Faida na athari za mafuta ya "ubuyu"

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
3,211
988
Maajabu ya juisi ya Ubuyu

Ubuyu8.jpg


Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng'ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng'enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.


Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.


Tazama video hapo chini jinsi ya kuandaa juisi hii ya ubuyu. Ikiwa utahitaji unga wa ubuyu uliotayari kama utakaouona kwenye video hii usisite kuwasiliana na mimi kwa simu namba 0769142586 au email hizi: info@fadhilipaulo.com au fadhilipaulo@gmail.com

Makala hii ni kutoka fadhilipaulo.com

 
Last edited by a moderator:
Nimetoka kunywa jana tu ila mtoto Wangu aipendi mpka nichanganye na Matunda mengine vip hapo itakuwa pouwa?
 
kama haiongezi nguvu za kiume, kwangu mimi haina mantiki
 
Isije ikawa kama yale mafuta ya ubuyu ambayo watu waliyafakamia mwisho wa siku ikawa taharuki baada ya yule jamaa wa external kuamka toka usingizini
 
Mafuta na juisi ni vitu viwili tofauti na hata hayo mafuta ni njama tu za watu wachache kuwaharibia kazi wajasiriamali

Isije ikawa kama yale mafuta ya ubuyu ambayo watu waliyafakamia mwisho wa siku ikawa taharuki baada ya yule jamaa wa external kuamka toka usingizini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom