Exclusive: Video ya mlipuko wa bomu Arusha

unawadhalilisha wazazi wako mkuu sababu wanaamin wana mtoto mwenye akili timamu sasa mbona unaonekana unawaza kama mtoto anae lilia chuchu????una mdhalilisha zaid maako alie kupa virutubisho vyote lakini bado huna akili au ni usahabiki tu unaokuendeshaa???unajilemaza kifikra we endelea kuigiza huna akili sababu ya posho za nape utakuwa ivoivo milele shauri yako!!!!

huyu anaonekana haknyonya sawasawa,akili yake fupi sana huyu!
 
Wababodi hii mambo inashangaza sana Rais mara hii hajataka kabisa vunja safari au hata kuonyesha concern yoyote ili wakubwa wasianze mshangaa.Kajitahidi sana act km hakuna kitu.

Rais kasahau kuwa waliokufa ni raia na yeye ni rais wa nchi....Na tukio la ugaidi si la kawaida kwa nchi yetu na popote duniani.Na hili linaweza lisiwe kitu kikubwa ama kitu cha uani kwa wale waliopanga tuu.

Kwa kiongozi mwingine hii si habari nzuri kwani ni dalili hata yeye anaweza kumbwa na haya mambo.Ila kwa aliyepenga anajua hili halihusiani na kuhatarisha utawala wake?

Rais pi anasahau kuwa kibaya hapa si kuwa atasingizia CDM na hata ikithibitika ni serikali basi yeye ahtofanywa kitu,kibaya hapa ni kwamba ikithibitika ni CCM (Kwa kiasi kikubwa tayari) basi VATICAN WATAKUWA NA HAKI YA KUWAULIZA SERIKALI KUHUSU JARIBIO LA KUMUUA BALOZI WAKE.

Sijui km Rais kaliona hili vyema, au anapambana kuuza kuuza nchi na kuomba omba kusiingie mchanga.Hajui kwamba CDM wanazidi shinda hii propaganda waliyoanzisha CCM.
 
Bado nafikiri na kuwapongeza sana CDM kwa kuwa na offshore storage ya video...Polisi walipoamua shambulia watu na gari walikuwa wame aimu ktk total destructions.Je wangefanikiwa lipua gari leo wsingetuambia kuwa gari ile ilisheheni mabomu?Ingawa mabomu kwa wataalamu wangeuliza uwepo wa maultiple explosions...pengine polisi wangeendelea chochoea kwa kutuia mengine ila kuna mengi ya kuuliza.Habari isingekuwa hii tuliyo nayo leo.

hakuna anayejua CDM waliweka kamera ngapi na maendeo gani ili baada ya camera moja kulipuliwa ktk tukio basi ingine iwe inapata kwa mapana yaleyale pamoja na matukio yaliyopelekea ingine kulipuliwa.


Gari ile ingelipuka basi leo tungekuwa na version ingine pengine mbaya zaidi ya kubeba mabomu.
 
Serikali+bunge+polisi wamejaribu sana kuwa waangalifu ktk kupotezea ili lisiate umuhimu unaostahili ili raia wasianza uliza sana zaiid ya kuona km ni issue ya CDM.
 
Bomu lawatesa CCM, Polisi

• Mwigulu, Ghasia wakimbilia kujisafisha

na Edson Kamukara na Josephat Isango





MLIPUKO wa bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA mkoani Arusha na kuua watu wanne, umeiweka kwenye wakati mgumu serikali ya CCM, Jeshi la Polisi na Bunge.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema juzi bomu lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA ni la kijeshi na limetengenezwa China na uzoefu unaonesha hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.
Wakati Pinda akitoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa CHADEMA wamelihusisha Jeshi la Polisi na tukio hilo huku wakidai wanao ushahidi unaonesha askari aliyevalia sare akilirusha kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii, wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kukiri kwa serikali kuwa bomu hilo limetengenezwa China, inapaswa iibane nchi hiyo ieleze iliyemuuzia na alivyoliingiza nchini.
“Kwanini isiundwe tume huru nchini ili nchi ya China iulizwe baada ya kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Na kama haikuiuzia serikali, basi ni dhahiri tuiulize China kwanini inafadhili vikundi vya kigaidi nchini kwetu?
“Je, kama bomu lilitengenezwa China, tuangalie kama mkataba wa majukumu ya mataifa duniani kuhusu silaha, nchi hiyo inatakiwa kutoka na kauli kuhusu bomu hilo na kwa kukaa kimya maana yake wanakubaliana na maelezo ya serikali,” alisema.
Wakati maswali hayo yakionekana kuumiza vichwa vya watawala, viongozi wa CHADEMA kwa upande wao wamegoma kutoa ushahidi walionao kwa Jeshi la Polisi mpaka Rais Jakaya Kikwete atakapounda tume ya kijaji itakayosikiliza ushahidi huo na kuendesha kesi hiyo.
Hali ya mambo ikiwa hivyo, viongozi wa CCM na wabunge wameanza kulitumia Bunge kukishambulia CHADEMA kuhusu mlipuko huo kwa lengo la kukinusuru chama chao, Tanzania Daima limedokezwa mbinu hiyo.
Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, juzi bungeni walidai kuwa CHADEMA ndio wamekuwa wakihusika na vurugu zote zinazohusisha mauaji nchini.
Kauli za viongozi hao zinakuja takriban siku tano tangu Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kudai CHADEMA kiliandaa na kuratibu shambulio hilo ambalo lilitokea kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani.
Licha ya Mwigulu kujadili jambo lililokuwa nje ya mjadala wa bajeti na linaloendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alimwacha aendelee kukilaumu CHADEMA ikionekana ni mkakati rasmi wa kulinasua Jeshi la Polisi na serikali ya CCM kwenye tuhuma hizo.
Katika madai yake, Mwigulu alianza kusema kuwa jambo la usalama wa nchi hii amekuwa akiliongelea kwa haraka haraka, hivyo watu wamekuwa hawamwelewi.
“Leo naomba nilisema kwa utaratibu, jambo la usalama nimekuwa nikilisema na kuomba kama Elia aliyemwambia mtumishi wake kuwa anamwombea Mungu amfungue macho ya kimungu ili aone jinsi yeye anavyoona.
“Jambo limetokea kama hili la Arusha, nimeyaongea sana mambo haya na sasa hivi ilipotokea mimi nitasema tena na wenzetu nikiwasema mara wanasema wataenda jimboni. Nawashauri wasiende tu jimboni, bali wajenge kabisa makao makuu ya chama chao,” alisema.
Mwigulu ambaye alikuwa akishangiliwa na baadhi ya wabunge na baadhi ya mawaziri akiwemo William Lukuvi, George Mkuchika, Ghasia, Mary Nagu na wengine alisema anausema ukweli.
“Ni lazima tuwaze tuvuke mipaka, kuna mambo yanawezekana kabisa yakawa yamejificha pale. Watu wanaangalia, wanaojitoa ufahamu wanafikiria CCM inaweza kushiriki.
“Mimi niwaambie CCM, hata bila kushiriki, moja kwa moja inawekwa kwenye lawama, jambo kama hilo likitokea. Ila CCM haina ushiriki katika jambo kama hili kwa sababu ndio watu wake kupitia serikali yake inatakiwa kuwahakikishia usalama,” alisema.
Alisema kuwa ni lazima waangalie maana wengine waliojaa ushabiki linapotokea jambo wanakwenda moja kwa moja kuwa inawezekana CCM imeshiriki.
Mwigulu aliongeza kuwa lazima yaangaliwe mazingira ya nchi kwa sasa, hasa kipindi hiki ambapo wanakuja wageni wakubwa wakiwamo marais wa China na Marekani, kwamba mataifa mengine ambayo yanajua ujio wa wageni ni biashara, wanaweza kuichafua Tanzania.
“Sisi tunakimbilia tu CCM ndiyo imejaa midomoni mwa watu, lakini hoja nyingine Tanzania imekuwa kisiwa cha amani, hivi wale ambao hawatutakii mema hamjajua eneo wanaloweza wakagusa?” alihoji.
Huku akinukuu ripoti ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kuhusu utekwaji wa Mwenyekiti wake, Absalom Kibanda, katibu huyo alidai CHADEMA imetajwa kuwa ndiyo inahusika na matukio hayo ya utekeaji kwa kushirikiana na maofisa usalama wasio waadilifu ili kuonesha kuwa CCM imeshindwa kuongoza na sasa inaua watu wake.
“Niliwahi kulisema hili kuwa kuna mambo mengine yanafanyika kwa hujuma na tumeziona hizo hujuma lakini watu wengine wanawahi kuamini haraka.
“Lakini hawa wenzetu kama waliwahi kumvalisha raia sare za jeshi na alihukumiwa, wanashindwaje kila wakati wanasema polisi… polisi. Tunashindwaje kuamini kama wanaweza kumvalisha mtu nguo za polisi na akafanya yale?” alihoji.
Mwigulu alisema taarifa ya Polisi Mkoa wa Morogoro kuhusu tukio la kifo cha kijana Ali Zona, kilichotokea wakati wa maandamano ya CHADEMA, zinasema chama hicho ndicho kilihusika.
“Yule kijana aliyeuawa Morogoro taarifa zilizopo hakuuawa na polisi, ni CHADEMA wao wenyewe walitoka pale wakatengeneza ile vurugu wakamfyatulia risasi ili kutengeneza kwamba serikali ya CCM inakandamiza wapinzani,” alisema.
Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi aliongeza kuwa hata video ya mauaji ya Arusha iliyowekwa kwenye mtando wa You tube inaonesha wazi kuwa yalipangwa.
“Yule aliyekuwa anachukua video eti hakushtushwa kabisa na lile bomu, aliendelea kufuatilia kama vile ni mkanda wa harusi. Iliwahi kutokea wapi mchukua video kwenye mkutano wa hadhara kitu ambacho hakikupangwa kimelipuka, kinaua watu, yeye anendelea kama anachukua ‘sendoff’?” alihoji.
Baada ya Mwigulu kumaliza, Hawa Ghasia ambaye ni mjumbe wa NEC alipewa nafasi ya kuchangia bajeti hiyo kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge, lakini naye akatumia muda mwingi kuilaumu CHADEMA kwa matukio ya vurugu nchini.
Ghasia alitumia muda huo kupanda mbegu ya ubaguzi wa kimaeneo akidai kuwa CHADEMA wamechochea vurugu Mtwara, Mwanza, Mbeya, Morogoro na sasa Arusha ili maeneo hayo yasipate maendeleo kama Mkoa wa Kilimanjaro wanakotoka baadhi ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho.
Ghasia alisema wiki iliyopita alikuwa Kilimanjaro anakotokea Mbowe na Ndesamburo, hakuona vurugu za kuchoma matairi wala kupigwa kwa mabomu kama ilivyo Arusha.
“Jamani tuwe macho na hawa CHADEMA hawataki wawekezaji waende mikoa mingine tofauti na Kilimanjaro ndiyo maana wanahamasisha vurugu katika mikoa ya wenzao.
“Wanafanya vurugu Arusha ili watalii wagome kwenda huko, wanataka watalii wakimbilie Kilimanjaro. Jamani tusiwakubalie hawa jamaa wataliingiza taifa letu kubaya,” alisema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji alisema kinachofanywa na CHADEMA mkoani Arusha na kwingineko kinaathiri uwekezaji kwani wawekezaji watakimbilia nchi jirani.
Nagu alisema kutokuwapo kwa wabunge wa CHADEMA kumelifanya Bunge liwe tulivu tofauti na linavyokuwa wakiwapo wabunge hao.
Katika kile kinachoonekana wabunge wa CCM walijipanga kikamilifu kukisulubu CHADEMA, kilichokosa wawakilishi, Waziri asiye na wizara maalumu, Mark Mwandosya, alitumia kauli mbalimbali za mafumbo kukinanga chama hicho cha upinzani.
Mwandosya alisema anaamini uchaguzi mkuu ujao, watu watachagua amani dhidi ya vurugu, upendo dhidi ya chuki, amani dhidi ya vita huku kwenye siasa watachagua vyama vinavyowaelekeza katika maendeleo na si vile vinavyowaelekeza katika vurugu, migogoro na machafuko.
Kutokuwepo kwa wabunge wa CHADEMA pia kumeonekana kunatoa nafuu ya mijadala ambapo Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema mijadala mbalimbali iliyofanyika kwa siku nne imekwenda vizuri na Bunge limekuwa kama la zamani.
Wakati hali ya mambo ikiwa si shwari ndani ya CCM, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, juzi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanawasiliana na makachero wao kuangalia hatua za kisheria wanazoweza kuwachukulia viongozi wa CHADEMA waliogoma kutoa ushahidi.
Alisema maelezo ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa waandishi wa habari aliozungumza nao hivi karibuni ni tofauti na yale waliyoyatoa polisi, hivyo jeshi hilo litaangalia njia za kuuthibitishia umma kuwa tuhuma dhidi yao si za kweli.

 
mimi kuanzia 1:21:00 nnashindwa kuelewa, maana waliojeruhiwa hawazidi pamoja na kufa hawazidi watu 10 lakini baada ya tukio imeripotiwa watu zaidi ya 60 walijeruhiwa Kwa hili Polisi wana la kusema, nnaamini polisi ndo waliongeza idadi ya majeruhi
 
Mie naomba wawakamate kina Mbowe, Lema, Lisu waliohutubia katika mkutano ule wa pale Soweto. Wakifikishwa mahakamani mbivu na mbichi zitajulikana.

Lengo la kina mwigulu (savimbi) nchimbi (bokasa) ilikuwa kulilipua gari la matangazo la CDM ili mlipuko uwe mkubwa na uuwe wengi akiwemo Mbowe, Tundu Lisu na Lema. Ila Jehova Adonai aliepusha ushetani wao huo.
 
Tungekuwa na versions ngapi toka kwa polisi waliozoea kupika "chunguzi" na "matukio"?Habari zingekuwa nyingi kichwani kwa watanzania km miluzi mingi kwa mbwa..

Mwigulu angelia kabisa Bungeni...kuwalaani CDM kwa kubeba mabomu mengi vile ktk umati mkubwa vile...?
 
Je Cjhagonja atawatuma hao makachero wakapole hiyo video au wapandilize Ludovictoria mwingine ili waupate? Nawashauri makamanda wafiche kucha zao na meno yao vinginevyo wanaweza kuendeleza orodha ya waathirika wa kauli ya Pinda.
 
Jamani Wakuu Vp ule Ushahidi wa Video alizosema Mh.MBOWE
Je! Ni kweli Polisi walihusika katika Ulipuaji wa hayo Mabomu.?
 
Unawazimu...swali gani hilo unauliza...ht km umejiunga juzi..pitia thread zilizomo usome..ss tukujibu nini...bora tu trh 24 ifike mwende jeshini au we ndo wale wa miduara
 
We Umejuaje Me naenda Jeshini!
Nakujua habari Ni haki yangu wewe kama hujui unatulia..
 
Kwakuwa kujua habari ni haki yako wacha tukuhabarishe:
Polisi walirusha bomu na kuwapiga risasi watu hovyo, watoto waliokuwa wanatoka madrasa nao walipigwa risasi na polisi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Pitia thread mbalimbali humu jamvin ujionee wewe mwenywe hiyo video
Jamani Wakuu Vp ule Ushahidi wa Video alizosema Mh.MBOWE
Je! Ni kweli Polisi walihusika katika Ulipuaji wa hayo Mabomu.?
 
Back
Top Bottom