajawahi hata kuviona. Hivi ulikosa picha za hivyo ulivyoviandika (picha kubwa inayoonekana vizuri)????? yaani vitu kama tangawizi, chungwa, karoti,papai, na mengineyo.
Watu humu ndani mkuu hawafuati picha wanachofuata maelezo yako hebu na wewe toa hizo picha na utoe maelezo yake Watu wapate kukufuata.
 
Back
Top Bottom