Ezekiel Wenje awasha moto Bungeni

Naunga mkono hoja; kama baba, huwezi kukemea tabia mbaya za mtoto ambazo na wewe unazo!!!!!!!!!!
 
Safi saaaana, Nami naunga mkono hoja
"Organisation culture in any organization is strongly influenced by the personality of the CEO (i.e. Ministers, Secretaries, Police Officers, etc). The subordinate do and behave the same as what CEO in the organisation do and behave"

Kwa hali hii nakubaliana na Wenje kuwa, ni lazima kwanza RUSHWA IKOMESHWE KUTOKA JUU na si kulalamikia POLISI WANAOPATA KIDOGO SANA.
 
duh ...... nchi hii sasa tunaoyeshwa kuwa tulifungwa vitambaa vyeusi machoni na kuwekwa pamba masikioni mwetu na sisi wenyewe hatukutaka kuvitoa vitambaa vyeusi na pamba

watanzania wenzangu ....... wamekuja wale walioamua kututoa vitambaa vyeusi machoni na pamba masikioni ili tuweze kuona na kusikia udhalimu wa serikali hii .... naomba tuwasikilize hawa waliojitoa muhanga na kuwapa moyo pia

ujasiri huu unaoonyeshwa na wabunge wachache ndiyo matumaini ya mtanzania kwa sasa
 
Leo Wanje kanifurahisha sana

Wanje kasema
hawezi kusema ni sahihi polisi kula rushwa pia hawezi kutumia nguvu na akili nyingi kupiga kelele kwa polisi wapunguze rushwa
Akaongeza wabunge wengi wa CCM wanawakandia polisi kwa kula rushwa ila wanasahau kuwa polisi wameamua kujimegea kilicho mbele yao kama vile mawaziri wanavyojimegea.

Akamaliza hivi :kama tunataka rushwa ikomeshwa ndani ya jeshi la polisi tuimalize kwanza kwenye baraza la mawaziri na wakuu wa idara vinginevyo tuwaache polisi waendelee hivyohivyo walivyo.

my take: ccm wasilinyooshee kidole jeshi la polisi kwa rushwa kwani na wao (ccm) NI MAFISADI WAKUBWA.

kwenye baraza la mawaziri hawaliiti ni rushwa, bali ufisadi.
kwa hiyo ni haki ya wabunge wa ccm kupiga vita rushwa ya polisi, kwani kwa upeo wao rushwa ni kiwango cha hela isiyozidi laki moja. na mawaziri wanajichotea kiwango kisichopungua bilioni, ambacho wao hawaiiti ni rushwa bali ufisadi, na wao hawapigi vita ufisadi zaidi ya rushwa
 
Ngumu sana hii,wanakula rushwa ya mamilioni then wanamkamata mtu aliepokea rushwa ya 20000 huu ni ujinga.peopleiz power
 
kuna muuza popconi hapa? naona kama vile movie ndo linaanza vile...au mbwa(magamba) wameshapotezwa na filimbi nyingi
 
Kikubwa kinachofurahisha ni kwamba muda mwingi Chadema wanatoa hoja za mateso na shida wanayopata wanainchi, Wakati Serikali na wabunge wa CCM vilevile wao ni kama wako mahakamani muda wote ni kukanusha yale ya CDM walichosema na kidogo mwisho wanaelezea shida za wanainchi ktk mtindo wa .."machozi ya Mamba"

CCM/Serikali wameingia ktk mtego ambao nafikiri kwa usingizi walio nao hawataona kamba imefungwa wapi

Chadema endeleeni hivyo hivyo Jino kwa jino kwani hamukwenda pale kutafuta wachumba wala posho, wengi wanakueleweni tofauti na wao wanavyotangazia umma

Naunga mkono!!:rapture:
 
mfano mdogo tu!!! tulikuwa tunahitaji samaki toka japan? sasa waliohusika mbona hawajakamatwa mara moja....nchi imeonza hii,inaitaji ukombozi wa kweli.hongera wapinzani kwa kusema ukweli....daima msema ukweli ni mpenzi wa mungu
 
Leo Wanje kanifurahisha sana

Wanje kasema
hawezi kusema ni sahihi polisi kula rushwa pia hawezi kutumia nguvu na akili nyingi kupiga kelele kwa polisi wapunguze rushwa
Akaongeza wabunge wengi wa CCM wanawakandia polisi kwa kula rushwa ila wanasahau kuwa polisi wameamua kujimegea kilicho mbele yao kama vile mawaziri wanavyojimegea.

Akamaliza hivi :kama tunataka rushwa ikomeshwa ndani ya jeshi la polisi tuimalize kwanza kwenye baraza la mawaziri na wakuu wa idara vinginevyo tuwaache polisi waendelee hivyohivyo walivyo.

my take: ccm wasilinyooshee kidole jeshi la polisi kwa rushwa kwani na wao (ccm) NI MAFISADI WAKUBWA.

Nitasema ukweli siku zote, unafiki kwangu mwiko. Chadema (Wenje) wako extremly right. Jairo wamemlinda wanawasumbua mapolisi. CCM acha unafiki wacha rushwa tawale. Suluhisho ni nguvu ya Umma.
 
Inahitajika mbinu mpya kuizuia cdm coz wanacho kisimamia ni haki na uhuru wa mtanzania wa chini na tena ni masikini,wanyonge na waliokata tamaa na maisha.peopleiz power.
 
Wenje kasema kweli. Kumbe rushwa na ufisadi ni sera ya CCM.

Shime CDM pigeni vita RUSHWA NA UFISADI
 
Walaaniwe wanaowanyanyasa wapinzani bungeni kwa kuulinda ufisadi wa wachache!wajinga mno
 
wakuu naomba kama kuna mtu alisikiliza mchango wa Werema aweke hapa nataka kujua alichangia nini maana nimesikia tetesi nataka kuzi-clear,

niombi jamani naomba kuwasilisha!
 
Nitasema ukweli siku zote, unafiki kwangu mwiko. Chadema (Wenje) wako extremly right. Jairo wamemlinda wanawasumbua mapolisi. CCM acha unafiki wacha rushwa tawale. Suluhisho ni nguvu ya Umma.

Mkuu hilo la Jairo nalo neno, let us wait and see...........................
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom