Exclusive interview: Halima Mdee kuhusu mahusiano yake

Status
Not open for further replies.
Na mimi I was about to connect. Sasa unaonaje ukimtafuta maana naona mna mawazo na mitizamo sawa. Maana akizaa na wengine hawakawii kumletea usumbufu. Na utakuwa umesaidia jamii maana hawa wadada "nataka kuzaa tu" ni mabingwa wa kuzaa na waume za watu na kuharibu ndoa za watu!

Umeona eeeh! hata hivyo sijajua unataka nifanyeje unaposema nitakuwa nimesaidia jamii kivipi yaani? na suala la kuzaa na waume za watu manake nini? au unamaanisha wanaume kama tools and then kuna watu wanawamiliki sio? Tafadhari nisaidie kumtafuta
 
Yatoke wapi? Kama wapo ni mmoja kati ya kumi. Mtoto anashuhudia mama anaingiza kila aina ya mwanaume ndani what do you expect. Si mara kumi baba anayejinyea kwani watoto wataiga kunya?

Hapa bi mkubwa he sorry Nyumba kubwa naona kweli uko obsessed na ndoa! yaani unaolewa na mwanaume wa namna uliyoitaja hapa (samahani siwezi kuandika hilo) halafu unasema watoto watakuwa na maadili? uoni kwamba hata watoto wankuwa wameambukizwa ulevi tangia tumboni mwako kwakuwa mimba iliwekwa jamaa akiwa nzwii?! teh!
 
I just like the lady na jinsi anavyojiamini. Ni kati ya wanawake wachache TZ wenye upeo. Haya ni baadhi ya majadiliano kati yake na Dina Marios.

Dina Marios(dm): TAMKO LA MHESHIMIWA HALIMA MDEE KUHUSU MAHUSIANO YAKE...

Mheshimiwa Halima James Mdee mbunge wa kawe amezaliwa Mwaka 1978 ana shahada mbili za sheria moja aliipatia katika chuo kikuu cha dare s salaam nay a pili katika chuo kikuuu cha cape town Afrika ya kusini.

Kitaaluma ni mwanasheria na wakili wa mahakama kuu kutokana na kazi za kisiasa taaluma yake ya kisheria anaitumia kwa muda mchache sana.

Mahusiano yake ya kifaragha....

Halima hajaolewa wala hana mchumba ila anatamani sana kupata mtoto na anapanga kupata mtoto hivi karibuni hata kama atakuwa bado hajaolewa.Anasema hajapata mtu ambae anasifa anazozitaka yeye ili kuishi nae mpaka uzeeni kama mume na mke yeye ndoa anaona ni jambo kubwa la commitment ya milele hivyo anahitaji mtu sahihi na si kukurupuka.'

'Kuna watu wapo kwenye ndoa lakini ni wezi tu wanawake wana wanaume wengine nje ya ndoa na wanaume kadhalika wana wanawake wengine nje ya ndoa.Sasa kiapo mlichokila kwa shekhe au padre kina tija gani?kwa nini uwe katika ndoa iliyojaa uongo??''alisema.

Halima anahitaji mwanaume anaejiamini, mtu asimuone yeye ni mbunge na msomi akamuogopa mapenzi ni kitu cha ajabu sana hayachagui cheo, ukubwa wa umri wau muonekano kwa nini mwanaume atishwe na cheo chake? Mwanaume atakayempenda na kumkubali yeye na asitishwe na majukumu aliyonayo kiserikali huyo ni mtu sahihi kwake.

Ndoa inapangwa na mungu na kama mungu amempanga mume fulani kwa ajili yake atakuja.Na wakati wote ambao unasubiri unatakiwa uwe unaishi katika misingi ya kujiheshimu.Wanaume wamejaa sana ila sio kuokoteza kisa unatafuta mtu sahihi.

God bless you Halima, usikonde Mungu kakuandalia dume la nguvu ili mjenge familia bora, wanaume mnaojiamini mchumba huyo.
 
on contrary,halima hajiamini linapokuja swala la mwenza,haamini km atapata mtu atayeweza kuwa faithful maisha yake yote...pole halima anza kufanyia kazi hio fear uliyonayo ya kupata mume faithful kisha utaanza kuyaona maisha katika mwanga bora(positively):mod:
 
hakuna cha kujiheshimu hapo, sasa kama unazaa na mtu ambaye si mume wako means unaiba wa mwingine. so in the same boat of wezi..
 
hakuna cha kujiheshimu hapo, sasa kama unazaa na mtu ambaye si mume wako means unaiba wa mwingine. so in the same boat of wezi..

(red)Some point here!

Unapanga vipi kupata mtoto na mtu ambaye hutoolewa naye?, AU MUME WA MTU?, au mpenzi wa mtu?...
Mwanaume yeyote atajiamini kama atakuwa yuko safi mfukoni bana!...Tofauti n hivyo unabaki kutumwa na kutumika hovyo!
 
I just like the lady na jinsi anavyojiamini. Ni kati ya wanawake wachache TZ wenye upeo. Haya ni baadhi ya majadiliano kati yake na Dina Marios.

Dina Marios(dm): TAMKO LA MHESHIMIWA HALIMA MDEE KUHUSU MAHUSIANO YAKE...

Mheshimiwa Halima James Mdee mbunge wa kawe amezaliwa Mwaka 1978 ana shahada mbili za sheria moja aliipatia katika chuo kikuu cha dare s salaam nay a pili katika chuo kikuuu cha cape town Afrika ya kusini.
Kitaaluma ni mwanasheria na wakili wa mahakama kuu kutokana na kazi za kisiasa taaluma yake ya kisheria anaitumia kwa muda mchache sana.

Mahusiano yake ya kifaragha....

Halima hajaolewa wala hana mchumba ila anatamani sana kupata mtoto na anapanga kupata mtoto hivi karibuni hata kama atakuwa bado hajaolewa.Anasema hajapata mtu ambae anasifa anazozitaka yeye ili kuishi nae mpaka uzeeni kama mume na mke yeye ndoa anaona ni jambo kubwa la commitment ya milele hivyo anahitaji mtu sahihi na si kukurupuka.''Kuna watu wapo kwenye ndoa lakini ni wezi tu wanawake wana wanaume wengine nje ya ndoa na wanaume kadhalika wana wanawake wengine nje ya ndoa.Sasa kiapo mlichokila kwa shekhe au padre kina tija gani?kwa nini uwe katika ndoa iliyojaa uongo??''alisema.
Halima anahitaji mwanaume anaejiamini,mtu asimuone yeye ni mbunge na msomi akamuogopa mapenzi ni kitu cha ajabu sana hayachagui cheo,ukubwa wa umri wau muonekano kwa nini mwanaume atishwe na cheo chake?mwanaume atakae mpenda na kumkubali yeye na asitishwe na majukumu aliyonayo kiserikali huyo ni mtu sahihi kwake.
Ndoa inapangwa na mungu na kama mungu amempanga mume fulani kwa ajili yake atakuja.Na wakati wote ambao unasubiri unatakiwa uwe unaishi katika misingi ya kujiheshimu.Wanaume wamejaa sana ila sio kuokoteza kisa unatafuta mtu sahihi.

God bless you Halima, usikonde Mungu kakuandalia dume la nguvu ili mjenge familia bora, wanaume mnaojiamini mchumba huyo.

Kama kweli amenukuliwa vema, basi hapo kwenye bold if you read between the line utaona a frustrated women in terms of relatioship ya ke/me anayehitaji healing before hajaingia mahusiano mapya. Kwana yuo tayati kuzaa na mtu yeyote alafu anatafuta mme mwaminifu! hahahahaaaa kweli mapenzi hayajali cheo ni ugonjwa uanosumbua wengi. Mheshimiwa nadhani unahitaji msaada mkubwa sana ili uwezu ku-venture kwenye ndoa
 
Haya, Maisha ya wasomi hayo, Kumbe kusoma saana pia kuna shida zake!!!!!
 
Haya, Maisha ya wasomi hayo, Kumbe kusoma saana pia kuna shida zake!!!!!
Sasa hapo shida ya usomi na kutokuolewa kwa halima vinahusiana vipi?wanawake wengi tu waliosoma na wasiosoma hawajaolewa,kwa nini kila kitu kisingiziwe elimu?haya ni mawazo hasi ya kutaka kuwakatisha tamaa watu wasisome...
 
Tatizo bongo mwanamke akiwa kasoma sana halafu ana position kubwa kama ya Halima wanaume wengi wanakula kona, hii yote ni kwa sababu wanaogopa mikiki ya wanawake wasomi. Uamuzi wa Mh.Halima wa kutafuta mtoto bila kuolewa nauunga mkono manake ndoa zenyewe za siku hizi ni manyanyaso. Bora azae then awalee wanae, kila la kheri Mh. Halima.

Kupata mwenza bora wa maisha ni shughuli sana, hasa unapokuwa mwanamke mwenye power.
 
Haya, Maisha ya wasomi hayo, Kumbe kusoma saana pia kuna shida zake!!!!!

Si kweli hayo sio maisha ya wasome, mbona wasomi wengine wameo/olewa na wanaishi vizuri. Muda wake haujafika kama ambavyo wapo wengi ambao hata darasa la kwanza hawakugusa lakini bado kuolewa. Wenye PHD wanaolewa ije iwe Digrii ya sheria? Agalia tabia ya mtu binafis pia inaweza kusababisha wachumba wamkimbie na sio kujumuisha wasomi wote halafu ukawakatisha tamaa watu kusoma. Kama mtu anawaza kuzaa kabla ya kuolewa, halafu anapinga wanaenda nje ya ndoa unadhani kuna mke mwema hapo? Maana kwa jinsi maisha yalivyo, kama atazaa kabla ya ndoa ni lazima atakuwa amezaa na mume/mchumba au mpenzi wa mtu mwingine!!!!!
 
Tatizo bongo mwanamke akiwa kasoma sana halafu ana position kubwa kama ya Halima wanaume wengi wanakula kona, hii yote ni kwa sababu wanaogopa mikiki ya wanawake wasomi. Uamuzi wa Mh.Halima wa kutafuta mtoto bila kuolewa nauunga mkono manake ndoa zenyewe za siku hizi ni manyanyaso. Bora azae then awalee wanae, kila la kheri Mh. Halima.

Kupata mwenza bora wa maisha ni shughuli sana, hasa unapokuwa mwanamke mwenye power.

Anatafuta mtoto kutoka kwa nani kama anachukia ke/me wanaojinafasi nje ya ndoa, maana kama anapanga kupata mtoto lazima apate kwa mume/mchumba au mpenzi wa mtu.
 
Mbona mambo ya Mdee yanajadiriwa sana humu ndani kuliko wenzake wa kike,ama Mdee ndo case study?mnavyozidi kumuongea humu ndani mnamzidishia stress,tumwache atafute mwenyewe na mahusiano ni suala bnafsi sana (intimate affair)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom