f4 div1, f6 div 1 seminary , chuo Kikuu supp,supp na hatimae Pass ya kuchoka

muhogomchungu

JF-Expert Member
Jan 9, 2011
375
3
kuna wanafunzi ambao nawajua, walikuwa wazuri sana walipkuwa seminary school, kwa bahati ni wale waliokuwa wakiongoza shule zao kila miaka yaani 10 bora. lkn wanpokua vyuo vikuu huwa tofauti, yaani ukionyeshwa unaweza ukasikitika, ukahoji ulazima yeye kupata madaraja makubwa hayo. yaani ni mzigo darasani. hupitwa kabisa na wale wa div 3 shule za kata, shule za gov na shule nyengine.kwa tabia ni zile zile no change, kilichochenj ni matukio ya mitihani
supp kwake jambo la kawaida, mchango wake kwa wanfunzi wenziwe ni mdogo sana.
masomo ya chuo ni magumu?
 
Kwa hiyo unafikiri walichakachua au! Inawezekana ila mfumo ulipo unasema hivi ''WINNING IS EVERYTHING NO MATTER HOW YOU WIN''

Yan kama alichakachua, akapata DV 1, yeye anakua wakwanza kufikiriwa kupata loan ya kusoma chuo, anakuwa wa kwanza kufikiriwa kujiunga na chuo, anakua wa kwanza kufikiriwa ana akili! Hayo unayosema ni matokeo ya baadae kama ulivyojionea hawana mchango kwa wenzao! Lakini hiyo siyo kwamba inathibithisha alichakachua paper form VI!! inawezekana mazingira yamebadilika
 
Seminary ni 100% spoon feeding wakati ukienda chuoni au sule za serikali mda mwingi unasota mwenyewe prepo na kupigwa baridi kali ili ufaulu. Nakumbuka Alevel kulikuwa na mtu katoka seminary na div 1 ya 7....alipokuja shule ya serkali aliondoka form six na div 3 akakimbilia uganda Makerere manake alikosa chuo bongo.

Na pia chuoni eg MU Lecturer anakupa only 40% hizo 60% inabidi ukomae library ili ufaulu kitu ambacho seminary hakipo....nahisi umenipata.

To me, shule za seirkali ni nzuri kumjenga mtoto ajue kujitafutia material mwenyewe na sio kuwa spoon fed kama seminary nyinginezo.
 
Sababu ya Spoon feeding walipokuwa secondary school

Inabidi wajengewe na vyuo vyao vya seminary ili wapewe elimu ya chuo kikuu kwa mtindo wa spoon feeding na kupewa g.p.a za juu, wakipelekwa chuo kama dit au sua hawatafika mbali!!
 
Inabidi wajengewe na vyuo vyao vya seminary ili wapewe elimu ya chuo kikuu kwa mtindo wa spoon feeding na kupewa g.p.a za juu, wakipelekwa chuo kama dit au sua hawatafika mbali!!

Kwani SUA na DIT ndio kugumu? Nilidhani Medical School ndio balaa.
 
Inaweza kuwa kweli hoja yako si wote wanaofaulu form 4 au 6 wanafaulu pia vyuoni. Hii inatokana na mazingira mapya na ya uhuru zaidi ambapo hupelekea wale waliokuwa wanasoma kufuATA MKUMBO kushindwa. LAKINI ndugu naomba fanya research kidogo kati ya walimu wa vyuo vikuu ni wangapi wamepitia seminary. Department yangu walikua 7 kati ya 12. Fanya tu UDSM, ARU, MZUMBE,ETC acha SAUT halafu lete majibu.
 
@muhogo mchungu-sidhani kama ambacho unakileta jamvini kina ukweli asilimia mia ,let me ask you -unataka sema seminari ipi ya wakristu au waislam?then inatokea ktk kiwango kidogo kwa mtu kama huyo kupata gentleman chuo lakini kumbuka spoon feeding haipo seminari kwani mie mwenyewe nimesoma seminari ya mt.petro-morogoro na nimepata one o-level na advanced level vile vile nina one advanced na nimetoka chuo udsm mwaka jana na nina upper second na sijawahi sup unataka sema nini hapo ?labda ungechange title -SECONDARY DIV. ONE ,CHUO SUP SUP THEN PASS DEGREE ,WHAT IS THE MATTER?
 
@emrema,akhsante kwa kumuelekeza huyo jamaa maana amegeneralize muuuuno hadi inaboa,nimekugongea thank mkuu.
 
kuna wanafunzi ambao nawajua, walikuwa wazuri sana walipkuwa seminary school, kwa bahati ni wale waliokuwa wakiongoza shule zao kila miaka yaani 10 bora. lkn wanpokua vyuo vikuu huwa tofauti, yaani ukionyeshwa unaweza ukasikitika, ukahoji ulazima yeye kupata madaraja makubwa hayo. yaani ni mzigo darasani. hupitwa kabisa na wale wa div 3 shule za kata, shule za gov na shule nyengine.kwa tabia ni zile zile no change, kilichochenj ni matukio ya mitihani
supp kwake jambo la kawaida, mchango wake kwa wanfunzi wenziwe ni mdogo sana.
masomo ya chuo ni magumu?

Data zako hazitoshi na zimelalia upande mmoja tu mkubwa. Kuna jamaa kadhaa nawafahamu wamesoma shule za serikali na kupata ones kwa O and A levels lakini walidisco chuo kikubwa.
 
Maisha ya chuo ni tofauti na ya seminary mkuu!! Chuoni upo huru kujirusha au kusoma ! Sasa wale wanakuwa walibanwa sana. Hivyo wakiingia chuo wao ni kujirusha hasa na kujiachia , madisco, club, kunywa etc . hapo unategemea First class tena?
 
naomba kutoa hoja tofauti kidogo hapa..mtanisamehe kama nitawa-boa kwa hili...here goes...
miaka ya nyuma tulilalamika sana kuhusu kuvuja kwa mitihani, hasa ya kidato cha 4...hata serikali iliingilia kati kwa ku-muwasha moto aliyekuwa bosi mmoja/wawili hivi wa Baraza la mitihani....sasa je, kama Baraza limefanikiwa ku-PLUG ule uvujaji wa mitihani....hilo si linaweza kuelezea uvundo uliotokea mwaka huu? wanafunzi wetu walizoea mno kupata paper zilizovuja, wakabweteka, wakafeli mitihani.......kielelezo kizuri ni pale baadhi yao walipo tukana kwenye paper baada ya kuona wamekwaa kisiki!!
 
Huyo kijana anayefeli Chuo wakati alifaulu elimu sekondari anaweza akaelezwa tatizo ni lipi hasa kwake. Kumbuka huenda yeye kama individual ana idiosyncratic habits zake kwa hiyo blanket response ni ngumu kutolewa.
Ikiwa everything is constant, tunaweza kusema vitu kadhaa vinaletea kufeli kwake
1. Culture shock
2. Study strategies
3. Level of knowledge
Sababu ya kwanza hii inapata wengi na ndio maana ukitizama matokeo ya 1st semester au hata 1st year wengi wanapata alama za chini
Sababu ya pili, huletwa na kushindwa kubadilika kwa mwanafunzi ktk namna ambavyo anajisomea na anapowasiliana na wenzake au hata walimu kuhusiana na masomo. Sasa wale 1st years wanapogundua matatizo yao mapema ndio hufanya vizuri ktk mitihani ya mwaka wa pili na wa tatu. Hapa ndio wengine wanajifunza mambo ya madesa na mengineyo.
Sababu ya tatu inahusiana na namna ambavyo elimu hutolewa kwa wanafunzi wanapofika level ya chuo. Kwa anayeifahamu Bloom's taxonomy, haya nitakayoeleza hayatakuwa mageni sana. Elimu yetu ya sekondari inajikita bado ktk lower levels of knowledge hasa ktk utungaji wa mitihani. Japokuwa walimu wa form six wanapaswa kujua umuhimu wa kumfanya mwanafunzi awe na uwezo wa kupambanua maswali wengine hujikita katika levels za recall/knowledge questions which is very low. Mtu afikapo chuo anaulizwa maswali ya analysis na na aapplication akiwa masters anaulizwa maswali ya synthesis na akiwa PHD anatakiwa kufahamu nama ya kujibu maswali ya evaluation. Mara zote hata leo hii ukiwapa wanafunzi wa undergraduate swali la application wengi hushindwa kabisa na watatoka ktk chumba cha mtihani wakilaani sana. So namna ya utungwaji wa mitihani pia hufanya mtu aliyejikita ktk levels za chini ashindwe kufanya vizuri ktk maswali yanayohitaji upeo wa juu wa uelewa.
Hawa wa seminary inawezekana walikuwa wanatumia muda wakiwekeza ktk low level knowledge. Imefika wakati wa kubadilika wanashindwa kujua tofauti na hata wanatumia muda mwingi kutafakari kwa nini mbinu zao za zamani hazifanyi kazi tena. Mbaya zaidi huwa wanajitenga na watu maana wanahisi watu wamegundua udhaifu wao.
Sina mengi ni hayo tu.
 
Nadhani huwa wanafunguliwa uhuru wao sasa mademu wanawachanganya sana manake baadaye huwa wanatulia sana
 
..kuna factors nyingi sana zinazompelekea mwanafunzi kufeli.... Kupata One secondary haimaananishi atapata fist class university!.... Au unataka kusemaje?? Kwamaana nadhani kuna kaujumbe kamefichika ndani ya post hii!...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom