Facebook imenishinda!!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kwa zaidi ya mwaka na nusu sasa nimeshindwa kabisa kuiendesha Akaunti yangu ya face Book. Tatizo kwanza marafiki zangu niliowatafuta FaceBook wengi hawakupatikana na waliopatikana nadhani kutokana na majukumu yao tumeshindwa kuzifanya Akaunti zetu ziwe hai.

Kuna Binti mmoja ni meneja Kwenye Benki fulani hapa jijini nilipomuomba urafiki akakubali, hatimaye nikaishia kuambiwa "shikamoo kaka' hata wewe una akaunti ya Facebook?" tangu hapo hajawahi kuchangia chochote kwenye wall yangu ingawa mara zote namuona yuko online.

Nimegundua kwamba inawezekana kumbe umri nao umenitupa mkono, kwani wale niliowaona wakizaliwa sasa ni mameneja kwenye mabenki kwa hiyo wananiona kama vile nimevamia viwanja vyao. sijui niifunge akaunti yangu?
 
Umri unaweza kuwa sababu kwani kuna dhana hiyo kuwa facebook ni kwa ajili ya kizazi cha dot.com. Lakini zaidi, facebook nahisi mara nyingi sio pahali muafaka kwa kurejesha uhusiano uliokwishavunjika. Kwanza, kama kulikuwa na urafiki wa kweli, sio kujuana, isingefika hadi mkatengana. Pili, ikiwa mlikuwa marafiki kweli, hampaswi kuishia kuwa na mawasiliano katika facebook tu, bali nyia nyengine kama vile simu na anuani za posta.

Mimi kinachonishinda kwenye facebook ni ule upuuzi wa watu kubandika ukutani kila kitu na kupeana Likes. Chochote kinachoandikwa kinagongwa malikes, comments za kufa mtu na maandishi ya kiajabu ajabu:

Nimegombana na mchumba wangu (so and so liked it)
Ninaumwa na kichwa (so and so liked it)
Nimefiwa na baba/mama yangu (so and so liked it).
 
Facebuk hakuna adabu kule,utakuta katoto ka form 6 au chuo,anamuadd mdada wa ofisini.hata hamjui,na ukute huyo mdada hajaweka inf.zake,halafu amuone ni kababy gal.yan ana baby face.kakijana kanatongoza tu.

Na huyo manager wa benki.kweli wanavyobanwa vile huo muda wa kuwa online muda mrefu anatoa wapi?.
Lastly,Facebuk haina umri,ni mtu 2 kujiheshimu.
 
HIvi unajua kila kitu unacho kipost facebook kinakua mali yao?
Mfano: ukipost picha nzuri na wamiliki wakaitaka kibyashara
wanaruhusiwa kuitumia kwa njia yoyote wanayo itaka bila ruhusa yako
Actually mkienda mahakamani wanaweza kukuomba wewe ulipe
ikiwa utatumia picha yako ya fb kufanyia biashara sehem nyingine
 
mh,kaz kwel kwel
 
Nilishindwana nayo zamani sana yani. We fikiria class mates, priests, neighbors, casual friends, intimate friend, family, boss, colleagues, business partners all under one roof.
Na mbaya zaidi class mate akapekue details za intimate friend, in worst cases amu-add friendship licha ya kwamba hamjui! Facebook hiyo.
 
Kwani how old r u?.Kuna some circumstances as the age goes,majukumu yakiwa mengi,mtu hustop mambo kadhaa.mwingine cyo age tu,utakuta mambo yamekuwa mengi,sasa muda wa kujitundika online fb,wakati mambo kibao unasubiria uyafanye hailet picha nzuri.Madent sawa,ndo time yao.ila mfanyakazi.Mmh.Its ur own decision kufunga.Kama Facebuk inakuingizia kipato ya nini ufunge?.Otherwise,utaishia kuchat na watoto,uanze kuamkiwa kama huyo rafiki yako manager wa bank.Kama kazi zimezid funga.I like fcbk.
 
HIvi unajua kila kitu unacho kipost facebook kinakua mali yao?
Mfano: ukipost picha nzuri na wamiliki wakaitaka kibyashara
wanaruhusiwa kuitumia kwa njia yoyote wanayo itaka bila ruhusa yako
Actually mkienda mahakamani wanaweza kukuomba wewe ulipe
ikiwa utatumia picha yako ya fb kufanyia biashara sehem nyingine

Vigezo na masharti kuzingatiwa! lol
 
Back
Top Bottom