Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Hahahahaha lol!!!! Umenikumbusha dada mmoja hapa aliwahi kuandika kwamba asali pia hutumika katika lile tendo linaloitwa "tendo la ndoa" na jinsi ilivyo bomba na kuongeza utamu wa tendo yeye nyumbani kwake hakosi asali hata siku moja. Kesho yake wauza asali wote Dar walipandisha bei ya asali na miezi miwili asali ikaadimika sana MUJINI.

CC: Nyamayao


Ukitaka kuwapata Wabongo wengi watajie hapo kwenye bold nyekundu utaona hata bei ya asali kwenye soko itapanda. Maana tunapenda hiyo kitu kupita kiasi na ndio maana mabango ya waganga wa kienyeji yamekuwa yakilenga hiyo kitu.
 
Last edited by a moderator:
Dr Mzizi Mkavu asali nzuri inayotibu maradhi uliyoyataja hapo juu ni asali gani? ya nyuki wadogo au wakubwa? na inatakiwa iwe mbichi au iwe imepikwa?
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa majibu yako mzee nitashughulikia leo afu kesho nitaweka feedback hapa

Nimejaribu kiukweli tumbo limeniuma sana hata kuamka sasa ndio naamka nielekee kazini kwani tumbo lilikuwa na gesi ila nimezitoa zote sasa lasuka suka tu, sijui tatizo langu ni lipi
 
Habari za muda huu wana-JF!

ASALI inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini katika kujenga afya bora.

Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork.

Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwamba matumizi ya kila siku ya asali yanapunguza viwango vya lehemu mwilini.

Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha imegundulika na wataalamu kwamba hupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti mmoja wa Hispania imethibitisha kwamba, aina ya dawa moja asilia iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo mafua ilitengenezwa kwa kiwango kikubwa na asali.

Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo. Asali inaaminika pia huamsha hamu ya tendo la ndoa. Wale ambao mambo katika eneo hilo si mazuri wanashauriwa angalau kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Kuna wakati asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya kuwaongezea mihemko.

Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji, itapunguza hali hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

Utamaduni wa kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi uliofanywa huko India na Japani kwa miaka mingi. Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia, mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara wakati wa kifungua kinywa.

Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu, pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali iliyochanganywa na mdalasini.

Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja, wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba unaonesha kwamba, asali ina hazina kubwa ya virutubisho na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga, itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea virusi na bakteria. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia pia. Inasemekana kuwa, unaweza kuishi hadi miaka 100 ukifurahia maisha ya afya bora na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai iliyowekwa mdalasini na asali.

Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10, kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne, watafiti wanasema.

Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee. Asali, wanasema inairudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondola, washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

Utafiti uliofanywa karibuni nchini Australia na Japan, umeonesha kuwa, asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa ya kutibu saratani. Katika utafiti uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wakitumia madawa ya saratani pekee. “Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi,” anasema Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. “Kunywa tena saa 9:00 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka,” anashauri Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.

Asali inao uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

Baadhi ya watu Marekani ya Kusini, wanasukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi ili kufanya harufu mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).

Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za asali na mdalasini, hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi mkutanoni kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani. Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa. Lakini inayozungumzwa hapa ni asali mbichi ambayo inapatikana kwa wingi Tanzania, lakini tatizo kubwa ipo pia feki inayouzwa kama mbichi!

Kwa hisani ya AFYA.KWANZA
 
iyo imekaa poa xana mkubwa, asante kwa somo bt utaijuaje mbch na ambayo c mbch?
 
1972373_10154452754960198_5570273292799709668_n.jpg
10491211_10154452760175198_6753893315303117684_n.jpg



Asali inatibu Maradhi haya Hapa chini:
1. Ugonjwa wa viungo/maumivu na uvimbe.
2. Kukatika kwa nywele.
3. Ukungu wa miguu.
4. Maambukizo kwenye kibofu cha mkojo.
5. Maumivu ya jino.
6. Lehemu (Cholestral).
7. Ugumba
8. Mchafuko wa tumbo.
9. Ugonjwa wa moyo
10. Shinikizo la damu.
11. Kinga ya mwili.
12. Ukosefu wa nguvu za kiume.
13. Flu.
14. Umri wa kuishi.
15. Chunusi.
16. Kuumwa na wadudu (kwa washawasha) wenye sumu.
17. Madhara ya ngozi.
18. Kupungua kwa uzito.
19. Saratani.
20. Uchovu mwilini.
22. Harufu mwilini.
23. Kupungua kwa usikivu.


Matumizi ya Asali kwa hayo Maradhi niliyoyataja hapo juu kula Asali kijiko kimoja Asubuhi kabla ya kula kitu kijiko kimoja mchana na kijiko kimoja usiku kula kila siku utapona kwa kila maradhi uliyonayo mwilini mwako.

Kuleni Asali mupate Afya na nguvu mwilini
 
Mkuu asali naipenda lkini kila nikiila tu ni shida yani tumbo linauma naharisha tu...nimeamua kuachana nao tu huku hata chupa aijaisha kabixa...!!sijui ttzo ni nini hapo???
 
Mkuu asali naipenda lkini kila nikiila tu ni shida yani tumbo linauma naharisha tu...nimeamua kuachana nao tu huku hata chupa aijaisha kabixa...!!sijui ttzo ni nini hapo???

Mi naipenda kutumia ila inanishinda mana
nikiila sana tumbo hujaa gesi mda wote.
 
Mi naipenda kutumia ila inanishinda mana
nikiila sana tumbo hujaa gesi mda wote.

Mkuu jaribu kuchunguza kiwango cha ubora wa asali unayotumia!

Kuna asali zinauzwa mitaani ubora wake unatia wasi wasi..kuanzia chombo kilichoihifadhi hadi ladha yake.
 
Back
Top Bottom