F.F.U wametapakaa kila kona ya manispaa ya Iringa Mjini!

Mliopo Iringa tujuzeni mkutano upo au haupo??na hali ikoje mpka sasa??
 
Tunawaomba vijana wa Iringa wasidanganyike na vihela wanavyo pewa wafanye fujo, hizo hela hazita kusaidieni baada ya kutenguliwa kiuno.
 
Kwani barua ya mkutano ilikua inasemaje?? Na kwanini mkutano uzuiwe na unafanyika saa 8, na mbona kuna muda mwingi tu wa kuhesabu watu, ila kama hali si hali, ni bora mkutano ukahairishwa kwa busara za viongozi, kuliko kuendelea kuwaangamiza raia wasio kuwa na hatia, kama ilivyotokea jana Morogoro.
 
Sidhani kama mkutano utakuwepo maana hamna dalili zozote, na hali ya mji ni shwari...
Chezea dola wewe. mkutano utakuwepo polisi ikiruhusu. Bila hivyo hakuna kitakacho endelea zaidi ya rasharasha.
 
Mtasema yote, ila mkutano hauto fanyika ulinzi ni mkali mno ambapo hata nzi wamekimbia licha ya binadamu. Hiyo ndio maana ya dola, ikisema kitu lazima kifuatwe na hakuna anae weza kuitisha dola, asogee mtu sasa aone atakacho fanywa.


Simba akivamiwa na mbwa mwitu hukimbilia miguuni pa binadamu, iko siku hayo mabomu, risasi havitakuwa msaada kwenu, mtaomba kurewind time haitawezekana.
PETER TOSH. DOWNPRESSOR MAN.
 
Hiyo kitu imeingiaje tena hapo?


Mhe. sweke34,
Nimeshafanya editing mkuu. Nilikuwa namaanisha CCM na siyo kanisa!

Unajua wengine huwa tunapeleka matatizo ya nchi kanisani kwa ajili ya maombi. Kwa hiyo wakti mwingine unapozungumzia critical problems za nchi hii unafikiria pia na maombi ili Mungu atunusuru na huu utawala dhalimu na mbovu uliokwisha poteza dira na mwelekeo!
 
Chezea dola wewe. mkutano utakuwepo polisi ikiruhusu. Bila hivyo hakuna kitakacho endelea zaidi ya rasharasha.

ccm kuhamishia makao makuu yake kwenye ghala la silaha/mabomu, kibaya zaidi ni kuwa wanavuta sigereti ndani ya ghala, haiko salama hata kidogo. Wameingia na majembe na nyundo zao, hawajui jinsi ya kukaa na mabomu, naona mwigulu anagonga gonga haya makitu kwa nyundo, Nape ana jembe, badala ya kulibeba begani, analiburuza juu ya maguruneti,
MSAADA TAFADHALI.
 
Kwa safari wanazofanya hawa F F U na magari yao ni dhahiri kwamba mafuta yaliyojazwa kwenye magari hiyo fedha ingetumika kwenye shughuli za maendeleo.
 


:


IMG_0886.JPG

Askari wa FFU mkoani Iringa wakiwa wametanda eneo la uwanja wa Mwembetogwa ambalo

Chadema ilipanga kufanyia mkutano wake leo wa kitaifa



IMG_0884.JPG







IMG_0885.JPG


Mkuu wa FFU mkoa wa Iringa afande Mnunka akiwa eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mkutano wa Chadema

IMG_0883.JPG






IMG_0889.JPG

Mfanyabiashara eneo hilo la Mwambetogwa akihamisha bidhaa zake kukwepa shari eneo hilo ambalo limetangazwa kuwa ni eneo la hatari na FFU:


Picha na Francis Godwin Blog-Iringa
 
Hiyo itakuwa ni typing error, nadhani alimaanisha kabisa, n na b kwenye keyboard ziko jirani mkuu
 
Dalili ya mvua ni mawingu, hii ni dalili tosha kwamba nchi imemshinda jamaa. Na asiponagalia hawa makamanda/polisi watamharibia asimalize 5yrs na peoples power[pp] wakaandamana mpaka....kieleweke. Si wameshajenga immunity na hayo mabomu na risasi moto? Yaani hapo itakuwa ni noma, yaani mshike mshike. Itabidi icc ihamie hapa. Au mnasemaje washikaji?
 
IMG_0886.JPG

askari wa FFU mkoani Iringa wakiwa wametanda eneo la uwanja wa Mwembetogwa ambalo Chadema ilipanga kufanyia mkutano wake leo wa kitaifa

IMG_0885.JPG

Mkuu wa FFU mkoa wa Iringa afande Mnunka akiwa eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mkutano wa Chadema

IMG_0883.JPG


IMG_0889.JPG

Mfanyabiashara eneo hilo la Mwambetogwa akihamisha bidhaa zake kukwepa shari eneo hilo ambalo limetangazwa kuwa ni eneo la hatari na FFU

Picha kwa hisani ya blog ya Francis Godwin

Naipenda sana Tanzania nchi ya kudumisha Amani. Majeshi yake ya Ulinzi na Usalama wanafanya kazi waliyoajiriwa kuifanya kwa umakini sana.

Lakini wanapungukiwa kitu kimoja, nacho ni "Kutumia nguvu kama hii kupambana na Majambazi wanaotunyima usingizi wananchi Raia wa Tanzania"

Hawa FFU wangelikuwa makini katika kupambana na vitendo viovu vyote hususani Majambazi, na wangelikuwa wanafika mapema hivi wanapopata taarifa za Kiintelijensia kuwa kuna majambazi yanarusha Risasi sehemu fulani. Nji hii tungeliishi kama tupo Peponi Wallahi tena!!!!!



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Gari ya RPC na Afisa usalama mkoa wa Iringa wanazunguka kwa umakini na kwa taratibu nyuma ya msafara mrefu wa magari ya FFU hii ni hatari zaidi.
 
Back
Top Bottom