Executive Solutions ndiyo inahusishwa na sakata la Jairo? - Marealle akanusha!

I will be very suprised kama sio ES. Core business ya hawa ni government relations'. With time details zitaibuka tu hapa.

ni kampuni pekee TZ ambayo core business yake kwenye mambo ya pr ni serikali? Makampuni mengine makubwa ni yapi?
 
Yaani, Umuulize Mtanzania kwanini alienda Dodoma? Tangu lini tunawauliza watu wanakokwenda? Hivi Dodoma nzima mtu pekee aliyekuweko Dodoma wakati wa tukio hili na anahusiana na Public Relations ni Marealle tu?

Hapo kwenye bold, hii sio maana yangu na hata ww unajua, labda unataka kupotosha makusudi. Kuhusiana na hili, mimi nilikuwa nataka kuonyesha circumstantial evidence na sio kumhukumu. Samahani, lakini naona kama uko desperate kumtetea huyu mtu. Labda unamfahamu vizuri na huamini kama anahusika. Nakufahamu kama mtu anaye-argue kwa pointi zilizoshiba, ila kwa point yako niliyoichallenge awali, ni dhaifu.

Yaani kwakuwa hakuna aliyewaambia TAKUKURU, basi hicho kitu hakikufanyika? TAKUKURU ni yetu sisi wanyonge, haina uwezo wa kukamata wakubwa.Pia ktk mazingira ya lobbying, ushahidi (hard evidence) unatoka wapi? Narudia tena, ni ngumu kwa ES kuwa cleared kwa sasa, mpaka hapo uchunguzi huru utakapofanyika. Kwani Murdoch 'alijua' wanachofanya waandishi wake?
 
Hapo kwenye bold, hii sio maana yangu na hata ww unajua, labda unataka kupotosha makusudi. Kuhusiana na hili, mimi nilikuwa nataka kuonyesha circumstantial evidence na sio kumhukumu. Samahani, lakini naona kama uko desperate kumtetea huyu mtu. Labda unamfahamu vizuri na huamini kama anahusika. Nakufahamu kama mtu anaye-argue kwa pointi zilizoshiba, ila kwa point yako niliyoichallenge awali, ni dhaifu.

Pointi yangu ni kuwa hatuwezi kwenda kumuuliza Marealle bila sababu! Kama Mtanzania anayo haki ya kuwa Dodoma wakati wowote na kujishughulisha na shughuli zake za kipato. Ndio maana ninaamini kama kuna kitu kimetokea kinyume cha sheria tuanze na kuwataja hao waliopokea au kama kuna mtu anayejua waliotoa awataje - so far hakuna mtu ambaye amesema kamuona nani akitoa nini kwa nani. NONE.

Yaani kwakuwa hakuna aliyewaambia TAKUKURU, basi hicho kitu hakikufanyika? TAKUKURU ni yetu sisi wanyonge, haina uwezo wa kukamata wakubwa.Pia ktk mazingira ya lobbying, ushahidi (hard evidence) unatoka wapi?
Sasa kama "hard evidence" hakuna, kwanini ES inashukiwa na siyo kampuni nyingine? Lazima kutakuwa na sababu siyo - sasa kusema kuwa Marealle alikuwa Dodoma - siyo sababu, think about it.

Narudia tena, ni ngumu kwa ES kuwa cleared kwa sasa, mpaka hapo uchunguzi huru utakapofanyika. Kwani Murdoch 'alijua' wanachofanya waandishi wake?

Well, kinachotuhumiwa ni ES au ni baadhi ya watu wake. Murdoch kampuni yake imekubali na wamewajibika, Marealle kama CEO kasema hakuna kitu kama hicho - sasa ni jukumu la watu wengine kuonesha kuwa Marealle kasema uongo, kuwa alikuwa anajua kinachotokea na kwamba kuna makubaliano kati ya kampuni yake na hao kina Jairo.

Labda nikuulize, kama hadi hivi sasa hakuna ushahidi mzito wa kujua nani kafanya nini, ni kitu gani kinakufanya ushuku ES kuhusika na kwamba kwa sasa hivi haiwezi kuwa "cleared"? Why suspecting ES na siyo kampuni nyingine?
 
Pointi yangu ni kuwa hatuwezi kwenda kumuuliza Marealle bila sababu! Kama Mtanzania anayo haki ya kuwa Dodoma wakati wowote na kujishughulisha na shughuli zake za kipato. Ndio maana ninaamini kama kuna kitu kimetokea kinyume cha sheria tuanze na kuwataja hao waliopokea au kama kuna mtu anayejua waliotoa awataje - so far hakuna mtu ambaye amesema kamuona nani akitoa nini kwa nani. NONE.

Yaani kwakuwa hakuna aliyewaambia TAKUKURU, basi hicho kitu hakikufanyika? TAKUKURU ni yetu sisi wanyonge, haina uwezo wa kukamata wakubwa.Pia ktk mazingira ya lobbying, ushahidi (hard evidence) unatoka wapi?

Sasa kama "hard evidence" hakuna, kwanini ES inashukiwa na siyo kampuni nyingine? Lazima kutakuwa na sababu siyo - sasa kusema kuwa Marealle alikuwa Dodoma - siyo sababu, think about it.

Well, kinachotuhumiwa ni ES au ni baadhi ya watu wake. Murdoch kampuni yake imekubali na wamewajibika, Marealle kama CEO kasema hakuna kitu kama hicho - sasa ni jukumu la watu wengine kuonesha kuwa Marealle kasema uongo, kuwa alikuwa anajua kinachotokea na kwamba kuna makubaliano kati ya kampuni yake na hao kina Jairo.

Labda nikuulize, kama hadi hivi sasa hakuna ushahidi mzito wa kujua nani kafanya nini, ni kitu gani kinakufanya ushuku ES kuhusika na kwamba kwa sasa hivi haiwezi kuwa "cleared"? Why suspecting ES na siyo kampuni nyingine?

Sawa Mwanakijiji, I rest my case.
 
MKJJ na wewe mbona unatoa povu hivyo kumtetea?Ama ni harakati za kuutafuta ukweli?I hope thats the case.
 
MKJJ na wewe mbona unatoa povu hivyo kumtetea?Ama ni harakati za kuutafuta ukweli?I hope thats the case.

Siku moja nilipita makutano ya Uhuru na Msimbazi - kulikuwa na duka la electronics; mostly used - nimeshuka tu kwenye daladala nikakuta watu wanampiga kibaka mmoja. Watu tulioshuka nao kwenye daladala na wakaanza kurusha ngumi au jiwe kumpiga. Na wapita njia wengine wanapita haraka na kumpiga na makonda wa kwenye vipanya waliruka mara moja na kupiga ngumi mbili tatu na kuondoka. Nilimuuliza mtu mmoja - kaiba nini? akasema "sijui"; nikauliza nani aliyeibiwa "sijui", sasa unampigia nini "ni kibaka!" Umejuaje ni "kibaka", si "watu wanampiga?".. by that time police toka Msimbazi walikuwa wameshafika, jamaa damu inamwagika na bila shaka mifupa kadhaa imevunjika.

Unajua kwanini alipigwa?
 
Sooth: Kuhusiana na hili, mimi nilikuwa nataka kuonyesha circumstantial evidence na sio kumhukumu. Samahani, lakini naona kama uko desperate kumtetea huyu mtu. Labda unamfahamu vizuri na huamini kama anahusika.
Yaani kwakuwa hakuna aliyewaambia TAKUKURU, basi hicho kitu hakikufanyika? TAKUKURU ni yetu sisi wanyonge, haina uwezo wa kukamata wakubwa.Pia ktk mazingira ya lobbying, ushahidi (hard evidence) unatoka wapi? Narudia tena, ni ngumu kwa ES kuwa cleared kwa sasa, mpaka hapo uchunguzi huru utakapofanyika
Sooth circumstantial evidence haziwezi kumhukumu mtu bali hutumika kushadidia ushahidi uliopatikana.Kwa mfano kuwepo kwako eneo la tukio si lazima kuwe ni ushahidi wa wewe kuhusika na tukio hadi pale tukio hilo litapokuhusisha na uwepo wako.

Hapo mwisho umemaliza vizuri sana kuwa 'hadi uchunguzi huru utakapofanyika'. Nakubaliana na wewe kabisa, nisipokubaliana nawe ni pale uliposema 'ni ngumu kwa ES kuwa cleared kwa sasa' mimi pia nasema ni ngumu kumtuhumu ES kwa sasa.

Kuna kitu kinaitwa natural justice, yaani kumpa nafasi kila mtu kusikika. Mahojiano ni sehemu nzuri sana ya kumsafisha au kumtia mtu hatiani kwasababu kuna record. Itakapotokea ES ikatajwa vinginevyo tutavuta uzi na kumuuliza Marealle,je atameza matapishi yake? Hiyo itatupa circumstantial evidence nyingine ya kauli yake mwenyewe pamoja na uwepo wake Dom.

Kuna aina ya uandishi inayomtega mtu. Kule US kuna bloga mmoja alizusha habari kuhusu mama Shely shrod(kama jina ni sawa) aliyetuhumiwa kutoa maneno ya kibaguzi akiwa mkuu wa idara ya kilimo. Waandishi wakampa bloga enough airtime ya kutoa hoja zake, lakini walikuwa na mkanda wa video wenye ukweli. Baada ya Obama kumfukuza kazi mkanda ukawekwa, ilikuwa ni aibu kwa Bloga maarufu wa republican, chama chake na Rais Obama. Investigative journalism inatoa nafasi kwa ukweli kutamalaki kwa njia mbali mbali.

Sidhani PCCB wana maadili ya kumkamata mtu wa Jairo calibre,historia inanitetea. Kinachoshangaza Shelukindo ametoa barua kama ushahidi kwanini yasifunguliwe mashtaka na ikidhirika vinginevyo shelukindo awajibike? Kwanini katibu mkuu kiongozi ashughulike na kosa la madai ya uhalifu na si vyombo vya dola? Hoja ni kuwa zinatafutwa mbinu za kuua hii issue kisiasa, na ndipo ninakuwa na wasi wasi kuwa kuna kundi kubwa la wanene wanajua kila kilichofanyika. Kwa vile kuna kundi kubwa la wazito itakuwa ni ngumu sana kujua akina nani wamehusika kuandaa, kupokea au kugawa pesa. Nikifika hapo nasema ES wabaki kuwa wahisiwa. Wao ni maua na hadi tujue mti na mizizi yake wanabaki kuwa wahisiwa.

Wanabaki kuwa wahisiwa kama Chenge ambaye circumstantial evidence beyond reasonable doubt zina mu implicate na BAE na bado anabaki kuwa huru hadi sheria itakapomthibitisha vinginevyo.

Ukweli utajulikana tutakapojua tumejikwaa wapi na sio tumeangukia wapi, hadi wakati huo mtu au watu wanabaki kuwa hawana hatia hadi itakapothibitishwa na vyombo vya sheria. Je sisi ni vyombo vya sheria kuanza kumtuhumu mtu au watu? Je kuna ubaya kusikia upande wa pili wa shilingi? Je mtu akisema Sooth alionekana Dodoma akiwa na brief case ya mbunge wa jimbo lake ilikuwa na JAIRO,inatosha sisi kuamini bila kumsikiliza Sooth?
Sina imani na vyombo vyetu hasa kwenye rushwa kubwa, lakini ndivyo vilivyopo hadi tutakapoamua kufungia kibebwa katiba mpya.
 
Mtatoka mapovu ya vinywa buree kwa vitu ambavyo vimepangwa... Jamani nani asiyejua Shelukindo kambi ya magam,ba na sasa wanataka kummaliza JK na marafiki zake? Hivi ni vita vya ndani ya CCM na JK alifanya koda kubwa sana kufanya usuluhisho baina ya Magamba na wapiganaji wa CCJ..
hili kundi la magamba wameanza na Jairo (mshikaji wa JK) ambaye kapumzishwa tu kwa muda na atarudi kazini..Membe is next kisha watawamaliza mmoja mmoja hadi JK amebakia hana mtu lakini kwa kiburi cha JK kazi hii tuiache kama ilivyo maana fahari wawili wakigombana nyasi ndio huumia na kama mnakumbuka vita hivi havikuanza jana... na hakika sisi ndio tunazidi kuumia siku hadi siku hakuna linalofanyika zaidi ya kuhujumiwa..

Toka Lowassa ameondoka kama Waziri mkuu, JK kashindwa kufanya lolote na sidhani kama kuna mtu anaweza kunambia mradi hata mmoja mpya alokuja nao.. Siku zote maugonvi tuuu, yeye akiruka majuu kuvinjari kuepa kushiriki toka Richmond maadam asishirikishwe directly, na hakika hata ktk swala la kumweka Kaimu katibu mkuu hamuoni kaa ni vichekesho ati Naibu katibu mkuu ndiye anatangaza jina la mteuliwa badala ya JK mwenyewe...

Hivyo hii sio vita yetu kabisa, mimi nataka nyote kina mwanakijiji, na wengine wooote wekeni nguvu yenu ktk kuhakikisha JK analazimika kufanya maamuzi magumu... tuzungumzie shida zetu hadi akereke na wabunge tusiwape pumzi kabisa na hizi hadithi za rushwa hali rushwa hiyo ilielekezwa kwao. Mbona wasisubiri hadi fedha hizo zitoke kisha ndio wamwage mboga?..Harufu pekee haiwezi kutupa ushahidi wowote zaidi ya kupotosha mada kubwa - Kwa nini hatuna Umeme?..
 
watampata vipi Aggrey bila kuwapata waliopookea?
Point inajieleza vizuri tu ''iwapo serikali ina nia ya dhati'',Beatrice ana barua, Beatrice anasema alifuatwa na watu, kwanin serikali isianze na Beatrice awaambie anayoyajua?Au ndo yaleyale ya Chikawe kwamba mwenye ushahidi unaomhusisha Chenge na Rada aende mahakamani?
 
Wakuu,

Mimi naamini kuwa lazima pesa iliyo kwenye account ya serikali itoke kwa dokezo, voucher na baadaye hundi iandikwe kwa anayelipwa kukiwa na viambatanisho kama vile invoice kuthibitisha malipo husika.

Kwa hili la Jairo itakuwa imefanyika hivyo hivyo. Kwa vile ES ni kampuni kubwa ya biashara kwa vyovyote huwa inadeal na serikali vile vile. Ninachokiona mimi ni kuwa ES waliambiwa waandike Invoice ya madai kuwa wame supply au wametoa huduma fulani wizarani. Then inapita kwenye mlolongo wa kawaida hadi hundi inaandikwa kwa jina la ES & co.

Kinachofuata ni Aggrey au signatory yeyote/wowote kuandika hundi yao (ES) kwenda kudraw cash, na walengwa kupelekewa au kupita pale kuchukua bahasha zao zikiwa na cash. Ndicho kitakachokuwa kimefanyika hata kama si kupitia ES, lakini lazima kampuni fulani ilihusishwa.
 
