EYE SPY: Time to retire, Mzee Kingunge

"Kingunge: Tutaumaliza kabisa upinzani TZ" kwa pesa au ....maana wapinzani halisi wako kama wawili watatu tu mkiwamwagia mtama basi mnawamaliza kabisa
 
Na huyo alikua mshauri wa Rais masuala ya Siasa.Hebu angalia jinsi nchi hii ilivyo na watu wa ajabu.Pengine hili ndilo alilokua akimshauri Rais.

Alfred Lwakatare kamwambia huyu Anyamaze maanke anaongera kama vile amekurupushwa.Huku ni kuzeeka vibaya,si aachane na siasa tu.Kama kumuheshimu mtu ni kutokana na Age yake tu,basi mimi........

Anafikiria kuumaliza upinzani? Atakwisha yeye na chama chake kwanza! Hizi ndiyo zile siasa za kwenye sewage system hasa!
 
Kingunge ni mwanasiasa wa zamani inapaswa tumheshimu.

Tunaweza tusimpende mtu au mawazo yake lakini hoja zetu zisiwe za kumlenga yeye binafsi kutokana na umri, jinsia, imani au vitu kama hivyo. Hayo ni masuala binafsi


Waziri Kalala,
Ninapenda kukupongeza kwa kuwakumbusha wachangiaji wengine kuwa kitu muhimu ni kujadili hoja ya Mzee Kingunge na wala siyo kutoa maneno ya kejeli juu yake kwani hayasaidii lolote. Vilevile tukumbuke kuwa Mzee Kingunge ni mwanasiasa mkongwe na aliyebobea kati propaganda, kwahiyo wakati anaongea hayo anajua huo mzigo wa kulumbana anaupeleka wapi.


=ochu;278141]Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitahakikisha kinawashughulikia wapinzani na kuhakikisha wanaumaliza kabisa upinzani. Kingunge ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, aliyasema hayo mjini Dodoma wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi.

Kauli hiyo hapo juu nadhani ni kauli muhimu sio tu kwa wana-CCM bali hata kwa wapinzani, kwani kila upande unaoshindana hutarajia ushindi. Ni sahihi kwa Mzee Kingunge kuweka tambo za kisiasa kama hizo. Ni jukumu la wasio wanachama wa CCM kuweza kujijenga na kujiimarisha kukabiliana na changamoto hiyo ya CCM. Msikae hata siku moja kama CCM itasema itasaidia kuviimarsha vyama vya upinzani, that will be an ugly statement of the decade.

Kingunge alisema nguvu ya chama kwa sasa inaelekezwa kwa wapinzani lengo kuu likiwa ni kuwamaliza licha ya kuwa tayari chama chake kimeshafanikiwa. "Sasa hivi hakuna kitu na tumefanikiwa kwa sababu ya kuwaunganisha wanachama wetu na kuwa kitu kimoja na haki ndiyo inayowaunganisha na ndio maana tumefanikiwa," alisema mkongwe huyo.

Kwa wasio wanachama wa CCM hii pia ni kauli nyingine ambayo pia inatakiwa kuchukuliwa kama changamoto kwani kama vyama vya upinzani vitawaunganisha wanachama wao basi ni dhahiri kuwa vitapata mafanikio

Alisema iwapo kiongozi wa CCM atashindwa kupambana na upinzani, ni lazima uongozi wake utakuwa na dosari na hivyo atanyang'anywa madaraka. Akimzungumzia Ndejembi, alisema ni vyema viongozi wa CCM wakatambua kuwa CCM imetoka mbali kwa historia ndefu ili iendelee kuwapo, ni vyema wakajivunia viongozi waliopita na kuwaenzi.

Alisema pamoja na hilo, pia CCM inaamini kuwa kazi kubwa ya kiongozi ni kuunganisha watu anaowaongoza na si kutenganisha watu au kutafuta vikundi vyake na kama kiongozi wa CCM atafanya hivyo, huyo hafai kuongoza chama hicho. Kingunge aliwataka viongozi ndani ya chama hicho kuwa wavumilivu na wasikivu na kuzisikiliza jumuiya zote ni nini zinataka na si kulazimisha na kufanya vile ambavyo yeye anataka
.[/QUOTE]

Maneno ya Mzee Kingunge ni ya maana sana kwa kila mwanasiasa awe ni wa CCM au opposition. CCM watayachukuwa wayafanyie kazi na ninyi wapinzani pia myachukue kwani yatawasaidia sana. Asiyeona hilo, naomba atafakari kwa kina. Tujadili hoja za Kingunge.
 
Jamani huyu mzee simwombei mabaya ila bora tu apumzike milele.

Hana cha kuongea sasa zaidi ya kuleta vurugu za maneno na hiyo CCM kama vile ni yake.

Inawezekana pia akili zimeanza kumruka maana uzee mwingine unamjia mtu vibaya.

Jaribu kufika Mirembe hapo dodoma mara moja maana mkoa huo mara nyingi waenda, uangalie afya yako ya kiakili.
 
Dhamira ya Rais, ambaye ndiye mwenyekiti wa chama cha Kingunge, ni kutouua upinzania. At least hivyo ndivyo alivyosema wakati wa hotuba yake Bungeni Desemba 2005. Sasa kama chama chake kinadhamiria kuufuta upinzani, tuelewe nini; kwamba rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama kinachotaka kufuta upinzani, hakusema hayo kwa dhati ya moyo wake? Au kuna mapambano ya dnani ya CCM ambako limezaliwa kundi la akina Kingunge ambao wanataka kuua upinzani tofauti na dhamira ya rais?

MN, Tatizo la kiongozi aliyeshindwa kuthibiti walio chini yake ndiyo hilo. Kila mtu ndani ya CCM anaweza kuzungumza upupu wake kwenye hadhara hama kama upupu huo unapingana na mtazamo wa kiongozi wa CCM, lakini cha kushangaza hakuna yeyote anayewajibishwa! leo utasikia Makamba kazungumza upupu, kesho atakuwa Kingunge, kesho kutwa atakuwa RA na mtondogoo atakuwa spika (mjadala huu inabidi unisubiri nitoke safari yangu ya Marekani) au kutompa muda Ngeleja wa kuzungumzia Bungeni kuhusu Kiwira, hivi Rais angemtaka Sitta alipe swala la Kiwira ungeshindwa kweli kupatikana muda wa kuzungumzia Kiwira? Ndiyo chama kimeshika utamu! kinaendeshwa kienyeji, kifisadi maana hakina mwenyewe!
 
Tatizo la Kingunge siyo usocialism bali ni Usisiem(U-CCM).Ni U-CCM ndiyo unaomfanya awe hivyo.Lakini kama kweli angeweza kuelewa japo punje ndogo ya misingi mikuu ya socialism asingeweza kutetea mafisadi au kuzuia wabunge wanaohoji juu ya ubadhirifu wa mali ya umma.
Wembe.

Mkuu Wembe,

Tatizo la Kingunge siyo U CCM kama unavyosema. Haliwezi kuwa tatizo hilo kwa sababu lingekuwa limewaathiri wote waliomo humo. Usingepata mifano ya akina Kilango, au wewe mwenyewe usingesema kuwa anajaribu kuwazuia wanaohoji juu ya mafisadi. Inawezekana amepitwa na wakati or something, au fikra zake zimezeeka. Hataki kubadilika.
 
kingunge still believes in part supremacy. you can see the way he addresses those who are critique within the part. it is time for him to GO!!! if he likes CCM too much he has to revamp the party and not otherwise, i wish nyerere was alive
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom