Exclusive: Picha ya ndege yetu iliyoanguka na Taifa lisilo na shukrani!

Mwiba's counter argument shows JF maturity in debates. Great work!

Tatizo ni kwamba, ukishakuwa mseminari kama Mwanakijiji (Mwanakiji nisamehe kuingiza issue ya useminari, lakini nafikiri ni relevant hapa) unakuwa ushafundishwa kwamba kuwa grateful ni a high virtue kiasi kwamba katika issue kama hii mtu ana rally kwenye passionate uzalendo, nationalism etc na ku let down guards zinazotupa critical analysis. There's gotta be a reasonable, respecting and critical analysis inayoweza ku strike balance between an overly reverent outlook towards the military and one that is overly dismissive, both are unhealthy, the middle way is most desirable.I don't see Manakijiji striking that middle way.

Watu wakimuuliza umejuaje kwamba wanajeshi walifanya jitihada zote kuepusha maafa (swali ambalo binafsi nin li admire kwa sababu liko blunt despite utamaduni wetu wa kutokuwa critical kwa waliokufa) jibu lake ni kuchukua swala la wanajeshi kuangusha dege pembeni na wananchi kama kuepusha maafa kwa njia zote. Wakati wengine tunaweza kusema mtu mwenye principles na kujali maisha hawezi hata kurusha hilo kaburi la angani kutoka vita vikuu vya pili vya dunia.

Katika mida kama hii ni rahisi sana kuwa carried away na kuandika hadithi, hasa kama mtu ni mtunga riwaya maarufu kama Mwanakijiji, ku paint picture ya heroic death kama in some tragic Greek mythology etc.

Lakini ukweli unabaki wanajeshi wamekufa si kwa sababu ni mashujaa, bali kwa sababu ndege zetu mbovu. Nachelea kusema hawakuthamini maisha yao kwa kurusha hizi ndege mana pengine uchaguzi wao ulikuwa mdogo katika hili swala, lakini hili nalo linaweza kuwa swala kama tutaamua kuwa wakweli kabisa.

Mi hunipandishi midege ya jeshi kirahisi hata unilipe.
 
iyo ndege mbona kama inafanan na MIG 15, nilichek database ya ndege zetu hakuna data ya mig 15, mig tulizonazo na ambazo nyingi sio air worth ni mig 17, izo mig 15 kwa record was the famous fighter airplane ktk korean war, wamarekani walichapwa sana na izo ndege na wachina baadae walizicopy na wanaendelea na production yake! kuhusu ubora kwa kweli ndege zetu ubora uko chini sana, ndege za kivita zinatembea kuanzia sonic speed na kuendelea, ndege ikiwa mbovu ina hatari sana ya kuanguka au kupatat hitilafu, sasa hawa jamaa kwani walikua ktk mission gani? au mbwembwe tu?
 
I have many things to cry for..yesterday I cried for these two guys. I cried because I heard their story and understood that they knew what they were doing. Kama wote waliokula kiapo cha kufanya kazi zao wangefanya hivyo, hii nchi ingekuwa tofauti. Kuna wengine wangeliangusha ndege juu ya vichwa vya watu
 
...rather an attempt to split hairs, isn't it?!

We humjui huyu mjukuu wa Dilunga bin Kuhani, si bora ata angekuwa ana split hairs tungejua anatumia mkasi tu.

Huyu anataka kutumia energy ya ku split subatomic particles kama CERN without the advantage of having a research mind.Huyu jamaa ni loose canon yuko hapa ku distract threads zote na viroja vyake, we muangalie tu.

Robot si robot, Himmler si Himmler, basi ujanja mwingi mbele kiza tu.
 
Tatizo ni kwamba, ukishakuwa mseminari kama Mwanakijiji (Mwanakiji nisamehe kuingiza issue ya useminari, lakini nafikiri ni relevant hapa) unakuwa ushafundishwa kwamba kuwa grateful ni a high virtue kiasi kwamba katika issue kama hii mtu ana rally kwenye passionate uzalendo, nationalism etc na ku let down guards zinazotupa critical analysis. There's gotta be a reasonable, respecting and critical analysis inayoweza ku strike balance between an overly reverent outlook towards the military and one that is overly dismissive, both are unhealthy, the middle way is most desirable.I don't see Manakijiji striking that middle way.

Sijawahi kuingia seminari katika maisha yangu, not even for a visit, so umechagua mfano mbaya.

Watu wakimuuliza umejuaje kwamba wanajeshi walifanya jitihada zote kuepusha maafa (swali ambalo binafsi nin li admire kwa sababu liko blunt despite utamaduni wetu wa kutokuwa critical kwa waliokufa) jibu lake ni kuchukua swala la wanajeshi kuangusha dege pembeni na wananchi kama kuepusha maafa kwa njia zote. Wakati wengine tunaweza kusema mtu mwenye principles na kujali maisha hawezi hata kurusha hilo kaburi la angani kutoka vita vikuu vya pili vya dunia.

hapana, kwa sababu ulitakiwa kusikia mashuhuda wa jinsi gani rubani alijitahidi kukwepesha ndege isigonge magari yote hayo njiani. Au ulifikiria walikuwa wanataka kutua barabarani kwa ajili ya kufanya maonesho ya ndege katikati ya barabara?

Katika mida kama hii ni rahisi sana kuwa carried away na kuandika hadithi, hasa kama mtu ni mtunga riwaya maarufu kama Mwanakijiji, ku paint picture ya heroic death kama in some tragic Greek mythology etc.

kwanza ni mseminari na sasa mtunga hadithi!

Lakini ukweli unabaki wanajeshi wamekufa si kwa sababu ni mashujaa, bali kwa sababu ndege zetu mbovu.

Na ukiulizwa wewe umefikia vipi hitimisho kuwa sababu ndege "zetu ni mbovu" unaweza ukatupa any emperical evidence ya assertion yako hiyo?

Nachelea kusema hawakuthamini maisha yao kwa kurusha hizi ndege mana pengine uchaguzi wao ulikuwa mdogo katika hili swala, lakini hili nalo linaweza kuwa swala kama tutaamua kuwa wakweli kabisa.

Sidhani kama unajua kwa sababu ndege ni mbovu? Kwanini isiwe kosa la marubani?

Mi hunipandishi midege ya jeshi kirahisi hata unilipe.

Of course, lakini unazungumza kana kwamba una guarantee kuwa ukipanda ndege ya kisasa ambayo toka mwanzo haina matatizo basi ndio huwezi kupata ajali au kutokea uzembe. Well..nina mifano kadhaa ya kuonesha jinsi gani hoja hiyo si sahihi.
 
Mmeanza kwa kujihuzunisha, mkajifanya hamtaki kutania. Kumbe bora Serikali mnaosema wamekaa kimya.

Hiyo ni kuwaonyesha walalmishi kama wewe kwamba siyo kwamba sijui kwamba hili ni jambo la huzuni, lakini hata kwenye huzuni watu huona mambo yaliyo si ya huzuni.

Mtu ambaye anajifanya hataki kutania hapa ni wewe unayetuletea hypocrisy ya kuwa serious katika hili jambo, wakati huo huo unadistract thread kwenda kwenye trivials za ku split atoms hapa.

Watu kama nyie tunawabalasa tu na fake seriousnes yenu, ungekuwa serious wewe hata mazungumzo ya "mzaha" usinge ya acknowledge, kwa kuingilia katikati mazungumzo haya na wewe ushajipaka matope ya mzaha kama unavyoyaona wewe.

Huwezi kuwafanya watu mashine mwanahiyana wewe usiye na aibu kwa kujishauashaua hapa.
 
We humjui huyu mjukuu wa Dilunga bin Kuhani, si bora ata angekuwa ana split hairs tungejua anatumia mkasi tu.

Huyu anataka kutumia energy ya ku split subatomic particles kama CERN without the advantage of having a research mind.Huyu jamaa ni loose canon yuko hapa ku distract threads zote na viroja vyake, we muangalie tu.

Robot si robot, Himmler si Himmler, basi ujanja mwingi mbele kiza tu.
...namjua mtu anayesusia jf kwa kununa pale atakapobanwa na kufurumushwa. doesn't take long either. hamadi kibindoni.....!!!
 
iyo ndege mbona kama inafanan na MIG 15, nilichek database ya ndege zetu hakuna data ya mig 15, mig tulizonazo na ambazo nyingi sio air worth ni mig 17, izo mig 15 kwa record was the famous fighter airplane ktk korean war, wamarekani walichapwa sana na izo ndege na wachina baadae walizicopy na wanaendelea na production yake! kuhusu ubora kwa kweli ndege zetu ubora uko chini sana, ndege za kivita zinatembea kuanzia sonic speed na kuendelea, ndege ikiwa mbovu ina hatari sana ya kuanguka au kupatat hitilafu, sasa hawa jamaa kwani walikua ktk mission gani? au mbwembwe tu?[/QUOTE]
Kama ndio ndege zilizopo wangerusha ndege gani? Hawana hatia...kazi wanayofanya ni ya kiapo na utii ndio nguzo nambari moja jeshini. Ukiamriwa kufanya kitu yo take it as an order. Hawa ni mashujaa.They could abandon the plane to save their lives....I would rather say it is wrong to underestimate what these befallen soldiers have done
 
Sikutaka kutoa maoni yoyote kwa siku kadhaa nione kama watawala wetu wanatambua kuwa vifo vya wanajeshi wetu wakiwa kazini ni kitendo cha kishujaa wakati wote. Kinachoniudhi kuwa tunaishi bila kutambua mashujaa; yaani wale wanaojitoa maisha yao ili kuokoa wenzao.

Alipokufa yule mwanamama mjeshi kwenye ile ajali nyingine ya ndege ni watu jeshini zaidi waliona kitendo hicho ni cha kishujaa na labda mimi ni mtu pekee niliyeandika kutambua damu hiyo ya binti wa kitanzania ikimwagika. Nikiwa na ndugu waliolitumikia JWTZ kwa uadilifu na wengine kumwaga damu katika utumishi najikuta kila wakati ninasisima ninaposikia vitu kama hivi vinatokea.

Habari hii ilivyoripotiwa imeripotiwa pasipo kuelewa kwa njia rahisi tu kuwa Rubani Meja Cuthbert Leguna na Luteni Andrew Kijangwa waliamua kufanya kitu cha kujitoa mhanga kwa kukwepesha ndege hiyo kuangukia makazi ya watu na kujaribu kutua barabarani. Na hata hapo barabarani walipoona kuna basi la Simba Mtoto na gari la Watalii huku ndege yao ikienda kuanguka walijitahidi kulikwepesha na katika kufanya hivyo wao pekee ndio wamekufa katika tukio hilo la kusikitisha lakini lenye kila chembe ya ushujaa.

Taifa lisilo na shukrani linachukulia tu kuwa ni ajali na "ajali haina kinga" kumbe wapiganaji wetu wamekinga ajali kubwa zaidi kwani leo tungekuwa na kilio kikubwa zaidi. Sijui kama Rais wenu, waziri mkuu wenu, au hata wabunge wenu wameonesha shukrani yoyote Bungeni au mahali pengine popote kwa kitendo hiki cha kishujaa. Yaani, waliona ni bora wao wawili wafe kuliko makumi au mamia kuangamia!

Nikiwa nimelengwa na machozi na nikitambua uzalendo huu wa hawa vijana wapiganaji ambao licha kupoteza ndugu, baba, kaka na watoto katika familia zao wamepoteza vile vile hazina kubwa ya ujuzi na utaalamu katika Jeshi letu, utaalamu ambao taifa linatumia kiasi kikubwa sana kupata. Wakati ndege ni rahisi kununua (wakiacha ufisadi kidogo) maisha yao na uzoefu wa ujuzi wao hauwezi kurudishwa kamwe.

Ninatoa shukrani kutoka familia moja ya kijeshi kwenda familia nyingine, Ninawapigia saluti wapiganaji hawa na kusema asante kwa kitendo chao cha kizalendo na kishujaa kupita kiasi. Wakati mafisadi wenu wanaendelea kutanua na kubishana nani ale nini zaidi hapa leo wanalala mautini wale ambao labda hata baada ya siku chache hawatakumbukwa, familia zao zitarudishwa kijijini, watoto wao watakosa elimu n.k n.k Laiti tungejua kusema asante kwa kafara hii ya utumishi.

Asante Meja Leguna
Asante Luteni Kijangwa

Majina yenu yatabakia moyoni..

Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania

Mlale salama enyi wana wa Tanzania, mlale salama mashujaa!!

Saluti!

what the hell is this? MV BUKOBA je?
 
Mwanakijiji,

Sijawahi kuingia seminari katika maisha yangu, not even for a visit, so umechagua mfano mbaya.

si lazima kuingia seminari ili kuwa mseminari, kwa matendo na maneno yao utawajua.Unaweza kubobea seminarini maisha yako yote na usiwe mseminari, na ukawa hujanusa hata harufu ya seminari, licha ya kutia mguu seminarini, lakini ukawa mseminari.Sema jingine, hii siyo counter argument ya ku dispute useminari kama philosophy/ outlook on life.

hapana, kwa sababu ulitakiwa kusikia mashuhuda wa jinsi gani rubani alijitahidi kukwepesha ndege isigonge magari yote hayo njiani. Au ulifikiria walikuwa wanataka kutua barabarani kwa ajili ya kufanya maonesho ya ndege katikati ya barabara?

Jitihada ya kwanza kabisa kwa rubani kuhakikisha ajali haitokei, akiambiwa kurusha dege la toka enzi za Harry Truman na Korean War huko ambalo rightfully linatakiwa kuwa makumbusho ya kijeshi, ni kukataa kulirusha kwa sababu by default dege hili kuu kuu ni kaburi la angani kama nilivyosema hapo mwanzo.Sasa hawa mashujaa wanaokubali kuendesha midege hii mikuukuu utasemaje wamefanya jitihada zote za kuepusha maafa wakati kwa kukubali kurusha midege hii tu washakubali maafa waziwazi? Huwezi kuniambia wamechukua tahadhari zote.

kwanza ni mseminari na sasa mtunga hadithi!

Na vyote huwezi kuvikanusha.

Na ukiulizwa wewe umefikia vipi hitimisho kuwa sababu ndege "zetu ni mbovu" unaweza ukatupa any emperical evidence ya assertion yako hiyo?

Actually ni zaidi ya mbovu, haziko airwothy by virtue of being air dinosaurs. Wanaanga wetu wanaweza kutumiwa nchi nyingine kutoa masomo ya military history maana naweza nisishangae nikiambiwa teknolojia za kurusha hizi ndege hazitumiki tena kwa ndege za sasa.

Ndege za WWII, wahandisi wa ukarafati wa kichina, halafu apologists wa serikali wanadai swala si ubovu wa ndege.

Hatari!

Sidhani kama unajua kwa sababu ndege ni mbovu? Kwanini isiwe kosa la marubani?

Kwa sababu ndege hazikutakiwa kuwa hewani to beginning with, by virtue of their ancient birthdate.

Of course, lakini unazungumza kana kwamba una guarantee kuwa ukipanda ndege ya kisasa ambayo toka mwanzo haina matatizo basi ndio huwezi kupata ajali au kutokea uzembe. Well..nina mifano kadhaa ya kuonesha jinsi gani hoja hiyo si sahihi.

Wapi nimesema au kutoa impression kwamba ndege ya kisasa haipati ajali?

Hii ndiyo mentality ile ile ya "ndege zote zinaanguka, mpya, za zamani, zilizokarafatiwa, zisizokarafatiwa, kwa hiyo hamna guarantee hata tikikarafati kwamba ndege hazitaanguka, kwa hiyo hamna hata point kukarafati, tupande ndege tu na kuomba mungu, kitakachotokea kitatokea tu, kazi yake haina makosa"

Ikitokea ajali, "kazi ya mungu haina makosa"

Unazungumza kama huelewi risk reduction? Wewe una insurance yoyote? Insurance inakupa guarantee yoyote kwamba ajali au dharura haitakukuta? Lakini kwa nini watu wanachukua insurance regardless ya kutokuwa na guarantee hii.

Unafunga mkanda kwenye gari wewe? Kufunga mkanda kunakupa guarantee kwamba ajali haitatokea? Kama hakukupi kwa nini unaendelea kufunga mkanda?

Unaandika kama huelewi umuhimu wa safety standards na sasa una dismiss watu wanao sisitiza safety standards kwamba "wanaongea kama kuongeza safety standards kutatoa guarantee ya kutokuwepo kwa ajali"

Let me tell you something, the only guarantee in life is that there is no guarantee, and even that is not safely guaranteed.
 
Lol...yaani hapo umeniwahi kiaina. Kwa kweli kuna watu hawajui kujificha kama lengo lao ni kutojulikana.

Inabidi tuisake tena thread ya Dk.Masau....

The guy is unnaturally bitter. It takes only two sentences for effect of the unknown venom to be noticed and traced back to the actual species. What a distraction!
 
The guy is unnaturally bitter. It takes only two sentences for effect of the unknown venom to be noticed and traced back to the actual species. What a distraction!

Yeah, while I understand the importance of thinking critically, outside the box or even being a reasonable contrarian, this guy is ttoo much, hata kwangu mie ambaye mara nyingine huenda against the grain panapohitajika.

Kwa huyu jamaa, yeye ni kama vile ni lazima aende against the grain kila mara, akikosa kitu cha maana ku object atakusema hata kwa font uliyotumia.

Yaani kumkuta jamaa yuko positive ni vigumu sana, ni kama vile ameambiwa atalipwa kwa kila negative comment atakayoitoa, na akiwa positive atakuwa penalized.

Yaani hata kwangu mie ninayevalue independency na kuwa contrarian when it is called for, naona huyu jamaa haelewi kabisa principle ya "point of diminishing returns" kwa contrarians. Hata H.L Mencken, that godfather of modern day critics alijua hili.

Hata mtu anayefanya mazoezi ili kujenga mwili wake uwe na nguvu zaidi, inafikia hatari mazoezi yanapozidi kiwango kinachotakiwa anakuwa anatishia maisha yake wmenyewe na anaweza kufa kwa mazoezi.

Huyu jamaa kazidisha mpaka anataka kujiua mwenyewe kwa kuondoa credibility yake, atakuwa kama yule mtoto aliyekuwa analia wolf, wolf, siku akija na objection genuine watu tutamwona "Tindikali bin Dilunga wa Kuhani Mkuu" tu huyo, ni kawaida yake.

Kumbe kuna kitu valid anataka kutuambia.
 
NI moyo wa kijasiri na kujitolea mno kuendesha ndege kuukuu za kijeshi kama hizi. Kwa mkufunzi ni kama kuwambwa msalabani kwa ajili ya maisha ya milele ya wenye dhambi!. R.I.P all deceased PSNS!.
 
Kiranga.. usichukulie kwamba napuuzia hoja zako ambazo ni za msingi mno; nilichoandika mimi hapa kinahusiana na vitendo vya kishujaa ambavyo mashujaa hawa walichukua kuepusha majanga makubwa zaidi. Hainisadii mimi kwa wakati huu kutokutambua sadaka kubwa ya kitendo chao hicho. Labda hujui nidhamu ya jeshi ilivyo lakini mwanajeshi siyo mtu anayeweza kusema "hapana" kirahisi rahisi tu. Na ndio sababu wanajipeleka vitani kupambana.

