Experiencing a very low internet speed?

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Wakuu sijui kama mmeshtukia kuwa Internet Service Providers kwa Tanzania speed imeshuka ghafla tangu Jumamosi (24/April/2010); mimi tatizo hili nilianza kulihisi na kubadilisha connections bila mafanikio.

Leo nimelazimika kuwasiliana na TTCL ambapo sikupata response yoyote, nikawasiliana na VodaCom wakani-hold mpaka nikajikuta nakata simu tu; Zantel nilipowasiliana nao wamenieleza hivi:

"We are very sorry for this, there is an outage on SEACOM since Saturday and we do expect this issue to be resolved today"

Nilipouliza kama ni kwao pekee wakasema ni kwa wote ambao wanatumia Fibre Cable ya SEACOM.

Sijui kama wakuu wengine mmekumbana na issue hii. TTCL kwangu ilikuwa ina-connect lakini hakuna response kwenye browser.
 
mimi kwangu ilikatika kabisa siku ya jumamosi na nilipowasiliana na vodacom wakanieleza kuwa wapo kwenye matengenezo, baada ya muda fulani ilirudi lakini speed sio kama zamani....asante mkuu kwa kutujulisha kinachoendelea
 
Sikuwa kazini jMOSI, lakini kwangu mwendo mdundo, no change...THANKS NodMarie, sijui hawa wanachukulia wapi!
 
Hata mimi nimeshitukia hii issue ya mtandao, Kwa maelezo hayo ya Maxence naamini ndivyo ilivyo kwa sababu hata mimi toka Ijumaa kama sikosei hadi hivi sasa ninapotuma post hii mtandao uko veeeeeeeeeeeeeeeeeeery slow na kuna wakati haupatikani kabisa hasa jana ndio usiseme, mimi natumia ya Vodacom.

Mkuu tunashukukuru kwa kutujulisha hilo maana nilishaanza kuwa na wasiwasi.
 
Hata mimi nimeshitukia hii issue ya mtandao, Kwa maelezo hayo ya Maxence naamini ndivyo ilivyo kwa sababu hata mimi toka Ijumaa kama sikosei hadi hivi sasa ninapotuma post hii mtandao uko veeeeeeeeeeeeeeeeeeery slow na kuna wakati haupatikani kabisa hasa jana ndio usiseme, mimi natumia ya Vodacom.

Mkuu tunashukukuru kwa kutujulisha hilo maana nilishaanza kuwa na wasiwasi.
Mkuu GM,

Mimi mwanzo nilihisi kuna kitu nimechemsha kwenye connections zangu. Lakini nikajaribu hata hizi wireless modem za Zain na VodaCom nikakuta mambo yaleyale.

Ila ukipiga Customer Service wanakuweka mpaka una-give up. Baadae majibu ya Zantel ndio yalinifanya nielewe kuwa issue sio kwangu na kuwa sasa hawa SEACOM wanaanza kutuaribia raha ya surfing.

Mkuu PJ, hao NodMarie itakuwa hawajajiunga na SEACOM na possibly internet speed yako always ni ndogo tu :smash:
 
Hata mimi mpaka leo Zantel iko chini mpaka sasa,na inakata,sasa hawajamaa si ilitakiwa watuhabarishe huku ndio kuwajari wateja kweli,lah kazi kweli TZ hata zingekuja kampuni kutoka wapi zitabadilika na kuwa za uswahili mtupu,asante Max kwa kutushtua,hata TCRA nao ni bomu sijui kazi yao nini na huyo profesa wao,hii ni aibu
 
Guys,

Maelezo aliyoyapata Mheshimiwa Max Melo ni ya ukweli.....

Kuna matengenezo makubwa yanaelendelea kwenye gateway duct kubwa saana inayozigawa worlwide pale suezi canal....hivyo SEACOM kama wateja wa hiyo wakathirika na matengenezo hayo ya siku tatu....

Hapa Bongo, ISP karibu wote walikuwa ni wateja wa SEACOM hivyo outage ya SEACOM ni outage yao pia.....Zain wanatumia alternative route kwa kipindi hiki,wateja wanapata low connection iliyokuwepo kabla ya seacom. zantel wanaweza kuwa hawana connection kabisa kwa kuwa wana ubia na SEACOM hivyo kudhani hawawezi kuathiriwa kwa vyovyote vile....

Lakini sasa wamejifunza hope watakuwa na alternative route kwa baadaye though inacost sana lazima uwe na commitment kwa wateja kwelikweli kwa kuwa bado data service hailipi sana kwa bongo especially kwa mobile operators.

Siku tatu nzima ni Jumamosi, Jumapili na Jumatatu leo..... tegemea mambo kurudia kama zamani by tomorrow kama zoezi lao litafanikiwa 100% kama walivyopanga.

Thanks.
 
Hata mimi mpaka leo Zantel iko chini mpaka sasa,na inakata,sasa hawajamaa si ilitakiwa watuhabarishe huku ndio kuwajari wateja kweli,lah kazi kweli TZ hata zingekuja kampuni kutoka wapi zitabadilika na kuwa za uswahili mtupu,asante Max kwa kutushtua,hata TCRA nao ni bomu sijui kazi yao nini na huyo profesa wao,hii ni aibu

Kwa hilo la zantel kiukweli jamaa wanatujali wateja wake, In person kwenye modem yangu ya Zantel nilitumiwa message hii hapa chini,

"Name:
Number: 107
Content:
Dear Customer owing to the expected fiber cable outage you will experience degraded Internet Service with effect from tomorrow April 24th to Monday April 26.
Time: 24/04/2010 09:12:04
Text message priority: Normal"


Kimsingi baada ya kupata hii message niliridhika na nikaona kuwa kiukweli wananijali, Lakini hao maprovider wengine wao wanchojali ni pesa mteja hawako nae time na hata ukipiga simu kwao ni kama unapoteza muda na kujichoresha kwani watakusikiliza then ukimaliza nao wamemaliza. Kiufupi quality service regulations and standards provision is still poor and no one is there to question about.
Kama kuna provider ambaye haku escalate sms kwa wateja wake on time on regard to that problem inahitajika alipie faini...

