Exclusive: Wizi nyumbani kwa Rais Mstaafu Mwinyi

Wizi umetokea wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi za kitanzania ndani ya nyumba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Wafanyakazi wa ndani ya nyumba ambao ni wa Serikali walikamatwa pamoja na wengine watatu ambao ni wajenzi wa kampuni moja binafsi waliokuwa wakifanya matengenezo madogo nyumbani hapo.

Wafanyakazi wa ndani waliachiwa huru na wale wa nje huenda watafikishwa mahakamani karibuni. Fedha hizo inasemekana ni za mtoto wa Mwinyi ambaye inasemekana ni daktari. Fedha hizo alishtukia tu hazipo hajui zilipotea lini na kwa namna gani.

Familia za waliowekwa ndani zinahangaika kuwatoa ndugu zao ambao hawana kabisa historia ya wizi na mmoja wapo ameshuhudiwa akilia kama mtoto.

Jambao la ajabu ni kwamba sheria za kiusalama ni kwamba wakati wa matengenezo mafundi hawaruhusiwi kuingia vyumbani bila mlinzi.

Katika mchakato wa dhamana pale mahakama ya Kinondoni Hakimu amelamba 100,000 kutoka kwa familia hizo tatu za watu masikini, huku afisa mzungusha faili akichukua 30,000.

Uonevu mtupu!!
Hakuna cctv kwa mstaafu?
 
Mi najua yule ni mzee wa RUKSA, inawezekana hao mafundi wameingia ndani wakijua ni RUKSA, wakaingia mpk chumbani RUKSA, wakafungua drooo RUKSA, wakabeba pesa RUKSA. Kama ni walinzi au wafanyakazi pia ni RUKSA, no accusation at all, simple because ni RUKSA........I wonder wanapelekana mahakani!!!!!!!

Umeniacha naumwa mbavu...pia sintoshangaa mzee yule akisema waachiwe huru,
 
Kuna mazungumzo yanaendelea kati ya mwenye kampuni ya ujenzi na Mzee Mwinyi. whether watafikia makubaliano lets wait and see.

Umeniacha naumwa mbavu...pia sintoshangaa mzee yule akisema waachiwe huru,
 
Hakuma mtt mwenye akiki timamu atakayeelewa. Taarifa zinasema mafundi walikuwa wanaingia na walinzi, sasa inakuaje wahusishwe?? Familia ya mzee Mwinyi imeanza utapeli. Mwinyi is now loosing his good reputation.

Si kweli huyo Mzee namtetea ila vijana wake ni wahuni, utawekaje ten mm ndani usijue ziko wapi??? Ukola huo, no case to unswer. Hao watu wamekamatwa na exibit??????????
 
Isijekuwa wamepanga ili wasiwalipe kwa kazi yao.

Kwa hali ilivyo sasa, jamaa wanaombea tu watoke na hiyo kazi ndiyo imetoka.

Sidhani kama watarudi hata kuchukua vyombo vyao.

Dunia hii, mtu anakamatwa tu hata bila ushahidi. Wao ushahidi upo wanasemwa "Mahakama itaamua."

Mahakama kabla haijaiona kesi, TAKURURU inamuosha mtu na kesi imekwisha.
 
Mnashangaa nini kama Msanii mmoja Dotnata anatumia Million kwa Siku, kuanzia kuweka mafuta Kwenye gari lake Range Rover Sport, kwenda Salon, Kula hadi wapambe , Kama wasanii wengi wanatumia laki saba kwa siku tunashangaa hizo, Mbona Mzee wa wa Vijisent anafua Nguo LONDON unafikili kuzisafilisha ni shilling ngapi, hizo hela ni matumizi tu ya kawaida. Kuibiwa angenyamaza tu huyu mzee, labda muibaji kasota sana pale Benki akisubili akopeshwe 5m bila mafanikio, hata hivyo anarudisha zilipotoka kwa wananchi
 
Umenikumbusha habari moja niliyoisikia miaka miwili mitatu hivi nyuma wakati EL bado ni PM. Katika mahesabu ya kufunga mwaka katika kampuni ya Caspian ya RA, mahasibu walikuta ziada ya Sh 400 milioni ambazo hawakujua zimeingia vipi katika vitabu vya mahesabu -- maana hazikuwa kutokana na mapato ya kampuni yanayoeleweka.

Wakamuuliza mmiliki, RA, kuhusu hela ile. Pale pale akampigia simu EL na kumuuliza: "Ulipeleka hela pale Sh 400 kule Casspian?" EL akajibu "la hasha."

Baadaye siku iliyofuata EL akakumbuka vizuri kumbe ni hela zake akampigia simu RA: "Hizo hela zililetwa na yule mjamaa? (akamtaja jina) -- ni zangu ndiyo."

Akamwambia aende akazichukuwe kwani zinawachanganya mahasibu wake.

This is a joke jamani. Yaani m2 anasahau kama kawekewa 400m kwenye A/c?:frusty:
 
Hii so wamewatengenezea mafundi basi tunakubali kaweka ndani nani alikuwepo ? Nani kawaona mafundi wakichukua ? Hapa hamna kesi usumbufu na uonevu . Yana mwisho .katiba mpya itakayolinda haki na heshima ya watz wote
 
kwani pesa siku hizi zinatunzwa ndani? bank ni kwa ajili ya nani? me nashauri naye akamatwe kwa uzembe
 
Wizi umetokea wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi za kitanzania ndani ya nyumba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Wafanyakazi wa ndani ya nyumba ambao ni wa Serikali walikamatwa pamoja na wengine watatu ambao ni wajenzi wa kampuni moja binafsi waliokuwa wakifanya matengenezo madogo nyumbani hapo.

Wafanyakazi wa ndani waliachiwa huru na wale wa nje huenda watafikishwa mahakamani karibuni. Fedha hizo inasemekana ni za mtoto wa Mwinyi ambaye inasemekana ni daktari. Fedha hizo alishtukia tu hazipo hajui zilipotea lini na kwa namna gani.

Familia za waliowekwa ndani zinahangaika kuwatoa ndugu zao ambao hawana kabisa historia ya wizi na mmoja wapo ameshuhudiwa akilia kama mtoto.

Jambao la ajabu ni kwamba sheria za kiusalama ni kwamba wakati wa matengenezo mafundi hawaruhusiwi kuingia vyumbani bila mlinzi.

Katika mchakato wa dhamana pale mahakama ya Kinondoni Hakimu amelamba 100,000 kutoka kwa familia hizo tatu za watu masikini, huku afisa mzungusha faili akichukua 30,000.

Uonevu mtupu!!

Upuuzi mtupu.
 
Umenikumbusha habari moja niliyoisikia miaka miwili mitatu hivi nyuma wakati EL bado ni PM. Katika mahesabu ya kufunga mwaka katika kampuni ya Caspian ya RA, mahasibu walikuta ziada ya Sh 400 milioni ambazo hawakujua zimeingia vipi katika vitabu vya mahesabu -- maana hazikuwa kutokana na mapato ya kampuni yanayoeleweka.

Wakamuuliza mmiliki, RA, kuhusu hela ile. Pale pale akampigia simu EL na kumuuliza: "Ulipeleka hela pale Sh 400 milioni kule Casspian?" EL akajibu "la hasha."

Baadaye siku iliyofuata EL akakumbuka vizuri kumbe ni hela zake akampigia simu RA: "Hizo hela zililetwa na yule mjamaa? (akamtaja jina) -- ni zangu ndiyo."

Akamwambia aende akazichukuwe kwani zinawachanganya mahasibu wake.

Haya ndo mambo ya secret service agent wa JackBouer!
Imekaa ki udaku vle ila inaukweli ndani yake coz diz guyz they really knw how to f**k 'emselves
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom