Exclusive interview: Diamond na Vanessa Mdee baada ya kupata tuzo

Stv Mkn

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
328
273
Hii interview imefanyika leo 7/31/2014

AZUNGUMZIA KUFANYA VIDEO NJE YA NCHI:

''Unajua madongo mengi yanayorushwa kuhusu wasanii wa bongo kufanyia video nje najua narushiwa mimi ila naamua kukaa kimya tu''...........

Anaendelea..." Mie siwezi kufanya video na madirector wa kibongo kwa sasa kwa sababu ni wazinguaji sana....Tatizo sio quality inayonikimbiza bongo ila utendaji wa kazi haswa ndio tatizo kubwa, hawathamini wateja wao(directors).

Mtu unamlipa pesa ila kufanya kazi inabidi umbembeleze,Nimeshawahi kususa video mbili kwa director nikiwa nimeshazilipia kila kitu, baada ya kuzifatilia nakuishia kuzungushwa miezi minne.

Ni video ya 'Nimpende nani na Lala salama', Nimeshawahi kumlipia ticket ya ndege director twende tukashoot South Africa na akaishia kunizingua.
Mtu unaamshwa na director saa kumi na mbili asubuhi ufike location, unafika unamsubiria yeye anatokea saa 4.

MaDirector wa nje wanakutreat mpaka unaona thamani yako kama msanii, pia wanaangaikia mpaka kukuconnect na media kubwa. Hapa kwetu ukisharecord unaangaika mwenyewe na bado mtu anakutreat kama anakupa msaada wakati pesa yote aliyotaka umempa''.

Azungumzia Changamoto:

''Changamoto kubwa ni kupata lawama, ujue kwa sasa nina marafiki wengi na najuana na watu wengi sasa kumridhisha kila mtu inafika kipindi nashindwa.

Unakuta unapata maombi mengi mfano ya interview mfano, sasa ratiba yangu ni tai sana ata muda wa kupumzika nakosa na ninatakiwa uku na uku, nikikosa uku unakuta mtu anajisikia vibaya anaona umeanza kumdharau na ata nafasi ya kumwelewesha nashindwa Dah hicho kitu uwa kinaniumiza sanakuliko vyote sababu mie sipendi kumuudhi mtu anayenisapot ila kama binadamu sometimes nashindwa you know msayn! ''.

'' Changamoto nyingineyo, nina watu wanaonpenda na kuniamini sana na wanaamini sitowaangusha ata siku moja. So wanafanya nifanye kazi kwa nguvu nyingi nisiwaangushe''........Anaendelea.''

Unakuta mtu ni shabiki wako mnakutana airport,umechoka kinoma unawaza kupumzika tu, anatokea anaomba mpige picha, inabidi ukubali na utupie na tabasamu japo upo hoi''

Aulizwa na Vanessa kama ana uwezo wa kurap, anaomba apewe beat achane....apewa beat ya laini aikataa anaomba beat ngumu........Anaonyesha uwezo wa kurap pia.


MENGINE ALIYOONGEA

'' Unajua muziki wako kwa sasa ukipita Nigeria ndio umepita Africa''.

'' Passport yangu ya pili inakaribia kuisha hapa nilipo nina visa kibao mkononi...unajua nasafiri sana ninachoka lakini siwezi kukaa chini inabidi nitumie huu wakati''

'' Wategemee collabo ya nyingi sana, zingine ni za nje ya Africa....nikitoka hapa naenda studiio kurekodi nyimbo ya collabo na Case wa Nigeria ni nyimbo yake''

'' Idea ya video ya Mdogomdogo ilianzia kwa Adam Kuambiana, baadae tukaiboresha mimi na Wema''

'' Nimemuona Rihana LIVE, alikaa nyuma yangu siku iyo.....yani nilikuwa sielewi chochote kugeuka nyuma namuona mtu kama Rihana, sikuamini ikabidi nigeuka zaidi ya mara mbili uku najiuliza hivi uyu si Rihana uyu?

Ikabidi nipotezee kama sijashtuka vile,ila kwa kweli kushangaa sio siri hakuniishi sababu vitu vingi tulikuwa tunavisikia tu nakuviona vya ajabu''
 
Kuna vitu amezungumza kwa mara ya kwanza nimemkubali yuko very honest na sana sana fact za utendaji wa kibongobongo ......
 
Lazima ashangaee wee hata kama ni mimii,tuseme tu ukwelii,kumbe wema nae msaniii khaz!!!
 
nampongeza sana diamond,,, nimetoka shuhudia ngoma yake kama dk 7 zilizopita on MTV BASE ,,,, SPANKING NEW ya MDOGO MDOGO...

hongera kwake
 
nampongeza sana diamond,,, nimetoka shuhudia ngoma yake kama dk 7 zilizopita on MTV BASE ,,,, SPANKING NEW ya MDOGO MDOGO...

hongera kwake

Mie nimeiona BUMBUM jana kwenye Fresh hits ya STV MUSIC......STV MUSIC wanapiga nyimbo zenye viwango vya kimataifa tu.
 
Lazima ashangaee wee hata kama ni mimii,tuseme tu ukwelii,kumbe wema nae msaniii khaz!!!

Mhh dadangu ushasahau kuwa Wema ni msanii........

10590651_1527912780760880_7200927843890600257_n.jpg
 
Mie nimeiona BUMBUM jana kwenye Fresh hits ya STV MUSIC......STV MUSIC wanapiga nyimbo zenye viwango vya kimataifa tu.

nimeutafuta huu uzi haraka baada ya kuona samuwea ndugu daimondi kasnapu shut sijui shot sehemu hii...

hmm nina wasiwasi na thread/comment za watu kujifagilia wenyewe humu...
 
nimeutafuta huu uzi haraka baada ya kuona samuwea ndugu daimondi kasnapu shut sijui shot sehemu hii...

hmm nina wasiwasi na thread/comment za watu kujifagilia wenyewe humu...

Sijakuelewa ndugu yangu.....ebu funguka zaidi.
 
Kujituma ni vizuri.
Mitanzania haiaminiki hata kidogo kwenye kazi
 
Ndo maana watu wanasema ukileta ushikaji kwenye kazi kazi haifanyiki ukileta undugu kwenye biashara unafilisika safi sana diamond kwa misimamo yako utafika mbali
 
Diamond namkubali sababu nimkweli na anasimamia humohumo..waTZ Tukiacha chuki kwa wenyekupiga hatua kuyaelekea maendeleo tutafika mbalisana..
 
Hilo tatizo la directors wa kibongo ni ugonjwa wa wabongo wengi sana.
Hata mama muuza chapati akiona anapata wateja wengi huwa haonyeshi kujali wateja mpaka pale wateja watakapoanza kumkimbia.
 
Back
Top Bottom