TCRA wanaweza wakawawajibisha na inawezekana kabisa, ila kwasababu nchi yetu ni ya mambumbumbu wanaohangaikia lunch na dinner, that problem will be overlooked and mambo yataendelea.
 
Asante Max, mimi naconect through enteprise server kupitia voda, huwa faster kuliko moderm zote nilizokuwa natumia, nilipoona iko slow nilidhani ni backbery maana zinaleta vimeo vya ajabu ajabu. Thanks for info.
 
Mkuu Max, Shukrani sana kwa taarifa hii, toka jumamosi sijatumia computer yangu kabisa nilikuwa na surf kupitia simu yangu na sikuweza kugundua tatizo ili, leo nimeingia officen ambako ISP wetu ni SimbaNet yaani ni balaaa! speed iko slow sana kupita kiasi,yaani file la kb 250 nimetumia dakika 7 kulishusha.
 
Faulty fibre cable affects internet in Kenya

NAIROBI, Kenya
Apr 24, 2010
Capital FM


Internet users in Kenya are likely to experience outages between Saturday and Monday due to a fault to a submarine cable in the Mediterranean Sea close to Alexandria in Egypt.

Fibre optic cable provider SEACOM says the underwater cable SEA ME WE 4 is what they use to connect East Africa with London via India.

A statement from the company says engineers were to repair the line between Saturday and Monday which would lead to disconnections for all Internet Service Providers (ISPs) using the SEACOM and TEAMs cables in the region.

“The ship needs to bring up the cable to replace the damaged portion, make the splice and put it back in the water under the sea bed. Traffic will then be restored as soon as the cable is spliced. Unfortunately it implies that for a short time they (engineers) will have to shut the power down on the cable system,” read the statement in part.

The East Africa Marine System (TEAMS) which is partially owned by the government uses the same cable to connect with London via Fujairah.

Local ISPs will be forced to revert to satellite means, which will mean reduced connectivity speeds for clients.

“We estimate that the duration of the repair itself will not take more than five and six hours. it is however unpredictable to have a precise chronology of th duration of the sequence,” added the SEACOM statement.

The company, which beat its competitors TEAMS and EASSy to land its fibre optic cable in Kenya last year, says it is seeking another solution that involves the crossing of Egypt via the Red Sea which should be completed by June.


Naona maumivu sio kwa Tz pekee, poleni mnaoathirika na balaa hili
 
mkuu upo juu niliona hili tatizo ila sikuelewa kabisa connection ilikuwepo ila ukifungua page balaa inatoa error in connection
 
Internet Cafe nyingi hawatoi huduma ya internet tangu juzi
 
2cen0qu.jpg


Internet Service Providers (ISPs) connected to the SEACOM marine submarine cables (SWM4) are experiencing an internet outage across African, Asia and Middle East.
The break down occurred on April 14 after the cable was damaged by a ship but repairs did not commence until April 25 and are scheduled to go on to until, Friday, April 30 2010.

SEACOM is the largest fibre optic cable carrier along the Indian coast and had since its launch last year steadily raised internet speeds and brought a significant drop in prices in the region.

Now SEACOM’s breakdown has been carried over from the different ISPs that subscribe to their bandwidth unto internet customers/users. Some are experiencing complete breakdowns, cut bandwidth or slower speeds.

Some Warid Telecom customers have already experienced slight but significant drops in internet speeds which had become a rarity in recent times after the landing of the fiber optic cable. The speeds have also reportedly dropped from 512 Mbps that the Telecom was offering to about half.

Hans Haerdtle, CEO of Infocom one of the largest ISPs in the country told The Observer on Tuesday that “There are slight reductions in capacity which has to do with how certain clients [customers] are being routed [connected]”

He added that “A client with general internet access should not experience any difference [following the breakdown]. Clients with complex and dedicated connections like private circuits or VPN [virtual private network] there might be a reduction in capacity. It depends entirely on what kind of connectivity a client has”

He said that Infocom has now re-routed its internet traffic through an alternative route of TEAMS another sub –marine cable carrier, that runs from Fujairah, UAE to Singapore although with a smaller bandwidth capacity.

A statement from Uganda Telecom notes that the company has purchased an extra alternative bandwidth that “has brought our operations back to 100%”.

The statement further notes that incase a need arises, Uganda Telecom is still in position to keep their customers connected through the WiMAX - a wireless broadband connection platform.

But more worrying is that SEACOM indicates that it’s not in control of the situation and “that the repair window may be extended to Friday 30 April 2010 for reasons unknown to SEACOM at this point”.


The telco said that the 20,000 km Sea-Me-We 4 cable, which runs from France to Singapore, connecting South East Asia to Europe via the Indian Sub Continent and Middle East, suffered a problem somewhere between Alexandria and Marseilles.

A spokesman for Etisalat said that the groups most affected would be high bandwidth users, including gamers, users of video sharing website Youtube and filesharers using peer to peer sites.

Etisalat said it is working with "the administration, partners and concerned operators for urgent repair works to ensure earliest possible restoration of the cables and internet service". In the mean time, traffic is being re-routed and priority given to business users.
 
Poleni mliojiunga nao...You guys have to be patient, hawa jamaa wanafanya kazi, hawana longolongo
 
sisi wa TTCL mbona tunakoma!!! sijaingia JF siku nne, ndy leo asbh naona kidooogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom