Fahamu tafsiri sahihi ya "computer" kwa kiswahili.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Remote, Jul 15, 2011.

 1. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 13,110
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 48
  Waswahili wengi hufikiri kwamba hakuna maana halisi ya computer na badala yake wanatohoa neno hilohilo nakuandika "Kompyuta". Hivyo ni makosa maana halisi ya Computer ni neno "NGAMIZI" na kwa laptop computer huitwa "NGAMIZI PAKATWA" Source: Ulimwengu wa kiswahili TBC1, Nawasilisha.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 22,764
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 113
  tarakilishi ni nini?
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 14,063
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 83
  Hata mimi nilidhani vivyohivyo!
   
 4. M

  Mtata Mbosa Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ni jibu sahihi """TANAKILISHI"""
   
 5. r

  rununu Senior Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! nakumbuka kuna mtu alishawahi kusema, je TARAKILISHI na NGAMIZI ni sawa? maana mimi naifahamu kuwa ni Tarakilishi
   
 6. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 690
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  Nawalaumu sana hao wanatoa tafsiri za maneno na vitu mbalimbali. Tukiangalia kwa uzuri lugha ni muingiliano wa lugha mbalimbali. Ndio maana tuna maneno bora kama shati, meza, chai, pesa, hela, gari n.k. Hivi kwa nini fan iitwe pangaboi badala ya feni tulivyozoea? Computer ingekuwa komputa, television ingekuwa televisheni, fax mashine ingekuwa faksi n.k. Hakuna ubaya kuiga. Lugha zote zinaiga.
   
 7. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 2,618
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 48
  Congo nakubaliana na wewe ila nafikiri computer ingeitwa kompyuta badala ya komputa!
   
 8. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 690
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  La muhimu hapa kwa mawazo yangu ni kuwa kitu tumekitumia kwa miaka nenda rudi kwa jina fulani. Wataalamu wanakuja na majina ya ajabuajabu. Ah nimekumbuka, calcultor inaitwa kikokotozi, ovyo kabisa. Tungesema kalikuleta. Asante.
   
 9. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,863
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 48
  Eti kiwembe cha kuchongea pencils kinaitwa KIFIRIO. Duh kazi kweli kweli.
   
 10. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,182
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 38
  Ninajaribu kukuelewa: unaona kama ni kupoteza wakati na rasilimali kutafuta tafsiri ya 'Kiswahili' ya maneno hasa yanayohusiana na sayansi na teknolojia. Unadhani hakuna haja ya kuwa na istilahi mpya, unataka tuendelee na 'utohozi'.

  Sioni shida sana ingawa sikubaliani na wewe kwenye baadhi ya maeneo.

  Lakini, huu u--'hovyo' unaouona umeutoa wapi?
   
 11. r

  rununu Senior Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana na wewe kabisa lugha hukua hasa ukizingatia kuwa tupo katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia na kuwa kuongeza istilahi si lazima utohoe au uangalie mazoea ya matumizi ya neno husika, tutatohoa hadi lini wakati uwezekano wa kutafuta istilahi mpya upo? kiswahili si maskini kiasi cha kutohoa kila neno, mimi naona ni vema kutumia haya maneno mapya kuliko yale tuliyoyazoea, na tuache kutumia lugha ya kiswahili kwa mazoea.
   
 12. P

  PSYCHOLOGY JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  swahili kina wenyewe.
  Ndio muwatafute majibu mtayapokea ya kutosha . Watu wa bara swahili wapi na wapi?
   
 13. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni sawa kabisa
   
 14. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2014
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiswahili raha
   

Share This Page