mchajikobe
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 2,652
- 1,238
Nenda kapime ujue afya yako na uondokane na huo msongo wa mawazo!!Kuna demu alikuwa girlfriend wangu zamani, majuzi kaonekana kitaa anahamasisha masuala ya UKIMWI na amejitangaza laivu kuwa na yeye pia anayo ngoma. Washkaji kibao wanaelewa nilikuwa namega. Lakini mie siku zote nimetumia kondomu. Sasa tangu amejitangaza huyo demu napigiwa simu na sms kibao za kunipa pole kama vile nami pia nina ngoma! Kwa kadri ninavyojua ngoma inaenea kwa kufanya ngono zembe, na mimi sikufanya hivyo hata siku moja.
Najua hata nikitangaza redioni kuwa mi sina ngoma watu hawataniamini, na sasa naona hata mchumba nitakosa, maana hii habari ni mbaya kinoma!
Nishaurini wakubwa. Naomba msinishutumu mnaposhauri, sikupanga yatokee kama yalivyotokea. Nifanyeje niaminike? Tabia flani mbaya nilizokuwa nazo zamani zote nimeacha, lakini naona hii ya huyu demu kujitangaza itatibua kila kitu!