Meja anatakiwa amfundishe rubani kwa ndege ambayo ndiyo serikali yake inasema inayo na sifa zote za kiufundi ziko sawa. Anatakiwa aseme "hapana sitaki hadi mnipe ndege mpya". Hakuna mwanajeshi anayeweza kufanya hivyo duniani. Ndio maana hata US iliwapelekwa wapiganaji wake vitani bila kinga za kutosha ya mabomu ya kushtukiza ya kutegwa njiani. Wale wapiganaji wasingeweza kusema "hatuendi vitani hadi tupate magari yenye amour ya kiasi hiki au kile" hilo haliwezi kuwa jeshi.

Hata hivyo nitairudia point yako kwa urefu zaidi na itabidi nivunje mwiko kwa sababu pamoja na ukweli huo lakini taifa letu haliwezi (kama nilivyosema hapo juu) kuendelea kulinda utajiri wake kwa mishale! - nadhani you missed what I really meant there.
 
Moja ya matatizo makubwa tuliyo nayo nchini kwetu ni hili la watu kutokuwa na integrity.

Watu wanajifanya kwamba wako victims of circumstances, kwamba kuna natural forces zilizo kubwa kuliko wao, kuna mabosi wamewataka wasaini mikataba na hawakuweza kukataa, kuna nidhamu ya kijeshi isiyoruhusu maswali ambayo iliwataka warushe hizi ndege na wasingeweza kukataa.

Guess what? This notion is wrong.

Ni kweli mwanajeshi hatakiwi kukataa amri, lakini si kweli kwamba mwanajeshi mwenye integrity hawezi kujiuzulu kazi yake, even at the risk of being court marshalled, kama anaona analazimishwa kufanya kitu against his will/ sense of integrity.Ndiyo maana hata utetezi wa the Nuremberg trials kwamba "sisi tulikuwa foot soldiers tu, tulipokea maagizo kutoka juu" haiwezi kusimama leo.

Mimi naendelea ku maintain, kwa mtu mwenye ushujaa hasa na integrity ya hali ya juu hawezi kukubali kurusha hizi ndege kwani ni hatari, na kama jeshi halina ndege nyingine ataondoka kwenda kutafuta kazi kwingine, na ikibidi anakuwa hata whistleblower kueleza uchakavu huu wa ndege.

Tunahitaji whistleblowers zaidi, tunahitaji watu wenye integrity zaidi, tunahitaji watu ambao hawaogopi kusema ukweli kwa kufikiri kitumbua kitaingia mchanga au kibarua kitaota nyasi, tunahitaji watu wanaoweza kumwambia hata rais, rais sijui kama nikikuambia ukweli kazi yangu nitakuwa nayo kesho, au sijui kama nitakuwa huru, lakini ukweli ni huu, ndege zetu mbovu na ni hatari kwa wananchi na wanajeshi wetu, na mimi siwezi kurusha ndege hizi.

Hili ni tatizo si katika swala hili tu, hili tatizo partly ndilo linalosababisha mikataba mibovu, watu wanategeana, bosi anaamrisha rushwa kwa kutegea wa chini yake wakubali hivyo yeye asiwe na sole responsibility, wa chini wanakubali kwa kutegea kwamba ni amri ya bosi na hawana jinsi.

Guess what, ukishazaliwa binadamu tu ushakuwa na jinsi.Hata hao wanyama mwitu wengine tumeshindwa kuwa domesticate widely, itakuwa sisi binadamu?

Kusema kwamba hawana jinsi, wamepewa amri kutoka juu, nidhamu ya kijeshi hairuhusu dissent etc ni kutukana intelligence zao.Hawa watu wanarusha ndege, they can't be that stupid.
 
Back
Top Bottom