Exclusive Interview - Mada: Mahusiano ya kimapenzi sehemu ya kazi

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
17,647
14,793
Salamu wakuu!!

Naamini siku imekwenda vyema.

Nawakaribisha sana kwenye interview yetu ya leo, kwa siku kadhaa sijaja hewani, leo tunakuja na mada kama ilivyo hapo juu. Tutajadili kwa kina mahusiano ya kimapenzi sehemu ya kazi na impact yake!

Je, mahusiano ya aina hii yanaongeza au yanapunguza ufanisi wa kazi?

Mgeni wetu leo ni atoto!

Host ni mimi mwenyewe.

Wadau wengine mnaweza mkatizama tu mjadala then pale mwishoni nitawapa nafasi ya kuuliza maswali ambayo yatakuwa hayajaulizwa.

Karibuni sana!
 
Sawa, lakini si kuna mahusiano ambayo yanaweza kuzaa ndoa pia? Kuna ubaya gani ukikutana na mume wako sehemu unayofanyia kazi?
Ni kweli waweza kutana na mwenza wako sehemu yoyote, ila kwangu sehemu ya kazi ni kwaajili ya kazi tu.
Kama tutakutana sehemu ya kazi ila tukawa katika sehemu za kazi tofauti, hapo sawa.
Ila katika ofisi moja ni big NO.
 
Ooops!! Hiyo restriction kali mno...
Atoto nilisahau kukuuliza hili swali...
Nini status yako kwa sasa kati ya hizi hapa chini, hii itasaidia kukuuliza maswali mengine ya msingi kabisa.
1. Umeolewa
2. Una mchumba
3. Una boyfriend
4. Non of the above
 
Sawa...
Turudi kwenye hiyo dhana ya mahusiano sehemu ya kazi, we umesema huwezi na hupendi!!
Hii ni kwa ajili ya kazi unayofanya au hata kama umgekuwa unafanya kazi nyingine msimamo wako ungekuwa huu huu?
 
Huo ni msimamo wangu hata kama ningekuwa nafanya kazi tofauti na nifanyayo sasa.
 
Back
Top Bottom