Expatriates hawana sifa

Mimi naunga mkono yote yalosemwa hapo juu, ila nakumbusha kuwa "SIO SIFA ZINAZOFANYA KAZI". Na hili ndilo tatizo letu, tunataka nafasi kwa sababu tuna "sifa", wakati kazi zenyewe kufanya kila siku ni "excuses tu". Hivi unadhani nani yuko tayari kumlipa mtu mwenye sifa asiyefanya kazi? Tubadilike, halafu utaona kama ataagizwa mtu nje !!!!

mi jamaa sikjakuelewa kabisa, make mjadala ni kuhusu hao expertriates wasiojua lolote, cha msingi mimi nimefanya kazi bongo na nafahamu kuhusu huu ukweli, tuna maex pertriates ambao ni ishu kabisa na kama sio ugomvi, utakuta jamaa alikotoka alikuwa mlinzi wa kasino and then analetwa bongo kuwa meneja wa tuseme labda kitengo cha metallurgy, so look the difference, au anakuwa snr supervisor labda wa production kwenye mine, so mtu kama huyu si maajabu hayo, badala ya kufanya kazi unakuta ni mtu wa mambo ya umbea kwa sababu hajui anachofanya.Kuna mfano mzuri tu, pale Geita gold mine kulikwahi kutokea miaka ya karibuni tu, jamaa alikuwa (by name Jordan) alikuwa Production meneja wakati hizo qualifications hana, elimu yake ni grade 12 ambay ni sawa na form six/four kwa hapo home Tz, wakati huo kuna watanzania lukuki wanamasters in Mining engineering, au honors degrees in the same profession, so hili linatakiwa kuangaliwa sana.
 
Mishahara wanayolipwa hawa 'vihiyo' hupelekwa nje ktk nchi zao, ni uporaji wa ki-haina haina!. Ni vema viongozi wetu watunge sera zinazolinda ajira kwa ajili ya wazalendo. Wazalendo hawana pa kwenda. Hawa watanzania wa kawaida ndio mtaji wa taifa hili. Mbona kwenye uchaguzi wanatunyenyekea saaaaaaaana.
 
Sasa hao wenye "sifa" wanafanya nini kukomesha upuuzi huo? Kama kweli wana sifa kwa nini hawa -argue their cases to their employers? Jibu ni kuwa waoga!!!! na hapo ndo unaona mashaka ya hizo "sifa". Uhamiaji si kuna watu wenye "sifa" za kutambua vihiyo au la ili watoe kibali cha kazi, sasa inakuaje wanawapa vibali? Sasa watu wana "sifa " gani zisizokuwa za msaada kwao ? Kila siku ni kulalamika tu? . Ninavyowajua "wakoloni (ngozi nyeupe)", hata kama wana ubaguzi, lakini kama "mtu ana sifa na ku-deliver" watamuheshimu !!!
 
Kwa hiyo case ya wahasibu, ina maana hatuna wahasibu nchini mpaka tunaleta wahasibu kutoka India?

Usiseme hivyo ndugu yangu tembelea EXIM Bank utaona, hao wanawaita expatriates ni uozo mtupu. Anakuja mhindi eti expatriate anakuwa oriented na mbongo halafu akisha shika kasi eti anakuwa bosi wa huyo huyo aliyemfanyia orientation. Hawa wahindi ni wezi wanataka watu wao wawasaidie kupindisha mahesabu na kuhalalisha wizi wanaoufanya!
 
Kwa hiyo case ya wahasibu, ina maana hatuna wahasibu nchini mpaka tunaleta wahasibu kutoka India?

Mimi limenikuta hili...nikiwa ACPA with MBA nimefanya kazi sehemu nyingi kwenye Finances...pahala fulani nikaletewa boss mzungu ana technician qualifications za ACCA basi anadai ana ACCA...Nikasema poa tufanye kazi...yeye kazi yake ku-probe na kuatafuta makosa kwenye kazi zangu...kwa vile tunatumia ma EXCEL muda mwing basi mimi nikawa namuwekea maformula magumu anashindwa kuona ndani...akawa analalama....ooh this guy is complicating his work for no reason......nikatmka zangu an yeye kazi ikamshinda bila mimi akahamishiwa Uganda nako kachemsha nasikia.....inasikitisha sana...halafu malipo yao utalia....interntaional salaries($10,000+ pm),watoto IST,gari,nyumba masaki etc...kazi zote tunafanya waTZ tena wengine kwa kukenua meno ati 'boss wangu mzungu'....Immigration na Masha wao(a lawyer that is) wako busy Nyamagana
 
KARIBUNI KWENYE MA-NGOs YA KIMAREKANI NDIO MUONE MAMBO!!!!

WANAKUJA INTERNS HALAFU WANAITWA EXPATRIATE... HIVI ILE SHERIA YA IDADI YA MA-TX IKO ACTIVE?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom