Exclusive Pictures: SeaFront- Imeuzwa nayo!

CCM----Chukua Chako Mapema, ndio wako kazini ati. Laitia hawa wangeondolewa wengine wamgeweza rectify mambo japo kwa kiasi kabla hawajajanjaruka(kila Mtz ni fisadi mtarajiwa).
Inauma sana wakuu....ila tu waoga, tungeweza kutia ngumu jamaa wasifanye chochote...mmh nani atataka kupigwa mabomu ya machozi....bora wajichukulie chao.......mimi wakianza levelling nitajitosa kwenye greda ili kujitoa muhanga kutetema mali yetu.....mmmh nitaweza kweli!

Jamani nami kibaruani kwangu kuko jirani kweli na eneo hilo, kila siku kuliona likitoweka inaumaaaa!
 
Mwenzenu nilishaona kulalamika hakunipi faida...hivyo dawa ni kwenda nao sambasamba...vikiuzwa na mimi nanunua. Nikiwa sina hela najipanga sehemu nyingine.

Arthi yetu ndio hii hii...tunabanana hivyo hivyo.

YY
 
Kuna umuhimu wa kuijua vema nchi yetu kiutawala, kisiasa, kiuchumi na kijamii ili tuweze kuijadilii kwa upeooo...

Kwa hili ningelalama na nitalalama tuu pamoja na mabadilko yotee ya kisheria yaliyofanya kuhalalisha matumizii hayooo..

Ila Mzee Mwinyi mbona mapungufu ya utawala wake yalishapitaa kwani hulka yake hairuhusuu tumlaumu sana sisi wa kupenda mambo mepesii mepesiii!! Afterall yeye ni wasaidizi wake ndo wenye makosa lakini BM Ule ujeuri na ujasiri wake yeye ndo tutajitahidii KUMLAUMUUU...
 
Kama wameweza kuwabomolea watu majumba kwa ajili ya upanuzi wa barabara, basi wajiandae, nchi ikiingia kwenye utawala wa sheria tu nao watabomolewa.
 
Picha zinaonekana, ila Mzee Mwanakijiji umeziacha kwenye file kubwa, hivyo internate zenye speed ndogo kama nyingi ya cafe zetu, then haifungui, ila picha zipo.

Ukanda wote wa beach toka Toure drive inakoanzia mpaka Sea Cliff, imeuzwa, miti yote imeshakatwa, wenye viwanja vyao wameanza kufanya fencing, hadi Coco Beach, yule mmiliki Alphonse Buhatwa, amepiga kelele sana, sijua kama kilio chake kimesikika na kubakizwa miongoni mwa wamiliki..

Tayari Zainudeen Adamjee amewaorganize wakazi, wamepinga mahakamani, ujenzi umeshasimamishwa. Nalo Baraza la Usimamizi wa Mazingira limewashikia kidedea wakitaka EIA kwanza.

Kwa mliosoma ile Ripoti yas Warioba, ilisema wazi kuwa Rais Mwinyi, ilisaini badiliko la matumizi ya ardhi ile kwa kutegua ile sheria ya mkoloni iliokataza ujenzi wa kando ya bahari.

Viwanja 18 wilipimwa kwa presidential discretion na alipewa yeye, familia yake na marafiki zake.

Miongoni mwa viwanja hivyo 18, ni 2 tuu ndio vimeendelezwa ambavyo vilitolewa kwa rafiki zake. Hivi ni kile kilichojengwa Sea Cliff na Golden Tulip, hivyo 16 vilivyobaki havijaendelezwa, sasa wamiliki waliogaiwa ndia wameamuas kuviendeleza, kelele za nini?

Baada ya rais kutengua lili zuio la mkoloni na baada ya kuwagawia hao nduguze na rafikize, ndipo rekebisho lilipelekwa bungeni kuwa endorsed. Mzindakaya alipiga kelele sana, iweje jambo lifanyike kwanza, kinyume cha sheria, halafu bunge lilitewe kuubariki uchafu huo!

Bunge likakaa kama kamati ya chama, Mzindakaya akatulizwa, nadhani kwa chochote kitu, ukiwemo mgao wake kwenye vitalu vya uwindaji, akatulia. Bynge likarejea, na wakabariki, sasa cha kushangaza ni kipi hapa?

Nchi ilishauzwa siku nyingi, wenye nacho, wanaongezewa, wasio nacho, wananyang'anwa kidogo walichonacho, hivyo tutafikia mahali, watoto wetu na watoto wa watoto wetu, waishia kuwa wapangaji ndani ya nchi yao for the rest ofb their life, by that time, waliofanya hayo, na tulioshuhudia yakifanyika na tukaa kimya, we will have been long gone!.
Thanks for this background kwa sababu kuna watu wanaweza kudhani kuwa viwanja hivi vimeuzwa juzi
 
Mkuu,

Mrema aliongelea sana hii enzi zile akiwa NCCR..lakini yeye pia alikuwa anaunga mkono...kwamba kuliko vivyo viwanja kupewa wakina Chavda ni afadhali Mwinyi aliamua kuwapa watoto wake..!!
There is something wrong with Tanzania
 
Hapo kwenye blue ndio tatizo letu kubwa, institutional framework system yetu ndio ya kulaumiwa. Kwa sababu unaweza kutokea mtu ukapinga ubaradhuli unaofanywa na watu lakini hakuna njia yoyote ya kukulinda. Unaweza kufikiri what Mwinyi did ingekuwa Marekani, I am sure impeachment ingemkuta.

Picha zinaonekana, ila Mzee Mwanakijiji umeziacha kwenye file kubwa, hivyo internate zenye speed ndogo kama nyingi ya cafe zetu, then haifungui, ila picha zipo.

Ukanda wote wa beach toka Toure drive inakoanzia mpaka Sea Cliff, imeuzwa, miti yote imeshakatwa, wenye viwanja vyao wameanza kufanya fencing, hadi Coco Beach, yule mmiliki Alphonse Buhatwa, amepiga kelele sana, sijua kama kilio chake kimesikika na kubakizwa miongoni mwa wamiliki..

Tayari Zainudeen Adamjee amewaorganize wakazi, wamepinga mahakamani, ujenzi umeshasimamishwa. Nalo Baraza la Usimamizi wa Mazingira limewashikia kidedea wakitaka EIA kwanza.

Kwa mliosoma ile Ripoti yas Warioba, ilisema wazi kuwa Rais Mwinyi, ilisaini badiliko la matumizi ya ardhi ile kwa kutegua ile sheria ya mkoloni iliokataza ujenzi wa kando ya bahari.

Viwanja 18 wilipimwa kwa presidential discretion na alipewa yeye, familia yake na marafiki zake.

Miongoni mwa viwanja hivyo 18, ni 2 tuu ndio vimeendelezwa ambavyo vilitolewa kwa rafiki zake. Hivi ni kile kilichojengwa Sea Cliff na Golden Tulip, hivyo 16 vilivyobaki havijaendelezwa, sasa wamiliki waliogaiwa ndia wameamuas kuviendeleza, kelele za nini?

Baada ya rais kutengua lili zuio la mkoloni na baada ya kuwagawia hao nduguze na rafikize, ndipo rekebisho lilipelekwa bungeni kuwa endorsed. Mzindakaya alipiga kelele sana, iweje jambo lifanyike kwanza, kinyume cha sheria, halafu bunge lilitewe kuubariki uchafu huo!

Bunge likakaa kama kamati ya chama, Mzindakaya akatulizwa, nadhani kwa chochote kitu, ukiwemo mgao wake kwenye vitalu vya uwindaji, akatulia. Bynge likarejea, na wakabariki, sasa cha kushangaza ni kipi hapa?

Nchi ilishauzwa siku nyingi, wenye nacho, wanaongezewa, wasio nacho, wananyang'anwa kidogo walichonacho, hivyo tutafikia mahali, watoto wetu na watoto wa watoto wetu, waishia kuwa wapangaji ndani ya nchi yao for the rest ofb their life, by that time, waliofanya hayo, na tulioshuhudia yakifanyika na tukaa kimya, we will have been long gone!.
 
Jirani na hapo palipouzwa, kuna ghorofa limeharibiwa na jiji utadhani lilipigwa mabomu vile. Sasa kwa kuwa kuna double standard, kuna ghorofa jingine jipya (8 floors) limesimikwa (linaonekana kwenye picha ya Mwanakijiji), na kila kitu juu ya mstari na wapangaji (ni appartment) wamo ndani.

Ilipouzwa jimkana grounds kujengwa Sheraton, kelele zilipigwa, lakini Mwinyi huyuhuyu akaweka gundi masikioni...na Mradi ndio ule, haujalipa kodi toka siku ya kwanza. Na Mwinyi naye bado yupo. kwanini asiitwe na wanahabari ajibu maswali tata kama haya? Au naye ni indispensable kama Mkapa? Labda yule aliyemchapa kofi alikuwa na hasira hizi.

Something has to be done kwa kweli, ingawa sijui ni kitu gani.
 
Asante tunaziona picha sasa. Inatia uchungu! Hivi maandamano nchini kupinga mambo kama haya yalishapigwa marufuku au watu hatuna guts za ku-mobilize? Au Polisi hawatatoa kibali?
 
yanatimia....!
TUMEUUZA UHURU WETU NA MALI ZETU...........

Kwa hiari yetu wenyewe, kwa kutumia nguvu zetu wenyewe, kwa akili zetu na utashi wetu ulioambatana na upofu uliojaa tamaa, uvivu, usengenyaji na uroho, Tumeuza Uhuru wetu na hazina yetu tumeifuja.

Sisi ni koloni lililo na Uhuru wa Bendera, tumejitakia kwa ujuvi wetu kuwa masikini wa kudumu, wanyonge ndani ya nchi yao na kuburuzwa kila siku kama majuha.

Angalieni jinsi neema tulizopewa na Mola tulivyoziharibu kutokana na tamaa, majaribu, ujinga na kiburi kilichojaa uvivu na utegemezi.

Zi wapi zile ndoto za Kujitegemea, Siasa safi, Uongozi Bora kwa kutumia Juhudi na Maarifa kuupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi?

Kila siku kukicha ni baragumu za ufujaji na uhujumu. Leo ni Benki Kuu, mara ni ATCL, TRL, Tanesco, Misitu, Utalii, ardhi, madini, uvuvi na hata kujiingiza katika kuatakia shari jirani zetu na kuneemesha maangamizi ndani ya ardhi yao.

Siwalaumu viongozi pekee, bali lawama za kwanza ni kwangu mimi (na wewe), niliye mjinga ambaye kwa upumbavu nimekimbia majukumu yangu na wajibu wangu niliopewa na Mola na kulindwa na Katiba ya Nchi yangu, kwa kuuza haki yangu ya kupiga kura kwa kukubali kuburuzwa kwa kulishwa andazi na chai.

Laiti ningekuwa mjasiri na kuitafuta kweli na haki na hata kuamua dira ya Taifa langu kwa kutumia umakini na busara, leo hii nisingekuwa hapa nikiangua kilio na kujitwisha mavumbi nikiwa nimevaa kaniki, nikihangaika kwa tabu na mateso, njaa na magonjwa yakiniwinda kwa urahisi nami nikawa mkimbizi wa ardhi niliyopewa na muumba.

Ni aibu ya kutisha, utajiri wote nimeutapanya kwa manufaa ya wageni na si ya ukoo na jamaa zangu. Nimeendelea kuwa mpumbavu kwa kulewa mvinyo na asusa za bure, nilizovimbiwa huku nikisifiwa kuwa nimejaaliwa neema na ni mpole.

Tumeuza nchi yetu, sasa tuamue tuendelee na maombolezo huku tukinyanyaswa na kusulubiwa na njaa na umasikini au tuamke tupukute vumbi, majivu na kufuta machozi na kuanza upya kwa kujitutumua na kutumia busara katika kutafuta haki.

Haki na hadhi yetu itarudi pale tutakapoamua kwa sauti moja iliyo kubwa na kishindo kuwa tumechoka kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa.

Tuikimbilie haki yetu kwa nguvu bila woga, tutumie dhamana yetu kwa ufasihi, ili hazina na rasilimali zetu ziwe kwa manufaa yetu, kama Muumba alivyotupangia.

Jiulize, mpaka lini utaendelea kuamini ahadi hewa, ukiwa umelewa togwa ya ukwaju na kupewa leso kufuta jasho, huku maji na kuku wa karamu ni yule uliyemtoa zaka?

Kuwang'oa mafisadi na kuushinda umasikini utaanzia na nafsi yako, kisha familia yako, ndipo cheche zitakaposambaa katika mtaa, kaya, kijiji, kata, tarafa, wilaya, jimbo, mkoa na Taifa.

Kuushinda Unyonge, Umasikini na Maradhi utaanzia kwako binafsi na kwa nguvu zako na majirani zako utaweza kuushinda utumwa.

Ni hiari yako kuendelea kuwa mtumwa au kuurudisha Uhuru wako na kulinda hazina yetu!
 
Ilipouzwa jimkana grounds kujengwa Sheraton, kelele zilipigwa, lakini Mwinyi huyuhuyu akaweka gundi masikioni...na Mradi ndio ule, haujalipa kodi toka siku ya kwanza. Na Mwinyi naye bado yupo. kwanini asiitwe na wanahabari ajibu maswali tata kama haya? Au naye ni indispensable kama Mkapa? Labda yule aliyemchapa kofi alikuwa na hasira hizi.

Something has to be done kwa kweli, ingawa sijui ni kitu gani.

....................Kupunguza hasira tukipata upenyo ni kuwachapa makofi tu.
 
yanatimia....!
TUMEUUZA UHURU WETU NA MALI ZETU...........
You are now recalling all posts by Rev. Kishoka, Invisible, Mwanakijiji etc?

Thanks Pasco, hata mimi nimefunguka macho. Walau nimepata mwanga. Wabunge wetu sijui wanasemaje katika hili?
 
Jamani hizi ripoti zinapotoka huwa zinawekwa wapi? Mbona watu hawapati fursa ya kuzijadili? Au ndo kama nilipowahi kusikia ya kuwa ukitaka kuwaburuza waTz weka mambo kwenye makaratasi hawana muda wa kusoma ila kwa kupiga soga ndio wenyewe!

Nimefurahishwa sana kwa idadi ya wachangia mada katika hili. Ila ratio yetu kwa Tz population is very minor lets establish live forum. Nilisahau wengi wetu tunachangia ila hatujitaji majina ya kweli. Kumbe sisi wote ni fisi maji!
 
Waulizeni wabunge kuhusu hilo soko la EAC ambalo mwezi Juni ndio litaanza. The time is now! Nchi inauzwa mko kimya halafu mnaanza kulalamika.
 
This is really disheartening. So sad. No decency at all? Most of Dar-es Salaam is already an eyesore. Now even the little remaining paradise is being raped!

I wonder if the late Mwalimu had any inkling of the pervasiveness of the dogs within when, in 1995, he joined the CCM campaign trail prompted by the fear of letting the country go to the dogs.
 
Serikali ya kifisadi inaendelea kufanya madudu yake. Si ajabu walionunua eneo hilo wakawa ni akina Rostam, Jeetu, Manji na Subhash kwa masharti kwamba hawatatoa michango ya mabilioni kwenye kampeni za uchaguzi wa 2010 mpaka wauziwe eneo hilo. Uongozi wa Nchi yetu umeoza.
 
Duh duh duh, Mkuu Pasco asante sana... Umetufungua wengi, hatukujua hili sakata lilitokea huko na wale wawakilishi wa wananchi 'walilibariki!!!', Ka 'nzi' pia...BIG UP..
 
Back
Top Bottom