Siku moja nilipita makutano ya Uhuru na Msimbazi - kulikuwa na duka la electronics; mostly used - nimeshuka tu kwenye daladala nikakuta watu wanampiga kibaka mmoja. Watu tulioshuka nao kwenye daladala na wakaanza kurusha ngumi au jiwe kumpiga. Na wapita njia wengine wanapita haraka na kumpiga na makonda wa kwenye vipanya waliruka mara moja na kupiga ngumi mbili tatu na kuondoka. Nilimuuliza mtu mmoja - kaiba nini? akasema "sijui"; nikauliza nani aliyeibiwa "sijui", sasa unampigia nini "ni kibaka!" Umejuaje ni "kibaka", si "watu wanampiga?".. by that time police toka Msimbazi walikuwa wameshafika, jamaa damu inamwagika na bila shaka mifupa kadhaa imevunjika.

Unajua kwanini alipigwa?

Shida kubwa iliyyopo hapa JF ni baadhi ya watu kupenda kuandika hata kwenye vitu ambavyo hawana facts navyo- matokeo yake unaweza kujikuta unashabikia hoja zilizoanzishwa makusudi kwa lengo la kumalizana kisiasa/kibiashara, minong'ono kwenye uchunguzi wowote ni mizuri ili kusaidia wachunguzi lakini ikifika mahali watu wana-conclude inatia shaka sana. Ni vizuri kama anavyoshauri MJ kama yupo mwenye ushahidi aseme, kama si hivyo tuamini kwamba ES hawahusiki hadi hapo uchunguzi utakapothibitisha tofauti
 
Siku moja nilipita makutano ya Uhuru na Msimbazi - kulikuwa na duka la electronics; mostly used - nimeshuka tu kwenye daladala nikakuta watu wanampiga kibaka mmoja. Watu tulioshuka nao kwenye daladala na wakaanza kurusha ngumi au jiwe kumpiga. Na wapita njia wengine wanapita haraka na kumpiga na makonda wa kwenye vipanya waliruka mara moja na kupiga ngumi mbili tatu na kuondoka. Nilimuuliza mtu mmoja - kaiba nini? akasema "sijui"; nikauliza nani aliyeibiwa "sijui", sasa unampigia nini "ni kibaka!" Umejuaje ni "kibaka", si "watu wanampiga?".. by that time police toka Msimbazi walikuwa wameshafika, jamaa damu inamwagika na bila shaka mifupa kadhaa imevunjika. Unajua kwanini alipigwa?
kwa hiyo MMM unataka kujua kwanini wanamtaja marealle kwenye kesi ya jairo..
 
kwa hiyo MMM unataka kujua kwanini wanamtaja marealle kwenye kesi ya jairo..

In a sense yes, kwa sababu yeye mwenyewe kashesema hahusiki wala kampuni yake haihusiki. Sasa angalatu - the closest thing - ni kwamba yatajwa majina ya wafanyakazi wake ambao walionekana wakitoa hizo rushwa kwa Wabunge, au watajwe wabunge waliopokea pesa toka kwa Marealle au watu wa ES. Sidhani kama hili ni gumu sana hivyo, hasa ukizingatia uwezo wa wana JF kujua. Hadi hivi sasa ukiondoa mimi kuitaka ES hadharani, hakuna mtu mwingine yeyote mwenye taarifa kinyume na hizi. NONE.
 
Mi huyu kijana siwezi kumtetea kabisa lakini honestly I smell a rat. Kuna possibility zifuatazo:
1. Anahusika lakini ame-preempt kwa denial na baadae ukweli ukijulikana basi ataaibika (hakuna siri ya watu 2)
2. Hahusiki na jina lake linatajwa kutokana na shughuli zake za kufanya kazi ya ku-lobby na masuala ya 'government relations' na PR yaani amewahi kufanya similar jobs (he is guilty of similar crimes but not this particular case)
3. Hahusiki kabisa na ni wivu za kibiashara kwani anafanya kazi nzuri (na safi?) ya PR na hivyo kuwapa wakati mgumu washindani wake ambao hutumia njia hizi za rushwa
4. Hahusiki ila watu wanaohusika makusudi wame-mislead umma ili wasishtukiwe na tutumie muda mrefu kumjadili mtu na kampuni nyingine badala ya focusing on the issue at hand and other possibilities - kitaalam to throw us 'off scent'
Kama kuna possibility zingine mtanisadia.

Ila in conclusion naona kama possibility ya kutohusika ni kubwa zaidi na inaonekana there is more to this story than we think. Tusiwe wavivu wa kufikiri na kupokea accusations ambazo hatuhujui nani kazi-initiate...
Mi nauliza:
1. Nani alianza kumtaja Marealle na Exectuive Solutions kama waliohusika?
2. Kuna evidence yoyote ya document au nyingineyo inayomhusisha Marealle na ES katika kesi hii?
3. 'Show me the money' - je pesa husika kutoka wizarani imeelekea wapi? Nadhani if we follow the money we get answers.

Otherwise mi nashauri badala ya kumjadili Marealle na ES - let's go back to the drawing board and follow the money.

In a sense yes, kwa sababu yeye mwenyewe kashesema hahusiki wala kampuni yake haihusiki. Sasa angalatu - the closest thing - ni kwamba yatajwa majina ya wafanyakazi wake ambao walionekana wakitoa hizo rushwa kwa Wabunge, au watajwe wabunge waliopokea pesa toka kwa Marealle au watu wa ES. Sidhani kama hili ni gumu sana hivyo, hasa ukizingatia uwezo wa wana JF kujua. Hadi hivi sasa ukiondoa mimi kuitaka ES hadharani, hakuna mtu mwingine yeyote mwenye taarifa kinyume na hizi. NONE.
 
Mimi kichwa changu hakisumbuliwi na ES wala Marealle, kama nao wamo wamo tu. La msingi kwangu tunatafuta mwisho wa kamba wakati ncha tayari tunayo, ni Kiasi cha kukamata kamba na kwenda nayo tu. Kama kuna Marealle, kuna nani watajulikana tu. Ndio maana siku zote nalia na vyombo vyetu vya kusimamia sheria, juhudi inayoonekana hapa ni ya kuzima hii ishu na wala si kutafuta ukweli ndio maana yanaanza kutajwa majina ya watu na makampuni mapema wakati mtoa madai yupo, wanaodaiwa kupokea bahasha wapo. Kamata ncha ya kamba na kwenda nayo utapata mwisho wake full stop!!!!!.
 
Hivi niulize kwani zile fedha zilikwisha changishwa toka hizo Taasisi, na wizara ilikuwa ktrk process ya kuzitumia? au mnatumia ushahidi wa barua ile ya Beatrice kama ndio ncha ya kamba..
 
Nadhani ndugu zangu tunatoka kwenye issue ya msingi na kuanza kudebate masuala ambayo hayana msingi. Suala muhimu hapa ni kujua nani aliidhinisha fedha zitoke na nani wametoa (zile taasisi) halafu pia ijulikane kama ndio utaratibu unaotumika hata kwenye wizara nyingine. Bw Aggrey Marealle ameshakanusha kuwa hahusiki. Ni vizuri kusubiri uchunguzi ufanyike. Halafu mimi nilidhani suala kubwa sasa hivi ni umeme. Tungekuwa tunatoa mawazo ya namna gani tunaweza kuondokana na hili tatizo lakini tumeshakubali kupindishwa mawazo haraka. Mjadala mkubwa ulikuwa kwenye umeme lakini sasa imekuwa Executve Solutions. Mimi binafsi nadhani this is so irrelevant tunalazimishwa kudivert debate kwenye vitu ambavyo havina msingi kwa sasa wakati mgao unaendelea na pia kuna masuala mengine muhimu ya kitaifa ya kujadili na sio ES.
 
Wildcard, unawasaidia kuhamisha magoli sasa Lol- tetesi ni kuwa kuna kampuni ya PR ndiyo imefanya hivyo - siyo Waziri! Well, kampuni iliyokuwa inatajwa ni hii na kama wamekuja kukanusha na kama ni kweli - basi kuna kampuni nyingine, Itajwe na yenyewe tuiweke on the record. Sasa mkianza kusema ni "waziri mwenyewe" nadhani hapa mtakumbana na ugumu mkubwa zaidi wa kuthibitisha. Njia pekee ya kujua nani alihusika ni kwa wabunge waliopewa fedha waseme walizipokea toka kwa nani... kama hayupo ambaye anaweza kujitokeza ni vigumu kweli kumhukumu Jairo... I can see this case crumbling like soaked biscuits..

Kwa kuwa hakuna utashi wa kutafuta ukweli ndio maana suala hili litakufa bila a hatua zozote kluchukuliwa. Ikumbukwe kuwa matumizi yote halali ya Serikali hufanyika under certain "accounting vote". Hivyo kitedo cha Jairo kutoa amri ya taasisi zilizoko chini ya wizara yake kutoa fedha nje ya utaratibu wa acounting vote ni matumizi mabaya ya madaraka. Hilo halihitaji uchunguzi wa aina yoyote. Aliyeharibu suala hili ni Pinda aliposhindwa kujiuzuru pale JK alipotoa maamuzi tofauti na yael aliyokuwa akiamini na kuyatia bungeni
 
Wildcard, unawasaidia kuhamisha magoli sasa Lol- tetesi ni kuwa kuna kampuni ya PR ndiyo imefanya hivyo - siyo Waziri! Well, kampuni iliyokuwa inatajwa ni hii na kama wamekuja kukanusha na kama ni kweli - basi kuna kampuni nyingine, Itajwe na yenyewe tuiweke on the record. Sasa mkianza kusema ni "waziri mwenyewe" nadhani hapa mtakumbana na ugumu mkubwa zaidi wa kuthibitisha. Njia pekee ya kujua nani alihusika ni kwa wabunge waliopewa fedha waseme walizipokea toka kwa nani... kama hayupo ambaye anaweza kujitokeza <span style="color:#ff0000;">ni vigumu kweli kumhukumu Jairo</span>... I can see this case crumbling like soaked biscuits..
<br><br>

Kwa kuwa hakuna utashi wa kutafuta ukweli ndio maana suala hili litakufa bila a hatua zozote kluchukuliwa. Ikumbukwe kuwa matumizi yote halali ya Serikali hufanyika under certain "accounting vote". Hivyo kitedo cha Jairo kutoa amri ya taasisi zilizoko chini ya wizara yake kutoa fedha nje ya utaratibu wa acounting vote ni matumizi mabaya ya madaraka. Hilo halihitaji uchunguzi wa aina yoyote. Aliyeharibu suala hili ni Pinda aliposhindwa kujiuzuru pale JK alipotoa maamuzi tofauti na yael aliyokuwa akiamini na kuyatia bungeni
 
Inawezekana unachokisema lakini mimi naona kama huu mjadala unalenga kueneza chuki kwa mtu binafsi. Sidhani kama Aggrey ninayemfahamu anaweza kukubali kujiingiza katika mambo kama haya. Yeye ni mfanyabiashara na si mara yake ya kwanza kwenda Dodoma wakati wa Bunge kwa shughuli mbalimbali. Uchunguzi utabaini kila kitu. Sote tunataka kujua ukweli maana hatuwezi kufumbia macho uchafu kama huu wizarani ila tu natahadharisha...tusije tukajikuta kunaeneza chuki kwa mtu binafsi bila kuwa na ushahidi wa jambo nyeti kama hili. Simtetei maana kama kweli amehusika then ukweli utajulikana tu na atachukuliwa hatua zinazostahili.
 
Back
Top Bottom